Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə19/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   15   16   17   18   19   20   21   22   ...   33

Usalama wa Vituo vya Kupigia Kura


Wasimamizi wa Uchaguzi kwa kushauriana na Makamanda wa Polisi wa Wilaya/Mshauri wa Mgambo wa Wilaya waliweza kupata Walinzi kwa ajili ya kulinda Vituo vya Kupigia Kura. Siku ya Uchaguzi kila Kituo cha Kupigia Kura kilikuwa na mlinzi mmoja.
    1. Maandalizi ya Vituo vya Kupigia Kura


Tume ilitoa orodha ya Vituo vya kupigia Kura kwa Wasimamizi wa Uchaguzi. Wasimamizi wa Uchaguzi walihakikisha kwamba Vituo vya Kupigia Kura vinakuwa tayari kwa ajili ya Uchaguzi. Maandalizi hayo yalihusisha ujenzi wa Vituo vya muda katika maeneo ambayo hayakuwa na majengo ya umma ya kudumu.
Kufuatia Chaguzi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na zile za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupangwa kufanyika siku moja, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilishauriana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na kukubaliana kuwa kwa upande wa Tanzania Zanzibar Vituo vya Kupigia Kura vitakavyotumika kwa Chaguzi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vitumike pia kwa Chaguzi za Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, kwa Wapiga Kura walioandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa upande wa Tanzania Zanzibar wenye sifa ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tu walipangiwa Vituo vyao vya Kupigia Kura.
    1. Mawakala wa Upigaji Kura


Kwa mujibu wa kifungu cha 57 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 58 cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Vyama vya Siasa vinatakiwa kuwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi orodha ya majina ya Mawakala na Vituo walivyopangiwa siku saba kabla ya Siku ya Uchaguzi.
Mawakala hupatiwa mafunzo na Vyama vyao. Baadhi ya Vyama vinashindwa kuwapatia Mawakala wao mafunzo kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha, hivyo, Mradi wa ESP kwa kutumia Taasisi ya Electoral Reform International Services (ERIS) ilitoa mafunzo kwa Wawakilishi wa Vyama vya Siasa ili baada ya mafunzo hayo Wawakilishi hao waweze kutoa mafunzo kwa Mawakala wa Vyama vya Siasa watakaohusika katika hatua mbalimbali za Uchaguzi. Mafunzo hayo yalichelewa kutolewa na kufanya baadhi ya Wawakilishi wa Vyama vya Siasa waliopatiwa mafunzo kushindwa kuendesha mafunzo kwa Mawakala wao. Isitoshe Vyama vya Siasa vina tabia ya kuteua Mawakala muda mfupi kabla ya Siku ya Uchaguzi, hivyo kukosa nafasi ya kuwapatia mafunzo yanayotakiwa.
    1. Mabadiliko ya Muundo wa Karatasi za Kura


Tume iliamua kubadili Muundo wa Karatasi za Kura uliokuwa ukitumiwa katika Chaguzi za nyuma kwa kufanya chaguo la Mpiga Kura kuwekwa katika chumba wazi kilichokuwa mwisho upande wa kulia kwa Picha ya Mgombea badala ya kuweka katika chumba wazi chini ya picha ya Mgombea.
Kufuatia uamuzi wa Tume wa kubadili muundo wa Karatasi za Kura za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Tume ilirekebisha baadhi ya vifungu katika vitabu vya Maelekezo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Maelekezo kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura ili kuendana na muundo mpya wa Karatasi za Kura.
    1. Upigaji Kura

      1. Matakwa ya Kisheria


Tarehe ya Uchaguzi ilipangwa kwa mujibu wa matakwa ya Sheria za Uchaguzi chini ya kifungu cha 46(1) na kifungu cha 48(1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambavyo vinaelekeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itapanga Siku ya Uchaguzi si chini ya siku 60 na si zaidi ya siku 90 tangu tarehe ya Uteuzi wa Wagombea Uchaguzi.
      1. Siku ya Uchaguzi


Tume ilipanga tarehe 31 Oktoba, 2010 kuwa ndiyo Siku ya Uchaguzi. Hata hivyo, kutokana na sababu mbalimbali Uchaguzi wa Wabunge katika Majimbo saba (7) na Madiwani katika Kata ishirini na tatu (23) haukufanyika siku hiyo. Uchaguzi wa Wabunge katika Majimbo yaliyoahirishwa ulifanyika tarehe 14 Novemba, 2010 na ule wa Madiwani ulifanyika tarehe 28 Novemba, 2010.
      1. Vituo vya Kupigia na Kuhesabia Kura


Upigaji Kura ulifanyika katika Vituo 53,039 vya Kupigia Kura vilivyopo katika Majimbo 239, kama inavyoonyesha katika Jedwali Na. 22. Kwa upande wa Tanzania Bara kulikuwa na jumla ya Vituo vya Kupigia Kura 51,392 na Tanzania Zanzibar vilikuwa 1,647. Vituo vilivyotumika kuandikisha Wapiga Kura ndivyo viligeuka kuwa vituo vya Kupigia Kura. Kila Kituo cha Kupigia Kura kilikuwa na idadi ya Wapiga Kura wasiozidi 500, kwa hiyo baadhi ya Vituo vya Kuandikisha Wapiga Kura viligawanywa na kutoa Vituo vya Kupigia Kura zaidi ya kimoja.

Jedwali Na. 22: Mgawanyo wa Vituo vya Kupigia Kura



Na.

Mkoa

Idadi ya Majimbo

Idadi ya Kata

Idadi ya Vituo vya Kupigia Kura

1

Dar es Salaam

8

90

5,400

2

Morogoro

10

181

2,860

3

Pwani

9

112

1,610

4

Dodoma

9

190

2,456

5

Singida

8

124

1,431

6

Tabora

9

163

2,377

7

Kigoma

8

110

1,830

8

Mwanza

13

214

4,410

9

Shinyanga

13

245

3,984

10

Mara

7

154

2,132

11

Kagera

10

203

2,282

12

Arusha

7

123

2,016

13

Manyara

6

123

1,533

14

Tanga

11

206

3,289

15

Kilimanjaro

9

153

2,171

16

Mtwara

7

149

1,978

17

Lindi

8

142

1,273

18

Mbeya

11

218

2,964

19

Iringa

11

189

2,369

20

Ruvuma

7

140

1,700

21

Rukwa

8

106

1,327

22

Unguja

32

97

1,105

23

Pemba

18

44

542




JUMLA

239

3,335

53,039
      1. Tangazo la Uchaguzi


Kwa mujibu wa kifungu cha 47 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 49 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tangazo la Uchaguzi (Notice of Election) linatakiwa litolewe kabla au siku ya nane kabla ya Siku ya Uchaguzi. Tangazo hilo, pamoja na mambo mengine, linajumuisha orodha ya Wapiga Kura waliopangiwa kupiga Kura katika kila Kituo cha Kupigia Kura.
Tangazo la Uchaguzi lilibandikwa katika Ofisi za Wasimamizi wa Uchaguzi, Ofisi za Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Kata na katika kila Kituo cha Kupigia Kura. Tume kupitia Vyombo vya Habari iliwatangazia Wapiga Kura kwenda kwenye Vituo walivyojiandikisha kuangalia majina yao katika orodha hizo ili kutambua Vituo walivyopangiwa Kupigia Kura Siku ya Uchaguzi.

      1. Usambazaji wa vifaa vya Siku ya Uchaguzi kwenda Vituoni


Wasimamizi wa Uchaguzi waligawa vifaa vya Kupigia Kura kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura na kuvisambaza baada ya kukamilisha mafunzo kwa watendaji hao.
      1. Kuahirisha Uchaguzi


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ililazimika kusitisha Uchaguzi wa Madiwani katika Kata mbili kutokana na vifo vya Wagombea. Katika Kata ya Nyanchenda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mgombea Udiwani wa Chama cha NCCR–Mageuzi alifariki tarehe 09 Oktoba, 2010 na Mgombea Udiwani wa Chama cha CHADEMA katika Kata ya Igunda iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kahama alifariki tarehe 05 Oktoba, 2010. Kwa mujibu wa kifungu cha 51 cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ilipanga siku nyingine ya Uteuzi. Tarehe 2 Novemba, 2010 Uteuzi wa Wagombea wa Udiwani wa Vyama vya NCCR–Mageuzi na CHADEMA ulifanyika. Tume ilipanga tarehe 28 Novemba, 2010 kuwa Siku ya Uchaguzi wa Madiwani katika Kata hizo.
Vile vile, Tume iliahirisha Uchaguzi wa Madiwani katika Kata ishirini na moja (21) kutokana na hitilafu/upungufu wa Karatasi za Kura. Kata zilizohusika na kuahirisha kwa Uchaguzi kutokana na sababu za upungufu wa Karatasi za Kura, makosa ya uchapishaji na kufariki kwa Wagombea ni kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 23: Orodha ya Kata Ambazo Hazikufanya Uchaguzi tarehe 31 Oktoba, 2010




NA.


HALMASHAURI





KATA

1

Wilaya ya Manyoni

1

Kitaraka

2

Wilaya ya Karagwe

2

Kimuli

3

Kamuli

3

Wilaya ya Njombe

4

Mji Mwema

4

Wilaya ya Same

5

Kisiwani

5

Wilaya ya Rufiji

6

Kipungira







7

Ngorongo







8

Chemchem







9

Mjawa







10

Kibiti

6

Wilaya ya Ulanga

11

Msogezi

7

Wialaya ya Newala

12

Mtonya

8

Jiji la Mwanza

13

Mkuyuni

14

Mirongo

9

Wilaya ya Kasulu

15

Kitagata

16

Nyanchenda

10

Wilaya ya Kibaha

17

Janga

11

Wilaya ya Mbulu

18

Endegikoti

12

Wilaya ya Chato

19

Buseresere

13

Wilaya ya Uyui

20

Kigwa

21

Ibelamilundi

14

Wilaya ya Sikonge

22

Kisanga

15

Wilaya ya Kahama

23

Igunda

Aidha, Tume ililazimika kuahirisha Uchaguzi wa Bunge katika majimbo ya Uchaguzi saba kutokana na hitilafu/upungufu wa Karatasi za Kura. Majimbo yaliyohusika ni Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini na Nkenge ambayo yapo Tanzania Bara, pia majimbo ya Wete, Magogoni, Mtoni na Mwanakwerekwe ambayo yapo Tanzania Zanzibar. Uchaguzi wa Bunge katika Majimbo hayo ulipangwa na kufanyika tarehe 14 Novemba, 2010.


Jedwali Na. 24: Orodha ya Majimbo ya Uchaguzi Ambayo hayakufanya Uchaguzi tarehe 31 Oktoba, 2010



Na.

Mkoa

Halmashauri/

Wilaya




Jimbo

1

KAGERA

Wilaya ya Missenyi

1

Nkenge



2

RUKWA


Wilaya ya Mpanda

2

Mpanda Vijijini

Mji Mpanda

3

Mpanda Mjini

3

Kaskazini Pemba

Wete

4

Wete

4

Mjini Magharibi

Magharibi

5

Magogoni










6

Mtoni










7

Mwanakwerekwe
      1. Maelekezo ya Tume Kuelekea Siku ya Uchaguzi


Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi ili Mpiga Kura aweze kupiga Kura yake hana budi kuwa na kadi yake ya kupigia kura na jina lake liwepo katika Daftari la Wapiga Kura la Kituo husika.
Tume ilitoa maelekezo ya nyongeza ya kuruhusu Kupiga Kura Wapiga Kura ambao namba za kadi zao zinatofautiana na namba zilizomo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Vile vile Tume ilitoa ruhusa ya Kupiga Kura kwa Wapiga Kura ambao wanazo Kadi zao za Kupigia Kura na Taarifa zao zinalingana na zilizopo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura isipokuwa picha zao hazimo katika Daftari hilo.
      1. Risala ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa Wapiga Kura.


Siku moja kabla ya Siku ya Uchaguzi, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Mst.) Lewis M. Makame kupitia Vyombo vya Habari alitoa Risala kwa Wapiga Kura kuhusu Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani uliotarajiwa kufanyika Siku ya Jumapili tarehe 31 Oktoba, 2010. Risala hiyo ilielezea muda wa kufungua na kufunga Vituo vya Kupigia Kura, utaratibu wa Kupiga Kura vituoni, utaratibu wa kuhesabu Kura, ujumlishaji Kura na utangazaji wa Matokeo ya Uchaguzi. Vile vile, Risala hiyo ilielezea mambo yanayopaswa kufanywa na Mpiga Kura Kituoni na yale yasiyopaswa. Risala hiyo imeambatishwa kama Kiambatisho G.
      1. Zoezi la Upigaji Kura - Siku ya Uchaguzi


Katika kila Kituo cha Kupigia Kura kulikuwa na Watendaji watatu ambao walihusika na majukumu ya kusimamia na kuendesha zoezi la Kupiga Kura na kuhesabu Kura. Aidha, kulikuwepo na Karani Muongozaji Wapiga Kura kwa ajili ya kuwaelekeza Wapiga Kura chumba/Kituo cha Kupigia Kura zao.
Vituo vilifunguliwa saa 1.00 asubuhi na kufungwa katika muda uliopangwa ambao ni saa 10.00 alasiri. Wapiga Kura katika Vituo vingi walifuata taratibu. Katika baadhi ya Vituo majira ya asubuhi kulikuwa na Wapiga Kura wengi lakini kufikia majira ya mchana ni Wapiga Kura wachache tu walikuwa wakienda vituoni. Wapiga Kura wengi walipomaliza Kupiga Kura waliondoka vituoni.
Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali/Maoni ya Watazamaji/Wadau wengine na Timu za Ufuatiliaji za Tume zilibainisha kuwa kwa ujumla, pamoja na kujitokeza kasoro ndogo ndogo, Watendaji wa Vituo vya Kupigia na Kuhesabia Kura walitekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi na Maelekezo ya Tume. Aidha, walishirikiana na kushauriana vizuri pale ilipobidi na Mawakala wa Vyama vya Siasa na Wagombea.
      1. Hali ya Usalama Katika Vituo


Kulikuwa na ulinzi wa kutosha katika Vituo vya Kupigia Kura vyote, pia kulikuwa na Polisi wa Doria waliozungukia sehemu mbalimbali kuhakikisha Usalama. Maeneo machache yaliyokuwa na vurugu yalidhibitiwa mara moja.
      1. Mahudhurio ya Mawakala Vituoni


Vituo vya Kupigia Kura vilikuwa na Mawakala wa Vyama vya Siasa. CCM kiliweka Mawakala katika Vituo vyote. Vyama vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR–Mageuzi viliweka Mawakala katika baadhi ya Vituo. Hata hivyo, Vyama vingine vilivyoshiriki viliweka mawakala katika Vituo/maeneo machache sana.
Mawakala wengi waliokuwa vituoni hawakuwa na Daftari la Wapiga Kura, kiasi cha wengine kutaka watumie Daftari moja na Wasimamizi wa Vituo. Aidha, baadhi ya Mawakala hawakuelewa majukumu yao, hivyo wakati mwingine kujaribu kuingilia majukumu ya Msimamizi wa Kituo. Kwa ujumla Mawakala walionesha ushirikiano mzuri na Watendaji wa Vituo ukiachia mbali matatizo haya machache yaliyojitokeza. Karibu Mawakala wote walijaza Fomu zilizotakiwa vituoni.
Kwa ujumla zoezi la Upigaji Kura lilifanyika kwa amani na uwazi, na Wapiga Kura wote waliojitokeza Kupiga Kura walipiga Kura zao.
1   ...   15   16   17   18   19   20   21   22   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət