Taratibu za Uteuzi wa Wagombea Ubunge
Mgombea Ubunge alipaswa kujaza Fomu Na. 8B ambayo ndiyo Fomu ya Uteuzi na Fomu Na. 10 ya kukubali kuzingatia Maadili ya Uchaguzi.
-
Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo ndio waliohusika na uteuzi kwa mujibu wa Sheria.
-
Mgombea hana budi kuwa na Sifa na atimize Masharti kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Maelekezo ya Tume.
Mamlaka ya Uteuzi wa Wagombea Ubunge
Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi Wasimamizi wa Uchaguzi ndio wenye jukumu la kuteua Wagombea Ubunge walio na sifa na waliotimiza masharti.
Sifa na Masharti ya Uteuzi -
Sifa za Kuteuliwa kuwa Mgombea Ubunge
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977 ili mtu aweze kuteuliwa kuwa Mgombea Ubunge hana budi kuwa na sifa zifuatazo; Awe:-
-
Raia wa Tanzania.
-
Ametimiza umri wa miaka ishirini na moja .
-
Anajua kusoma na kuandika kwa Kiswahili au
Kiingereza.
-
Ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa
na Chama cha Siasa.
-
Hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kodi yoyote ya Serikali katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi.
-
Masharti ya Kuteuliwa kuwa Mgombea Ubunge
Kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Maelekezo ya Tume ili mtu aweze kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge, pamoja na sifa zilizotajwa hapo juu, hana budi kutimiza masharti yafuatayo; Awe:
-
Amejaza kikamilifu Fomu ya Uteuzi yaani Fomu Na.8B.
-
Amedhaminiwa na Wapiga Kura wasiopungua ishirini na tano ambao wamejiandikisha kuwa Wapiga Kura katika Jimbo hilo.
-
Ameweka dhamana ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
-
Ametoa Tamko mbele ya Hakimu kuwa anazo sifa zinazotakiwa ili kugombea Ubunge.
-
Hajatenda vitendo vilivyokatazwa chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.
-
Amewasilisha picha nne za rangi zenye ukubwa sawa na Pasi ya Kusafiria (Passport size photo).
-
Amejaza Fomu zote zinazohitajika zikiwemo Fomu za kukubali kutekeleza Maadili ya Uchaguzi (Fomu Na. 10).
Uchukuaji na Urejeshaji wa Fomu za Uteuzi na Fomu za Maadili
Tume ilianza kutoa Fomu za Uteuzi (Fomu Na. 8B) na Fomu ya Kuthibitisha kutekeleza Maadili ya Uchaguzi (Fomu Na.10) tarehe 06 Agosti, 2010 hadi tarehe 19 Agosti, 2010.
Tume ilitoa nafasi kwa Wagombea kuwasilisha Fomu za Uteuzi (Fomu Na. 8B) mapema kuanzia siku tatu kabla ya Siku ya Uteuzi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na kurejeshewa. Upokeaji rasmi ulifanyika Siku ya Uteuzi.
Wagombea Ubunge Walioteuliwa Majimboni
Jumla ya Wagombea 1,036 waliteuliwa kugombea Ubunge katika majimbo 239 ya Uchaguzi. Kati ya Wagombea hao, jumla ya Wagombea 845 (asilimia 81.5) walikuwa ni wanaume na 191 (asilimia 18.4) ni wanawake. Vyama vyote vya Siasa kumi na nane (18) vilivyopata usajili kamili viliweka Wagombea katika majimbo mbalimbali.
Jedwali Na. 16: Idadi ya Wagombea Ubunge Walioteuliwa
-
Na.
|
Chama
|
Idadi ya Wagombea Ubunge
|
Jinsia
|
Me
|
Ke
|
1.
|
AFP
|
15
|
11
|
4
|
2.
|
APPT – Maendeleo
|
16
|
9
|
7
|
3.
|
CCM
|
239
|
215
|
24
|
4.
|
CHADEMA
|
179
|
154
|
25
|
5.
|
CHAUSTA
|
13
|
8
|
5
|
6.
|
CUF
|
182
|
168
|
14
|
7.
|
DP
|
35
|
24
|
11
|
8.
|
JAHAZI ASILIA
|
21
|
15
|
6
|
9
|
MAKINI
|
17
|
12
|
5
|
1010.
|
NCCR-Mageuzi
|
67
|
52
|
15
|
1111.
|
NLD
|
23
|
15
|
8
|
12
|
NRA
|
19
|
13
|
6
|
13
|
SAU
|
32
|
26
|
6
|
14
|
TADEA
|
32
|
20
|
12
|
15
|
TLP
|
42
|
36
|
6
|
16
|
UDP
|
45
|
31
|
14
|
17
|
UMD
|
23
|
13
|
10
|
18
|
UPDP
|
36
|
23
|
13
|
|
JUMLA
|
1036
|
845
|
191
|
Mchoro Na. 5: Walioteuliwa Kugombea Ubunge
Wagombea Ubunge kumi na saba (17) walipita bila kupingwa kutokana na baada ya Wagombea wengine kuenguliwa na Msimamizi wa Uchaguzi au Tume kwa sababu ya kukosa sifa au kutokana na kujitokeza kwa mgombea mmoja pekee katika Jimbo husika.
Katika Majimbo yote kumi na saba (17) ni Wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndiyo waliopita bila kupingwa, kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 17.
Jedwali Na. 17: Orodha ya Majimbo Ambayo Wabunge Walipita bila Kupingwa
-
Na.
|
Halmashauri
|
Jimbo
|
Sababu
|
1
|
Mji wa Njombe
|
Njombe Kusini
|
Hakupata mpinzani
|
2
|
Wilaya ya Chunya
|
Songwe
|
Hakupata mpinzani
|
3
|
Wilaya ya Iringa
|
Ismani
|
Hakupata mpinzani
|
4
|
Wilaya ya Kongwa
|
Kongwa
|
Hakupata mpinzani
|
5
|
Wilaya ya Ludewa
|
Ludewa
|
Hakupata mpinzani
|
6
|
Wilaya ya Mpanda
|
Katavi
|
Hakupata mpinzani
|
7
|
Wilaya ya Mpwapwa
|
Mpwapwa
|
Hakupata mpinzani
|
8
|
Wilaya ya Mufindi
|
Mufindi Kaskazini
|
Mpinzani kuenguliwa
|
9
|
Wilaya ya Mufindi
|
Mufindi Kusini
|
Mpinzani kuenguliwa
|
10
|
Wilaya ya Muleba
|
Muleba Kusini
|
Hakupata mpinzani
|
11
|
Wilaya ya Musoma
|
Musoma Vijijini
|
Mpinzani alijitoa
|
12
|
Wilaya ya Rungwe
|
Rungwe Mashariki
|
Hakupata mpinzani
|
13
|
Wilaya ya Rungwe
|
Rungwe Magharibi
|
Mpinzani kuenguliwa
|
14
|
Wilaya ya Sengerema
|
Sengerema
|
Mpinzani kuenguliwa
|
15
|
Wilaya ya Simanjiro
|
Simanjiro
|
Hakupata mpinzani
|
16
|
Wilaya ya Ulanga
|
Ulanga Mashariki
|
Hakupata mpinzani
|
17
|
Wilaya ya Lushoto
|
Bumbuli
|
Hakupata mpinzani
| -
Kwa mujibu wa taratibu za Uteuzi baada ya Tume kufanya Uteuzi, inapaswa kubandika Fomu za Uteuzi wa Wagombea wote mahali pa wazi kwa muda wa saa ishirini na nne (24) ili kutoa nafasi kuzikagua kwa wanaoruhusiwa Kisheria kuweka pingamizi. Baada ya Fomu hizo kubandikwa mahali pa wazi kuanzia saa kumi alasiri Siku ya Uteuzi hadi saa kumi alasiri ya siku iliyofuata.
-
Pingamizi za Msajili wa Vyama vya Siasa
Kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 Msajili wa Vyama vya Siasa anaruhusiwa kuweka pingamizi dhidi ya Mgombea yeyote ambaye hakutimiza au amekiuka masharti ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Msajili wa Vyama vya Siasa aliwasilisha pingamizi kwa Msimamizi wa Uchaguzi dhidi ya uteuzi wa Mgombea Ubunge wa TLP katika Jimbo la Mtama kwa kutokutoa taarifa za gharama atakazotumia katika Uchaguzi. Pingamizi hiyo ilikubaliwa na Msimamizi wa Uchaguzi. Hata hivyo, Mgombea alikata Rufaa Tume na Rufaa hiyo ilikubaliwa.
-
Pingamizi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 Kifungu cha 40(3), Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaruhusiwa kutoa pingamizi dhidi ya uteuzi wa Mgombea. Katika Uchaguzi uliopita hakukuwa na pingamizi yoyote iliyowasilishwa kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
-
Baada ya Siku ya Uteuzi, Wasimamizi wa Uchaguzi walipokea pingamizi mbalimbali na kuzitolea maamuzi. Wagombea ambao hawakukubaliana na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi walikata Rufaa kwa Tume.
Jumla ya Rufaa hamsini na moja (51) ziliwasilishwa Tume na Wagombea mbalimbali wa Ubunge. Katika Rufaa zilizowasilisha na kuamuliwa na Tume, Rufaa kumi na nne (14) zilikubaliwa na thelathini na saba (37) zilikataliwa. Kwa muhtasari sababu za Rufaa hizo ni pamoja na:-
-
Kutokujaza Fomu Na. 10.
-
Kutodhaminiwa na Chama chake cha Siasa.
-
Hakusaini Tamko la Kisheria.
-
Namba za kadi za Wapiga Kura waliomdhamini zilikuwa na kasoro.
-
Kutoa maelezo ya uongo katika Fomu ya uteuzi.
-
Tuhuma za rushwa.
Rufani zilizowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na matokeo ya Rufaa yanaoneshwa katika Jedwali Na. 18.
Jedwali Na. 18: Uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Rufaa za Wagombea Ubunge
-
Na.
|
Chama
|
Idadi ya Rufaa
|
Rufaa Zilizokubaliwa
|
Rufaa
Zilizokataliwa
|
1
|
AFP
|
1
|
1
|
0
|
2
|
CCM
|
11
|
0
|
11
|
3
|
CHADEMA
|
15
|
7
|
8
|
4
|
CUF
|
12
|
4
|
8
|
5
|
MAKINI
|
1
|
0
|
1
|
6
|
JAHAZI ASILIA
|
1
|
0
|
1
|
7
|
NCCR-MAGEUZI
|
4
|
0
|
4
|
8
|
SAU
|
2
|
1
|
1
|
9
|
TLP
|
3
|
1
|
2
|
10
|
UDP
|
1
|
0
|
1
|
|
Jumla
|
51
|
14
|
37
| |