Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə22/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   18   19   20   21   22   23   24   25   ...   33

Viti Maalum vya Wabunge na Madiwani Wanawake

  1. Viti Maalum vya Wabunge Wanawake


Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum, umeelekezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 78, kifungu cha 86A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2010 chini ya Kanuni ya 67.
Kwa mujibu wa taratibu hizo, kila Chama cha Siasa kilichoshiriki katika Uchaguzi Mkuu ambacho kimepata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za Ubunge zilizopigwa, kitapendekeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi majina ya Wanawake kwa kuzingatia uwiano wa Kura ambazo kila Chama kimepata katika Uchaguzi wa Wabunge.
Vile vile kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 endapo itajitokeza kuwa katika Jimbo la Uchaguzi, Mgombea wa Chama amepita bila kupingwa, idadi ya Kura halali za Urais wa Chama cha Mgombea huyo kama Chama husika kimeweka Mgombea, ndizo zitatumika katika zoezi hilo la kupata uwiano. Endapo itatokea kuwa Chama husika hakikusimamisha Mgombea Urais, asilimia hamsini na moja (51%) ya Kura za watu wote waliojiandikisha Kupiga Kura katika Jimbo hilo zitatumika kwa madhumuni hayo ya kutafuta uwiano.
Kutokana na uamuzi wa Serikali wa kuongeza idadi ya Viti Maalum vya Wabunge Wanawake kutoka asilimia thelathini (30) na kuwa asilimia isiyopungua arobaini (40) ya Wabunge waliotajwa katika Ibara ya 66 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, hivyo idadi ya Wabunge Wanawake kupitia Viti Maalum ilikuwa 102.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Vyama vya Siasa vitatu (3) tu ndivyo vilipata Kura halali zisizopungua asilimia tano (5%) ya idadi ya Kura halali zote za Ubunge zilizopatikana katika nchi nzima na kustahili kupata Viti Maalum vya Wabunge Wanawake. Vyama hivyo ni CCM, CHADEMA na CUF.
Mgawanyo wa Viti Maalum vya Wabunge Wanawake ni kama inavyoonesha katika Jedwali Na. 28.
Jedwali Na. 28: Idadi ya Viti Maalum vya Wabunge Wanawake kwa Kila Chama cha Siasa


Na.

Chama cha Siasa

Idadi ya Wabunge Wanawake

1

CCM

67

2

CHADEMA

25

3

CUF

10




JUMLA

102


Mchoro Na. 10: Wabunge wa Viti Maalum vya Wanawake kwa kila Chama


      1. Madiwani Wanawake wa Viti Maalum


Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa (Tawala za Wilaya) Sura ya 237, na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Tawala za Miji) Sura ya 288, zinaeleza kuwa kutakuwa na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum wasiopungua theluthi moja (1/3) ya Madiwani wa kuchaguliwa kwenye Kata pamoja na Mbunge wa Jimbo lililo kwenye Halmashauri husika.
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliteua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum 1,184 kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 29.
Jedwali Na. 29: Mgawanyo wa Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kwa kila Chama



Na.

Chama

Idadi ya Viti

1

APPT-MAENDELEO

1

2

CCM

972

3

CHADEMA

127

4

CUF

52

5

NCCR-MAGEUZI

11

6

TLP

10

7

UDP

10

8

DP

1




Jumla

1,184


Mchoro Na. 11: Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kwa kila Chama


    1. Changamoto Zilizojitokeza


  1. Mfumo wa kujumlisha Matokeo ya Urais na ya Ubunge Majimboni katika baadhi ya maeneo ulifanya kazi pole pole kiasi cha kusababisha hisia potofu kuwa Watendaji wa Uchaguzi wanachelewesha kwa makusudi kutangaza matokeo kwa hila za kubadilisha matokeo husika. Jambo hilo lilizua mashaka kwa mashabiki wa Vyama vya Siasa waliokuwa wanasubiri matokeo ya Uchaguzi. Hali hiyo iliwafanya baadhi Watendaji wa Uchaguzi watumie njia nyingine mbadala ya kujumlisha Kura ili kuweza kutangaza Matokeo hayo. Vile vile katika maeneo ya Miji mikubwa ambayo yalikuwa na vituo vingi vya kupigia kura, idadi iliyopangwa ya vitendea kazi (Laptops na scanners) havikuweza kuhimili kasi na idadi hiyo ya vituo kuweza kufanya kazi kwa haraka kama ilivyotarajiwa na hivyo kusababisha matokeo kuchelewa.




  1. Katika Zoezi la Ujumlishaji Kura katika baadhi ya maeneo, kutokana na hali ya kuonekana kuchelewa kutangazwa Matokeo ya Uchaguzi, baadhi ya washabiki wa Vyama vya Siasa waliokuwa wakisubiri matokeo katika maeneo hayo walihatarisha usalama kwa kutaka kuvamia eneo la Kujumlishia Kura. Hivyo, Jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati na hata kutumia nguvu. Matukio haya yalijitokeza ikiwa ni pamoja na katika Jimbo la Shinyanga Mjini ambapo Masanduku ya Kura na vifaa vingine vilichomwa moto na mashabiki wa Vyama vya Siasa baada ya kuvamia ukumbi wa kujumlishia kura baada ya kutangazwa matokeo.




  1. Maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu ujumlishaji na utumaji wa Matokeo ya Kura za Uchaguzi wa Rais kabla ya Matokeo ya Uchaguzi wa Wabunge hayakuzingatiwa na baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi.




  1. Wakati mchakato wa Ujumlishaji Kura ukiendelea, katika baadhi ya maeneo, baadhi ya Wagombea walitaka Kura zihesabiwe upya kwa baadhi ya Vituo bila kuwepo sababu za msingi isipokuwa kutokana tu na hisia za kushindwa. Wasimamizi wa Uchaguzi waliamua kufuata taratibu za Sheria zinazotawala suala hilo.




  1. Katika hatua ya kusaini Matokeo ya Uchaguzi baada ya kukamilisha Ujumlishaji wa Kura, baadhi ya Wagombea walikataa kusaini Fomu za Matokeo pamoja na kuwa walishiriki tangu mwanzo wa zoezi hilo kwa sababu tu ya kutokubaliana na matokeo hayo. Wasimamizi wa Uchaguzi waliendelea na hatua ya kutangaza Matokeo hayo kwa mujibu wa Sheria.




  1. CHADEMA kiliomba ujumlishaji wa matokeo ya Uchaguzi wa Rais usitishwe hadi malalamiko yake yatakaposhughulikiwa.




  1. Kuchelewa kutangazwa kwa Matokeo ya Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo kutokana na sababu mbalimbali.




  1. CHADEMA kutokutambua Matokeo ya Uchaguzi wa Rais.




  1. Baadhi ya Vyama vya Siasa kutozingatia utaratibu wa kuleta majina ya wanaopendekezwa kuteuliwa kuwa Wabunge au Madiwani Wanawake wa Viti Maalum siku 30 kabla ya Siku ya Uchaguzi.




  1. Tume kuchelewa kutangaza Majina ya Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kutokana na baadhi ya Vyama kutokuleta majina kwa wakati.


1   ...   18   19   20   21   22   23   24   25   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət