Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə9/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   5   6   7   8   9   10   11   12   ...   33

Ununuzi na Usambazaji wa Vifaa vya Uchaguzi


Maandalizi ya Ununuzi wa Vifaa na Usambazaji yalifanyika kwa kuzingatia Ratiba ya Utekelezaji iliyoandaliwa na Tume kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Maandalizi haya yalijumuisha pamoja na vifaa vyote vilivyohitajika katika kila hatua ya mchakato wa Uchaguzi kuanzia Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na hadi Utangazaji wa Matokeo ya Uchaguzi.
      1. Ununuzi wa Vifaa


Katika awamu zote za ununuzi, yaani vifaa kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ulifanywa na Tume yenyewe kwa kufuata Sheria ya Manunuzi ya vifaa vya Serikali Na. 21 ya mwaka 2004 na Kanuni zake za mwaka 2005. Vifaa vingine vilinunuliwa na Washirika wa Maendeleo kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Uchaguzi vimegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni:-


  1. Vifaa Vilivyonunuliwa na Tume

Tume ilinunua vifaa kwa njia ya Zabuni ya Wazi (Open Tender) na Moja kwa Moja (Single Source).


  1. Vifaa Vilivyonunuliwa kwa Njia ya Zabuni ya Wazi (Zabuni ya Kitaifa na Kimataifa)

Vifaa vilivyonunuliwa kwa njia ya Zabuni kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura ni pamoja na Sajara (Stationary), Vidau vya wino kwa ajili ya Dole Gumba, Vifuko vya kutengeneza kitambulisho (Lamination Pouches), Plastiki za kubandikia picha (Photofix Films), Karatasi za nyongeza za kuchapishia Picha kwa ajili ya Uandikishaji/Uboreshaji.
Vifaa vilivyonunuliwa kwa njia ya Zabuni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ni Vituturi, Fulana na Kofia, Taa, Bahasha Maalumu (Tamper-Proof Envelopes), Betri za taa, Karatasi za Kura na Fomu za Matokeo.


  1. Vifaa Vilivyonunuliwa kwa Njia ya Moja kwa Moja (Single Source)

Ununuzi huu ulifanyika kutoka kwa Mpiga Chapa wa Serikali. Vifaa vilivyonunuliwa ni Machapisho na Fomu mbalimbali zilizotumika kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Uteuzi wa Wagombea na Siku ya Uchaguzi Mkuu. Vile vile, kwa kutumia Idara ya Mpiga Chapa wa Serikali Tume ilichapisha Mfano wa Karatasi za Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu pamoja na Karatasi za Kura kwa ajili ya Uchaguzi katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi tarehe 31 Oktoba, 2010.


  1. Vifaa Vilivyotolewa na UNDP

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kutumia Mradi wa ESP liligharamia na kuipatia Tume vifaa mbalimbali kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Uchaguzi, na kuboreshea Mifumo mbalimbali ya Kompyuta ikiwa ni pamoja na Mfumo wa utunzaji kumbukumbu, Mifumo ya Kuingiza Taarifa za Wagombea kwa njia ya Scanning, Mfumo wa kujumlisha Kura za Urais na Ubunge, Mfumo wa kutoa taarifa za matukio, na Mfumo wa kupata taarifa za Mpiga Kura kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi katika simu ya kiganjani. Vile vile UNDP iligharamia masanduku ya Kura ya ziada na Lakiri.





  1. Vifaa vya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura

na Uchaguzi

Vifaa hivyo ni Fomu za OMR, Storage Units, Vifaa vya kupiga Picha (Photo Solution-Digital Camera Kit and Solar Kit), Karatasi za kuchapisha Picha, Vifutio maalum (dust free erasers), Kalamu maalumu ya risasi kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura; na Masanduku ya Kura ya nyongeza, Lakiri kwa ajili ya kufungia Masanduku ya Kura, Wino usiofutika, Mabegi, Fulana na Kofia kwa ajili ya Watazamaji wa Kimataifa, Kamera na vifaa vya kurekodia matukio mbalimbali na kurudufu, Vifaa vya Elimu ya Mpiga Kura (mabango, vijarida na vipeperushi), Vitabu vya Maelekezo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura, Makarani Waongozaji wa Wapiga Kura na Vyama vya Siasa na Wagombea kwa ajili ya shughuli za Uchaguzi.




  1. Vifaa vya Kuboresha Mifumo ya Kompyuta

Vifaa vilivyotolewa na UNDP kwa ajili ya kuboresha Mifumo mbalimbali ya Kompyuta ni storage units, servers na routers.


  1. Vifaa Vilivyoazimwa kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini

Tume iliazima mashine maalumu (Zip-Zip machines) 1,200 kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini kwa ajili ya kuwasaidia Wapiga Kura kupata majina yao na Vituo walivyopangiwa kupigia Kura kwa urahisi hususan kwa ajili ya Vituo vya Dar es Salaam.
      1. Ugawaji na Usambazaji wa Vifaa vya Uchaguzi


Ugawaji na Usafirishaji wa vifaa kwenda Majimboni ulifanyika mapema ili kutoa nafasi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kuhakiki utoshelevu wa vifaa hivyo na kupata muda wa kukabiliana na upungufu wa vifaa ambao ungejitokeza.

Zoezi la usafirishaji lilifanyika kwa kutumia Wazabuni/Watoa huduma ya usafirishaji ambao walipangwa Kikanda. Wazabuni wa Vifaa vya Uchaguzi walipatikana kwa njia ya ushindani kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma (Sheria Na. 21 ya mwaka 2004) na Kanuni zake za mwaka 2005.


Kwa ujumla, pamoja na mapungufu machache yaliyojitokeza, Ununuzi, Ugawaji na Usambazaji wa Vifaa vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Uchaguzi vilifanikiwa na kuwezesha hatua mbalimbali za mchakato wa Uchaguzi kufanyika kama ilivyopangwa na Tume.
    1. Rasilimali Watu

      1. Makamishna na Watumishi wa Tume


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina Makamishna saba (7) ambao ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine watano (5), Katibu wa Tume ambaye ndiye Mkurugenzi wa Uchaguzi, na Watumishi mia moja na kumi na tisa (119) walioajiriwa kwa Masharti ya Kudumu.
      1. Watumishi Walioajiriwa kwa Mkataba na Walioazimwa


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa na Watumishi Wanne (4) walioajiriwa kwa Mkataba. Watumishi kumi na nne (14) waliazimwa kutoka Wizara na Idara za Serikali:- Madereva wanane (8), Makatibu Muhtasi wawili (2), Wanasheria wawili (2), Maafisa Habari wawili (2). Aidha, Watumishi 674 walitumika kama Vibarua hususan katika Sehemu ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (PNVR) na katika Sehemu ya Manunuzi na Lojistiki.
      1. Watumishi Walioteuliwa na Tume Mikoani na Majimboni


Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina Watumishi wake wa kudumu katika ngazi ya Mikoa, Majimbo, Kata na Vituo. Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi inalazimu kuteua Watumishi wa muda katika kipindi chote cha mchakato wa Uchaguzi ili kutekeleza majukumu mbalimbali katika Mikoa, Majimbo, Kata na Vituo. Walioteuliwa ni wafuatao:-
(a) Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa

Tanzania ina jumla ya Mikoa ishirini na sita (26). Kati ya hiyo Mikoa ishirini na moja (21) ipo Tanzania Bara na Mikoa mitano (5) ipo Tanzania Zanzibar. Mikoa ya Tanzania Bara, kila mmoja ulikuwa na Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa wakati kwa Tanzania Zanzibar kulikuwa na Waratibu wa Uchaguzi wawili (2), mmoja kwa Mikoa yote mitatu (3) ya Unguja na mwingine kwa Mikoa yote miwili (2) ya Pemba.


(b) Wasimamizi wa Uchaguzi Katika Majimbo

Tanzania ina Majimbo 239 ambayo kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi hayana budi kuwa na Msimamizi wa Uchaguzi. Tume iliamua kuweka Msimamizi wa Uchaguzi mmoja kwa kila Halmashauri katika Halmashauri 132 zilizohusika na Uchaguzi Tanzania Bara. Baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi waliwajibika kwa majimbo zaidi ya moja yaliyokuwa katika Halmashauri zao. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam haifanyi Chaguzi, kwakuwa chaguzi zinafanyika katika Halmashauri za Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke zilizo ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa Wilaya kumi (10) za Tanzania Zanzibar, Tume iliamua kuteua Msimamizi mmoja kwa kila Wilaya na hivyo, kufanya jumla ya Wasimamizi wa Uchaguzi nchi nzima kuwa 142.


(c) Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi

Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi Tume imepewa Mamlaka ya kuteua Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika Majimbo na Kata. Tume iliamua kuwa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi watano (5) kwa kila Jimbo la Tanzania Bara, mmoja (1) kwa kila Jimbo huko Tanzania Zanzibar na wawili (2) kwa kila Kata za Tanzania Bara.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kwa jumla kulikuwa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo 995 na ngazi ya Kata 6,670 Tanzania Bara.
(d) Maafisa Uchaguzi wa Halmashauri

Kiutawala Tume ilikuwa na Maafisa Uchaguzi, mmoja kwa kila Halmashauri.


(e) Watendaji Katika Vituo vya Kupigia Kura

Tanzania ilikuwa na Vituo vya kupigia kura 53,039. Kila kituo kilikuwa na Msimamizi wa Kituo mmoja (1), Wasimamizi Wasaidizi wa Kituo wawili (2), Karani Mwongozaji mmoja (1), na Mlinzi wa Kituo mmoja (1) kwa mujibu wa Maelekezo ya Tume. Kwa hiyo, jumla ya Watendaji na Walinzi katika vituo vyote ilifikia 265,195.



Jedwali Na. 8: Idadi ya Watendaji na Walinzi Walioteuliwa



Na.

Ngazi

Idadi

1.

Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa

  • Tanzania Bara - 21

  • Tanzania Zanzibar - 2

23

2.

Wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri/Wilaya (RO)

Tanzania Bara (Halmashauri) - 132

Tanzania Zanzibar - 10


142


3.

Maafisa Uchaguzi katika Halmashauri za Tanzania Bara.

132

4.

Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo

Tanzania Bara - 945



  • Tanzania Zanzibar (Wilaya) - 50

995

5.

Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Tanzania Bara

6,670

6.

Watendaji Ngazi ya Vituo (4 kwa kila Kituo). Vituo vilikuwa 53,039

  • Tanzania Bara - 51,392 Vituo vya Kupigia Kura

  • Tanzania Zanzibar (ZEC) - 1,291 Vituo vya Kupigia Kura

  • Tanzania Zanzibar (NEC) - 356 Vituo vya Kupigia Kura

212,156


7.

Walinzi wa Vituo 1 kwa kila Kituo

Tanzania Bara - 51,392

Tanzania Zanzibar (ZEC) - 1,291

Tanzania Zanzibar (NEC) - 356


53,039





Jumla

273,157

Tume ya Taifa ya Uchaguzi hutumia Vituo vya Tume ya Uchaguzi Zanzibar na Vituo ambavyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi yenyewe inavianzisha kwa ajili ya Wapiga Kura ambao hawakuandikishwa na ZEC lakini wanastahili kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.


      1. Wataalam Washauri


Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, walikuwepo Wataalam Washauri mbalimbali wakiwemo wa UNDP kupitia Mradi wa Kusaidia Uchaguzi (ESP).
Wataalam hao walihusika katika maeneo ya Elimu ya Mpiga Kura, Teknohama, Mafunzo kwa Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Watu wanaoishi na Ulemavu na Makundi maalum.
1   ...   5   6   7   8   9   10   11   12   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət