Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə14/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   ...   33

Mafanikio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Katika Awamu ya Kwanza ya Uboreshaji idadi ya Wapiga Kura waliokadiriwa kuandikishwa ilikuwa 2,690,000, Tume ilifanikiwa Kuandikisha Wapiga Kura 2,079,378 ambayo ni asilimia 77.3 ya makadirio.
Katika Awamu ya Pili idadi ya Wapiga Kura waliokadiriwa kuandikishwa ni 1,750,000 na Wapiga Kura walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura walikuwa 1,686,100 ambao ni sawa na 96.3% ya makadirio.
    1. Changamoto Zilizojitokeza


Pamoja na mafanikio yaliyopatikana ya kuandaa Daftari lililokuwa sahihi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu, zilikuwepo changamoto mbalimbali katika kila hatua ya Uboreshaji. Baadhi yake ni pamoja na:-


        1. Wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Awamu ya Kwanza, Tume ilipata changamoto zifuatazo:-

          1. Baadhi ya Wapiga Kura kujiandikisha zaidi ya mara moja.

          2. Baadhi ya Wapiga Kura majina yao kutoonekana kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

          3. Kutojitokeza kwa baadhi ya Wapiga Kura waliotarajiwa kusahihisha taarifa zao za alama ya dole gumba na picha.

          4. Wananchi wengi hawakutoa taarifa za jamaa zao waliofariki.




        1. Wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili Tume ilipata changamoto zifuatazo:-

          1. Uboreshaji kutokamilika kwa wakati.

          2. Ongezeko la Watu wengi zaidi ya ilivyokadiriwa kujitokeza

kubadilisha Taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Miji.

          1. Vifaa vya Uboreshaji kuharibika mara kwa mara.

          2. Ugumu wa upatikanaji wa taarifa za Wapiga Kura

waliofariki ili waondolewe katika Daftari.

          1. Wapiga Kura kuboresha taarifa zao zaidi ya mara moja

katika Vituo tofauti.

          1. Baadhi ya Waandishi Wasaidizi kutokuwa makini katika

kujaza Fomu na Kadi za Wapiga Kura.

          1. Wapiga Kura wengi kutokwenda kukagua taarifa zao

wakati wa kuweka wazi Daftari katika Vituo vya Uboreshaji.

SURA YA NNE




UTEUZI WA WAGOMBEA NA KAMPENI ZA UCHAGUZI

    1. Ratiba ya Uchaguzi Mkuu


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza Ratiba ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2010 kama ifuatavyo:-

      1. Uteuzi wa Wagombea tarehe 19 Agosti, 2010.

      2. Kampeni za Uchaguzi kuanzia tarehe 20 Agosti, 2010 hadi tarehe 30 Oktoba, 2010.

      3. Siku ya Uchaguzi tarehe 31 Oktoba, 2010.
    1. Uteuzi wa Wagombea

Uteuzi wa Wagombea wa Urais, Ubunge na Udiwani ulifanyika katika hatua mbili. Hatua ya kwanza ilikuwa ni uteuzi ndani ya Chama ambapo kila Chama cha Siasa kilitumia utaratibu wake wa kuwapata Wagombea. Uteuzi katika hatua ya pili, ulifanywa na Mamlaka za ngazi mbalimbali za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutegemeana na aina ya Uchaguzi.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliweka utaratibu wa kupokea Fomu za Uteuzi. Siku ya Uteuzi inapangwa na Tume kwa ajili ya Wagombea kuwasilisha rasmi Fomu za Uteuzi kabla ya saa kumi alasiri. Fomu hizo huwasilishwa katika Ofisi ya Tume kwa Uchaguzi wa Rais; katika Ofisi za Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo kwa Uchaguzi wa Wabunge na kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Kata kwa Uchaguzi wa Madiwani. Baada ya Fomu kupokelewa taarifa zote katika Fomu za Uteuzi zilichukuliwa kwa njia ya scanning kwa ajili ya maandalizi ya kutayarisha Karatasi za Kura.
      1. Aina za Wagombea


Uchaguzi Mkuu hujumuisha aina sita (6) ya Wagombea ambao ni; Wagombea Urais, Wagombea Umakamu wa Rais, Wagombea Ubunge, Wagombea Ubunge wa Viti Maalum vya Wanawake, Wagombea Udiwani katika Kata na Wagombea Udiwani wa Viti Maalum vya Wanawake.
      1. Mfumo wa Kushughulikia Fomu za Uteuzi za Wagombea


Mfumo wa kushughulikia Fomu za Uteuzi za Wagombea walioteuliwa hutumika kuandaa rasimu za Mfano wa Karatasi za Kura za Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Majimbo na Madiwani wa Kata za kila Halmashauri. Rasimu hizo hatimaye hutumika kuandaa Mfano wa Karatasi za Kura kwa ajili ya kutumika wakati wa Kampeni, kutoa Tangazo la Uchaguzi na Upigaji Kura kwa kubandikwa nje na ndani ya kila Kituo, na kutayarisha Karatasi za Kura.
    1. Taratibu za Uteuzi wa Mgombea Urais/Umakamu wa Rais


Utaratibu wa Uteuzi ulifanyika kwa Wagombea kutoka Vyama vya Siasa kujaza Fomu Na. 8A na kukamilisha masharti mengine kama yalivyoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika hatua ya kuthibitisha Wadhamini wa Wagombea husika, kwa upande wa Tanzania Zanzibar, Tume iliwatumia Waratibu wa Uchaguzi wa Pemba na Unguja na kwa Tanzania Bara, Tume iliwatumia Wasimamizi wa Uchaguzi. Hatua hii ilikusudia kuthibitisha kama wadhamini wamejiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
      1. Mamlaka inayohusika na Kuteua Wagombea


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo yenye jukumu la kuteua Wagombea Urais na Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kujiridhisha kwamba Mgombea hajapungukiwa na sifa yoyote na ametimiza masharti yanayotakiwa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi.
      1. Sifa na Masharti ya Kuteuliwa Kuwa Mgombea


Kwa mujibu wa Ibara za 39 na 47(4) (a) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Mgombea Urais/Umakamu wa Urais hana budi kuwa na sifa zifuatazo; Awe:

  1. Raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

  2. Ametimiza umri wa miaka 40 au zaidi;

  3. Ni mwanachama na Mgombea aliyependekezwa na

  4. Chama cha Siasa;

  5. Anazo sifa za kumuwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi; na,

  6. Hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi.

Mgombea Urais/Umakamu wa Rais hana budi kutimiza masharti yafuatayo ili ateuliwe; Awe:



  1. Amejaza Fomu Na. 8A.

  2. Ameweka dhamana ya shilingi milioni moja (1,000,000/=) Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  3. Amedhaminiwa na Wapiga Kura wasiopungua mia mbili ambao wameandikishwa kwa madhumuni ya Uchaguzi katika mikoa isiyopungua 10, kati ya mikoa hiyo angalau mikoa miwili (2) iwe ya Tanzania Zanzibar.

  4. Amekula Kiapo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa, kwamba anazo sifa zinazotakiwa, hajaondokewa na sifa hizo na anakubali kugombea.

  5. Hajatenda vitendo vilivyokatazwa kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

  6. Amewasilisha picha 4 za rangi zenye ukubwa sawa na picha ya pasi ya kusafiria (Passport size photo).
      1. Uchukuaji na Urejeshaji wa Fomu za Uteuzi na Fomu za Maadili


Tume ilianza kutoa Fomu za Uteuzi (Fomu Na. 8A) na Fomu ya Kuthibitisha kutekeleza Maadili ya Uchaguzi (Fomu Na.10) tarehe 01 Agosti, 2010 hadi tarehe 19 Agosti, 2010.
Tume ilitoa nafasi kwa Wagombea kuwasilisha Fomu za Uteuzi (Fomu Na. 8A) mapema kuanzia siku tatu kabla ya Siku ya Uteuzi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na kurejeshewa. Upokeaji rasmi ulifanyika Siku ya Uteuzi wa Wagombea.
        1. Wagombea Waliochukua Fomu za Uteuzi na Fomu za Maadili ya Uchaguzi


Jumla ya Wagombea kutoka Vyama vya Siasa kumi na mbili (12) walichukua Fomu za Uteuzi na Fomu za Maadili ya Uchaguzi kwenye Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Vyama hivyo ni APPT-Maendeleo, CCM, CHADEMA, CUF, JAHAZI ASILIA, MAKINI, DP, NCCR-Mageuzi, NRA, SAU, TLP na UPDP.
Hata hivyo, Mgombea kupitia Chama cha SAU, Bw. Paul Kyara, na Mgombea kupitia Chama cha DP, Mch. Christopher Mtikila, walishindwa kutimiza sharti la kuwa na Wadhamini wa kutosha kwa mujibu wa Sheria, hivyo hawakuteuliwa. Vyama vya Jahazi Asilia, Demokrasia Makini na NRA havikurejesha Fomu zao.
Jumla ya Wagombea saba (7) kutoka Vyama vya Siasa saba waliteuliwa na Tume kugombea Kiti cha Urais/Umakamu wa Rais baada ya kukidhi matakwa ya Sheria na masharti. Wagombea hao ni kama wanavyoonyeshwa kwenye Jedwali lifuatalo:-
Jedwali Na. 15: Orodha ya Wagombea wa Uchaguzi wa Rais/Makamu wa Rais, 2010


Na.

Chama

Jina laMgombea

Nafasi Aliyogombea

Jinsia



1

APPT-MAENDELEO

1. Mziray, Kuga Peter

Urais

Me

2. Mchenga, Rashid Yusuph

Umakamu wa Rais

Me


2


CCM

1. J 1. Kikwete, Jakaya Mrisho

Urais

Me

2. Bilal, Mohammed Gharib

Umakamu wa Rais

Me

  1. 33

CHADEMA

1. Dr. 1. Slaa, Wilbrod Peter

Urais

Me

2. Said, Mzee Said

Umakamu wa Rais

Me



4

CUF

1. Prof. Lipumba, Ibrahim Haruna

Urais

Me

2. J 2 2. Duni, Juma Haji

Umakamu wa Rais

Me



5

NCCR- MAGEUZI

1. Rungwe, Hashim Spunda

Urais

Me

2. Alli 2. Ali, Omar Juma

Umakamu wa Rais

Me



6

TLP

1. M 1. Mgaywa, Muttamwega Bhatt

Urais

Me

2. Mgaza, Abdallah Othman

Umakamu wa Rais

Me



7

UPDP

1.Dovutwa, Yahmi Nassoro Dovutwa

Urais

Me

2. Hamad, Mohammed Ibrahim

Umakamu wa Rais

Me
      1. Pingamizi Zilizotolewa Dhidi ya Uteuzi wa Wagombea


Baada ya Tume kuwateua Wagombea ilibandika nakala moja ya Fomu ya Uteuzi ya kila Mgombea mahali pa wazi kwa muda wa saa ishirini na nne (24) kuanzia saa kumi alasiri ya Siku ya Uteuzi hadi saa kumi (10.00) alasiri siku iliyofuata ili kutoa nafasi ya kuzikagua kwa wanaoruhusiwa kisheria kuweka pingamizi.
Wanaoruhusiwa kuweka pingamizi dhidi ya Uteuzi wa Wagombea Urais au Umakamu wa Rais kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 ni Wagombea, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hadi saa ya mwisho ya kupokea pingamizi dhidi ya uteuzi wa Wagombea Urais au Umakamu wa Rais, Tume haikupokea pingamizi yoyote.
      1. Matatizo Yaliyojitokeza Wakati wa Uteuzi


  1. Mgombea Urais wa Chama cha SAU hakukamilisha sharti la kuwa na Wadhamini mia mbili (200) kwa kila mkoa. Fomu za Wadhamini katika mikoa saba (7) hazikuthibitishwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa majimbo husika. Mikoa hiyo ni Ruvuma, Kigoma, Pwani, Dodoma, Lindi, Dar es Salaam na Mbeya. Chama cha SAU kiliamua kufungua lalamiko Mahakama Kuu. Lalamiko hilo hatimaye lilitupiliwa mbali na Mahakama kutokana na taratibu za Kimahakama kutozingatiwa.




  1. Mgombea Urais wa Chama cha DP alishindwa kupata Wadhamini wa kutosha katika mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro na Pwani, hivyo Fomu zake hazikupokelewa.
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət