Taratibu za Uteuzi wa Wagombea Udiwani
Utaratibu wa Uteuzi ulianzia kwa Mgombea mwenye sifa kujaza Fomu Na 8C na Fomu Na. 10 kukamilisha masharti mengine yaliyoainishwa na Tume kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2010.
Mamlaka ya Uteuzi
Uteuzi wa Wagombea Udiwani ulifanywa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa ngazi ya Kata chini ya usimamizi wa Wasimamizi wa Uchaguzi.
Sifa na Masharti ya Uteuzi -
Sifa za Mgombea Udiwani
Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ili mtu aweze kuteuliwa kugombea Udiwani hana budi kuwa na sifa zifuatazo; Awe:
-
Raia wa Tanzania;
-
Ametimiza umri wa miaka ishirini na moja (21) au zaidi;
-
Mkazi wa eneo la Halmashauri anayogombea;
-
Anaweza kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili au
Kiingereza;
-
Mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na Chama cha
Siasa;
-
Na kipato halali kinachomwezesha kuishi; na
-
Hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa
kulipa Kodi ya Serikali katika kipindi cha miaka mitano kabla ya
tarehe ya Uchaguzi.
-
Masharti ya Uteuzi kwa Mgombea Udiwani
Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 na Maelekezo ya Tume, ili mtu aweze kuteuliwa kuwa mgombea hana budi awe ametimiza masharti yafuatayo; Awe:
-
Amedhaminiwa na Wapiga Kura wasiopungua kumi (10) walioandikishwa Kupiga Kura katika Kata anayogombea;
-
Ametoa Tamko la kisheria mbele ya Hakimu kuthibitisha kuwa anazo sifa za kugombea;
-
Ameweka dhamana ya shilingi 5,000/= kwa Msimamizi wa Uchaguzi;
-
Hajatenda vitendo vilivyokatazwa kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010;
-
Amejaza Fomu zinazohitajika za Uteuzi ambazo ni Fomu Na. 8C na Fomu Na. 10 ya kukubali kutekeleza Maadili ya Uchaguzi; na
-
Amewasilisha picha nne (4) za rangi zenye ukubwa wa pasi ya kusafiria (Passport size photo).
Uchukuaji na Urejeshaji wa Fomu za Uteuzi na Fomu za Maadili
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianza kutoa Fomu za Uteuzi (Fomu Na.8C) na Fomu za Maadili ya Uchaguzi (Fomu Na. 10) tarehe 6 Agosti, 2010 hadi tarehe 19 Agosti, 2010.
Tume ilitoa nafasi kwa Wagombea kuwasilisha Fomu za Uteuzi (Fomu Na. 8C) mapema kuanzia siku tatu kabla ya uteuzi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na kurejeshewa. Upokeaji rasmi ulifanyika Siku ya Uteuzi.
Wagombea Udiwani Walioteuliwa
Kwa ujumla idadi ya Wagombea 7,934 waliteuliwa kugombea kupitia Vyama vya Siasa mbalimbali katika jumla ya Kata 3,335. Aidha, katika Kata 600 Wagombea wa CCM walipita bila kupingwa.
Jedwali Na. 19: Idadi ya Wagombea Udiwani Walioteuliwa
-
Na.
|
Chama
|
Idadi ya Wagombea Udiwani
|
Jinsia
|
ME
|
KE
|
1.
|
AFP
|
11
|
9
|
2
|
2.
|
APPT-MAENDELEO
|
27
|
19
|
8
|
3.
|
CCM
|
3,335
|
3,112
|
223
|
4.
|
CHADEMA
|
1,864
|
1,786
|
78
|
5.
|
CHAUSTA
|
23
|
17
|
6
|
6.
|
CUF
|
1,575
|
1,510
|
65
|
7.
|
DP
|
41
|
33
|
8
|
8.
|
JAHAZI ASILIA
|
26
|
14
|
12
|
9.
|
MAKINI
|
13
|
8
|
5
|
10.
|
NCCR-MAGEUZI
|
280
|
251
|
29
|
11.
|
NLD
|
37
|
26
|
11
|
12.
|
NRA
|
43
|
26
|
17
|
13.
|
SAU
|
97
|
81
|
16
|
14.
|
TADEA
|
15
|
11
|
4
|
15.
|
TLP
|
285
|
258
|
27
|
16.
|
UDP
|
188
|
167
|
21
|
17.
|
UMD
|
42
|
25
|
17
|
18.
|
UPDP
|
32
|
22
|
10
|
Jumla
|
7,934
|
7,375
|
559
|
Mchoro Na. 6: Walioteuliwa Kugombea Udiwani
Wagombea Udiwani mia sita (600) walipita bila kupingwa kutokana na baada ya Wagombea wengine kuenguliwa na Msimamizi wa Uchaguzi/ Tume kwa sababu ya kukosa sifa au kutokana na kujitokeza kwa mgombea mmoja pekee katika Kata husika. Wagombea wote waliopita bila kupingwa ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kama inavyooneshwa kwenye Kiambatisho H.
-
Pingamizi dhidi ya Uteuzi wa Madiwani ziliwasilishwa na kufanyiwa Uamuzi kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Kata. Msimamizi wa Uchaguzi alikuwa na mamlaka ya kupitia Uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata. Wagombea ambao hawakuridhika na Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi walikata Rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Rufaa kutokana na Uteuzi
Jumla ya Rufaa 122 ziliwasilishwa Tume baada ya uamuzi uliotolewa na Wasimamizi wa Uchaguzi kupingwa na Wagombea husika. Rufaa ishirini na mbili (22) zilikubaliwa na Rufaa 100 zilikataliwa. Miongoni mwa sababu za rufaa hizo ni:-
-
Mgombea si mkazi wa Halmashauri husika;
-
Mgombea ni mtumishi wa Serikali;
-
Mgombea ana Uraia wa nchi mbili; na
-
Mgombea ana mkataba wenye maslahi na Halmashauri husika.
Jedwali Na. 20: Uamuzi wa Tume juu ya Rufaa za Wagombea Udiwani
-
Na.
|
Chama
|
Idadi ya Rufaa
|
Rufaa Zilizokubaliwa
|
Rufaa Zilizokataliwa
|
1
|
CCM
|
45
|
2
|
43
|
2
|
CHADEMA
|
35
|
13
|
22
|
3
|
CUF
|
34
|
5
|
29
|
4
|
NCCR-MAGEUZI
|
2
|
0
|
2
|
5
|
TLP
|
5
|
2
|
3
|
6
|
UDP
|
1
|
0
|
1
|
|
Jumla
|
122
|
22
|
100
| |