Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə11/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   ...   33

Changamoto zilizojitokeza


      1. Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2010 kutoandaliwa kwa wakati.

      2. Pendekezo la kuipa Tume mamlaka ya kuandikisha wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoingizwa kwenye marekebisho ya Sheria za uchaguzi.

      3. Kutokutenga fedha kwa ajili ya Kamati za kusimamia utekelezaji wa Maadili ya Uchaguzi.

      4. Mchakato wa kugawa Majimbo kutokamilika kwa wakati. Aidha, baadhi ya Wadau kutaka Majimbo yagawanywe hata baada ya zoezi kukamilika.

      5. Kutokukamilisha Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa wakati.

      6. Kutokutangaza Maeneo ya Uchaguzi (Kata) kwa wakati kutokana na Mchakato wa kugawa Kata kutokamilika mapema.

      7. Mfano wa Karatasi za Kura kutokuchapishwa na kusambazwa kwa wakati

      8. Karatasi za Kura za baadhi ya Majimbo na Kata kutokuchapishwa kwa wakati au kuchapishwa zikiwa na makosa.

      9. Baadhi ya Vifaa vya Elimu ya Mpiga Kura na Vitabu vya Maelekezo kwa Watendaji vilivyochapishwa kwa msaada wa UNDP kutopatikana kwa wakati.

      10. Kamati za Tume zilichelewa kuundwa na hivyo kuchelewa kuanza kazi.

      11. Bajeti ndogo kwa Mafunzo ya Watendaji wa Uchaguzi Majimboni, Katani na Vituoni.

      12. Watendaji wa Uchaguzi Majimboni kuwa na Majukumu mengine mengi zaidi ya Majukumu ya Uchaguzi.

      13. Kupanda kwa gharama za matangazo wakati wa uchaguzi kulifanya Tume kutoa matangazo machache kwa Vyombo vyote vya Habari nchini.

      14. Kuchelewa kuchapishwa na kusambazwa mabango ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na ya Uchaguzi kwa ajili ya Elimu ya Mpiga Kura.

      15. Kuwepo kwa Asasi chache zilizotoa Elimu ya Mpiga Kura.

      16. Kuchelewa kuanza kwa Mradi wa ESP.

      17. Mafunzo kwa baadhi ya Wadau wa Uchaguzi kutolewa bila Kushauriana na Tume.

      18. Baadhi ya Asasi za kiraia zilizopata ufadhili wa UNDP hazikutoa Elimu ya Mpiga Kura.

      19. Kuhusisha wageni kutoa Elimu ya Mpiga Kura bila wao kuwa na uelewa wa kutosha wa Sheria za Uchaguzi na mazingira ya nchi.

      20. Baadhi ya Asasi kushindwa kutofautisha kati ya Elimu ya Uraia na Elimu ya Mpiga Kura.

SURA YA TATU




UANDIKISHAJI NA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA




    1. Uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 5(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na vifungu vya 11 na 12 vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 15B cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, sura ya 292, na kutumika kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Katika kipindi hicho Tume iliandikisha Wapiga Kura 15,919,749 ambao ni sawa na asilimia 96 ya Wapiga Kura 16,578,466 waliokadiriwa kuandikishwa na Tume.

    1. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) na (5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linatakiwa kuboreshwa mara mbili kati ya Chaguzi Kuu mbili zinazofuatana. Katika zoezi la Uboreshaji, Wapiga Kura waliofikia umri wa miaka 18 na kuendelea au ambao hawakujiandikisha wakati uliopita wanapewa nafasi ya kujiandikisha. Aidha, taarifa za Wapiga Kura waliofariki hupokelewa na kuondolewa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Vile vile waliohama kutoka Kata au Jimbo moja na kuhamia Kata au Jimbo jingine taarifa zao zinahamishwa.

    1. Makadirio ya Takwimu za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu

la Wapiga Kura

Tume ya Taifa ya Uchaguzi hufanya Makadirio ya idadi ya Wapiga Kura wote ikijumuisha idadi ya Wapiga Kura Waliofariki, Wapiga Kura waliohama kutoka Kata au Jimbo moja kwenda Kata au Jimbo jingine na Wapiga Kura waliopoteza kadi zao.



(i) Makadirio ya Idadi ya Wapiga Kura Mwaka 2010

Katika kukadiria idadi ya Wapiga Kura waliotarajiwa kujiandikisha, kuboresha taarifa zao, kuondolewa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la mwaka 2005 na watakaohamia maeneo mengine, Tume ilitumia takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Takwimu hizo ni zifuatazo:-




  1. Idadi ya watu waliokadiriwa kufikisha miaka 18 kila mwaka kuanzia 2006 mpaka 2010

2006

2007

2008

2009

2010

833,000

805,000

1,052,000

742,000

1,008,000

Kwa hiyo, Tume ilikadiria watu ambao wangefikia umri wa kujiandikisha kuwa Wapiga Kura ni 4,440,000.




  1. Makadirio ya Wapiga Kura watakaofariki

2006

2007

2008

2009

2010

265,000

270,000

275,000

280,000

285,000

Tume ilikadiria kuwa Watu ambao wangekuwa wamefariki ni 870,000.

Aidha, kwa kuzingatia idadi ya Wapiga Kura walioandikishwa 2005 Tume ilikadiria kwamba:-


  1. Wapiga Kura 1,114,382 ambao ni asilimia saba (7%) wangehama kutoka Kata au Jimbo moja kwenda Kata au Jimbo jingine.

  2. Wapiga Kura 1,591,974 ambao ni asilimia kumi (10%) wangepoteza Kadi za Kupigia Kura.


(ii) Vituo vya Uboreshaji

Vituo vilivyotumika wakati wa Uanzishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2005 ndivyo viliamuliwa na Tume kutumika wakati wa Uboreshaji Awamu ya Kwanza na ya Pili. Idadi ya vituo hivyo ilikuwa 24,813. Katika Awamu ya Kwanza ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura vituo vitatu viliongezeka na kufanya jumla ya Vituo kuwa 24,816. Vituo vilivyoongezeka ni vituo viwili katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kituo kingine katika Jiji la Mbeya.


Katika Awamu ya Pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura vituo viwili viliongezeka na kufanya jumla ya Vituo kuwa 24,818. Kituo kimoja kiliongezeka katika Halmashauri ya Wilaya ya Same na kituo kingine katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Baada ya mgawanyo wa Kata uliofanywa na OWM – TAMISEMI jumla ya Vituo vya Kuandikisha mia moja na tano (105) vilianzishwa wakati wa kurekebisha taarifa za Wapiga Kura.
Baadhi ya Vituo vilihamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo:-

  1. Mabadiliko ya matumizi ya majengo.

  2. Kuharibika kwa majengo yaliyotumika mwaka 2005, hivyo kutofaa kuendelea kutumika kama vituo vya uandikishaji.

  3. Kujengwa kwa majengo ya umma na kutumiwa kama Vituo hususan Shule za Sekondari za Kata.

  4. Kubadilishwa kwa matumizi ya ardhi kulisababisha Vituo kuhamishwa. Mfano, Kata ya Msangaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali iliyobadilishwa kuwa Hifadhi ya Taifa.


Jedwali Na. 9: Idadi ya Vituo vya Kujiandikisha Mwaka 2010



Sehemu ya Jamhuri

Mikoa

Halmashauri/Wilaya (kwa Tanzania Zanzibar)

Majimbo

Kata/

Shehia

Vituo vya kuandikisha

Tanzania

Bara

21

132

189

3,335

24,818


Tanzania

Zanzibar


5

10

50

334

354

Jumla

26

142

239

3,669

25,172
      1. Ratiba ya Utekelezaji


Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilifanyika Kikanda. Awamu ya Kwanza ya Uboreshaji ilianza tarehe 14 Januari, 2008 na kumalizika tarehe 28 Desemba, 2008. Awamu ya Pili ilianza tarehe 31 Agosti, 2009 na kumalizika tarehe 19 Juni, 2010.
Hata hivyo, Tume kama ilivyofanya mwaka 2005, iliwapatia Wapiga Kura fursa ya mwisho kuhamisha taarifa zao. Muda uliotolewa ulikuwa tarehe 1 – 10 Julai, 2010.
Ratiba ya Uboreshaji kwa Awamu zote ni kama ifuatavyo:-

Jedwali Na. 10: Ratiba ya Uboreshaji Awamu ya Kwanza



KANDA/MIKOA

TAREHE

Kanda ya Kwanza

(Mtwara, Lindi)

14/01/2008-19/01/2008

Kanda ya Pili

(Mbeya, Ruvuma, Iringa, Rukwa,)

04/02/2008 – 09/02/2008

Kanda ya Tatu

(Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma)

17/03/2008 - 22/03/2008

Kanda ya Nne

(Kagera, Mwanza)

21/04/2008 - 26/04/2008

Kanda ya Nne

(Mara, Shinyanga)

18/08/2008 – 23/08/2008

Kanda ya Tano

(Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga)

22/09/2008 – 27/09/2008

Kanda ya Sita

(Pwani, Morogoro)

27/10/2008 – 01/11/2008

Kanda ya Saba

(Dar es Salaam)

23/12/2008 – 28/12/2008

Kanda ya Nane

(Zanzibar)

Uboreshaji haukufanyika Awamu hii bali ulifanyika Awamu ya Pili baada ya ZEC kukamilisha.



Jedwali Na. 11: Ratiba ya Uboreshaji Awamu ya Pili

KANDA/MIKOA

TAREHE

Kanda ya Kwanza

( Mtwara, Lindi, Ruvuma, Iringa)

31/08/2009 – 05/09/2009

Kanda ya Pili

(Mbeya, Rukwa, Dodoma, Singida)

21/09/2009 – 26/09/2009

Kanda ya Tatu

(Tabora, Shinyanga, Kigoma)

23/11/2009 – 28/11/2009

Kanda ya Nne

(Mara, Kagera, Mwanza)

21/12/2009 – 26/12/2009

Kanda ya Tano

(Kilimanjaro, Arusha, Manyara)

25/01/2010 – 30/01/2010

Kanda ya Sita

(Tanga, Pwani, Morogoro)

22/02/2010 – 27/02/2010

Kanda ya Saba

(Dar es Salaam)

22/03/2010 – 28/03/2010 na Marudio 22/05/2010 -23/05/2010

Kanda ya Nane

(Zanzibar)

14/06/2010 – 19/06/2010

Kanda Kwanza - Saba (Tanzania Bara)

Kuhamisha taarifa za Wapiga Kura kwa mara ya mwisho

01/07/2010 – 10/07/2010
      1. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yalianza mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Maandalizi hayo yalikuwa ni pamoja na:-

      1. Marekebisho ya makosa mbalimbali yaliyoonekana katika Daftari lililotumika katika Uchaguzi wa 2005.

      2. Marekebisho ya Sheria na Kanuni za Uchaguzi.

      3. Kufanya Ukarabati wa kituo kipya cha kuandalia Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Kuhamisha vifaa vya Daftari kutoka Baraza la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education – NACTE) na kuviweka katika kituo kipya cha sasa kilichoko kwenye Bohari ya Wakala wa Ununuzi Serikalini (Government Procurement Services Agency - GPSA).

      4. Kufanya maandalizi mbalimbali ya Fomu za Uboreshaji kufuatia changamoto zilizojitokeza katika Uchaguzi wa 2005.

      5. Kufanya maboresho ya Mfumo wa Daftari pamoja na Mifumo mingine ambayo imeunganishwa nayo (Intergrated System).

      6. Kufanya tathmini ya njia mbalimbali za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

      7. Kuandaa Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

      8. Kuandaa maelekezo kwa Watendaji na Viongozi wa Vyama vya Siasa na Mawakala.

      9. Kutoa mafunzo kwa Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.




  1. Awamu ya Kwanza ya Uboreshaji wa Daftari la

Kudumu la Wapiga Kura

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza ulianza tarehe 14 Januari, 2008 katika Kanda ya kwanza (1) na kumalizika tarehe 28 Desemba, 2008 katika Kanda ya saba (7). Uboreshaji ulifanyika kikanda kwa siku sita (6), Vituo vya Uandikishaji vilifunguliwa saa 2.00 Asubuhi na kufungwa saa 12.00 Jioni.

Kutokana na Uboreshaji wa Awamu ya Kwanza, Wapiga Kura walioandikishwa waliongezeka kutoka 15,935,493 (mwaka 2005) na kufikia 18,014,871 (mwaka 2008), ambayo ni sawa na ongezeko la Wapiga Kura 2,079,378. Aidha, Wapiga Kura 806,170 walipatiwa Kadi mpya za Kupigia Kura au kuhamisha taarifa zao kwenda kwenye Vituo vipya walivyohamia. Pia, Wapiga Kura waliofutwa kutokana na kutolewa taarifa za vifo ni 69,161.


  1. Awamu ya Pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Uboreshaji wa Awamu ya Pili ulianza tarehe 31 Agosti, 2009 na kumalizika tarehe 19 Juni, 2010. Uboreshaji ulifanyika kwa siku sita (6) kuanzia saa 2.00 Asubuhi hadi saa 12.00 Jioni, isipokuwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo Uboreshaji ulifanyika kwa siku saba (7) na ililazimika kurudia tena kwa siku 2 kuanzia tarehe 22 Mei, 2010 hadi 23 Mei, 2010 kutokana na idadi kubwa ya Wapiga Kura kutojitokeza katika siku zilizopangwa.

Katika Awamu ya Pili ya Uboreshaji, Tume pia iliwaandikisha Wapiga Kura waliotegemewa kufikisha umri wa miaka 18 siku ya Uchaguzi, kama ilivyofanyika wakati wa Uanzishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2005. Aidha, marekebisho yafuatayo yalifanyika:-





  1. Kuondoa Wapiga Kura waliotolewa taarifa kuwa wamefariki ambao idadi yao ilifikia 243,630.

  2. Kuhakiki na kuwaondoa Wapiga Kura 214,125 waliojiandikisha zaidi ya mara moja Katika Daftari. Wapiga Kura hao waliachwa katika kituo kimoja walichojiandikishia mwisho.

  3. Kuondoa Wapiga Kura 15,873 waliojiandikisha, ambao walionekana kutokuwa na Sifa za kuwa Wapiga Kura kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwa na umri chini ya miaka 18 na kutokuwa raia.



1   ...   7   8   9   10   11   12   13   14   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət