Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə13/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   9   10   11   12   13   14   15   16   ...   33

Uchapishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Orodha za Wapiga Kura

Baada ya kuingizwa kwa marekebisho na Taarifa zote zilizotoka vituoni wakati wa uwekaji wazi wa Daftari la Awali, ndipo Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilichapishwa ikiwa ni pamoja na Orodha za Wapiga Kura. Daftari lilichapishwa kwa kila Kituo kulingana na jinsi Wapiga Kura walivyojiandikisha. Hata hivyo, Uchapaji wa Daftari na Uandaaji wa Orodha ulifanyika baada ya kuwagawa Wapiga Kura katika Vituo vya Kupigia Kura ambapo Kituo kimoja kilikuwa na Wapiga Kura wasiozidi 500.


Sambamba na Daftari, ilichapishwa Orodha ya Wapiga Kura nakala tatu; nakala moja ilibandikwa kwenye Kituo Siku 8 kabla ya Uchaguzi, ili Wapiga Kura waweze kufahamu Vituo vyao vya Kupigia Kura, nyingine ilibandikwa Siku ya Uchaguzi na nyingine ilitumiwa na Karani Mwongozaji. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 uchapishaji wa Daftari la kila Kituo kwa nchi nzima ulikamilika tarehe 20 Oktoba, 2010.
Aidha, Vyama vya Siasa vilipatiwa nakala ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa “softcopy”.

Jedwali Na. 13: Idadi ya Wapiga Kura Walioandikishwa Tanzania Bara



Na.

Mkoa

Wapiga Kura 2005

Uboreshaji Awamu ya I 2008/09

Uboreshaji Awamu ya II

2009/10

Jumla ya Wapiga Kura

1

Dodoma

759,251

90,310

47,051

896,612

2

Kigoma

600,872

65,242

55,392

721,506

3

Singida

482,544

62,530

9,693

554,767

4

Tabora

723,319

116,695

77,833

917,847

5

Dar es Salaam

1,680,831

231,831

486,077

2,398,739

6

Morogoro

895,179

92934

92,656

1,080,769

7

Pwani

469,924

48,917

46,964

565,805

8

Kagera

906,852

141,442

61,778

1,110,072

9

Mara

663,774

89,132

65,725

818,631

10

Mwanza

1,397,673

189,246

116,846

1,703,765

11

Shinyanga

1,236,560

144,393

136,099

1,517,052

12

Arusha

650,199

73,675

89,170

813,044

13

Kilimanjaro

661,288

78,241

64,627

804,156

14

Manyara

484,230

49,664

61,701

595,595

15

Tanga

789,244

102,698

64,838

956,780

16

Mtwara

572,510

85,710

23,445

681,665

17

Lindi

388,384

62,236

14,096

464,716

18

Iringa

673,686

84,576

27,572

785,834

19

Mbeya

951,011

105,115

84,578

1,140,704

20

Rukwa

427,948

61,341

33,654

522,943

21

Ruvuma

504,470

103,450

26,305

634,225

 

Jumla

15,919,749

2,079,378

1,686,100

19,685,227


Mchoro Na. 3: Idadi ya Wapiga Kura - Uboreshaji Awamu ya Kwanza na Awamu ya Pili- Tanzania Bara


Jedwali Na. 14: Idadi ya Wapiga Kura Walioandikishwa Tanzania Zanzibar



 NA.

Mkoa

NEC 2005

ZEC 2005

JUMLA ya NEC na ZEC 2005

NEC 2010

ZEC 2010

JUMLA ya ZEC na NEC 2010

1.

Kaskazini – Pemba

726

81,438

82,164

13,477

66,052

79,529

2.

Kaskazini – Unguja

1,004

80,754

81,758

8,616

61,839

70,455

3.

Kusini – Pemba

2,185

75,290

77,475

7,510

62,915

70,425

4.

Kusini – Unguja

774

64,188

64,962

3,333

48,071

51,404

5.

Mjini Magharibi

11,055

205,565

216,620

11,482

168,781

180,263

 

Jumla

15,744

507,235

522,979

44,418

407,658

452,076


Mchoro Na. 4: Idadi ya Wapiga Kura Walioandikishwa Tanzania Zanzibar

Kwa hiyo, jumla ya Wapiga Kura walioandikishwa (2010) kwa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ni 20,137,303.

1   ...   9   10   11   12   13   14   15   16   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət