Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə8/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   4   5   6   7   8   9   10   11   ...   33

Misaada ya Washirika wa Maendeleo Kupitia Programu ya Kukuza Demokrasia Tanzania (DDTP) na Mradi wa Kusaidia Uchaguzi (ESP)

Baada ya mashauriano Kati ya Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na UNDP ilikubaliwa kuanzisha Programu ya Kukuza Demokrasia Nchini (Deepening Democracy Tanzania Programme) na Mradi wa Kusaidia Uchaguzi (Election Support Project) kwa nyakati tofauti.


      1. Programu ya Kukuza Demokrasia Nchini (DDTP)


Programu hii ilianzishwa tarehe 30 Januari, 2007 ili kusaidia na kuendeleza juhudi za Serikali za kukuza Demokrasia baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Programu hii iligharimu kiasi cha Dola za Marekani 21,543,396.72 (Sh. 28,006,415,736.00). Programu hii ilitekelezwa kwa njia ya “National Execution” (NEx), ambapo Taasisi zilizohusika katika Programu zilipelekewa fedha na UNDP kwa ajili ya kutekeleza shughuli zilizohusika.
Taasisi hizo ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Kituo cha Demokrasia, Bunge, Baraza la Wawakilishi, “African Peer Review Mechanism” (APRM) na Tume za Uchaguzi (NEC na ZEC) kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 4.
Jedwali Na. 4: Mgawanyo wa Fedha za Programu ya DDTP



Na.

Shughuli zilizopangwa

Fedha iliyotolewa

Dola za Marekani

Sh.

1

Kuanzisha African Peer Review Mechanism (APRM)

1,194,500.74


1,552,850,962.00



2

Kujenga uwezo kwa Tume za Uchaguzi (NEC na ZEC)

15,388,329.62


20,004,828,506.00



3

Kuandaa Mpango Mkakati wa Utoaji Elimu ya Uraia (Civic Education)

374,052.79


486,268,627.00



4

Kuimarisha Utawala Bora - Bunge

963,279.30


1,252,263,090.00



5

Kuimarisha Utawala Bora - Baraza la Wawakilishi

898,532.49


1,168,092,237.00



6

Kuimarisha Utawala Bora - Msajili wa Vyama vya Siasa

175,487.35


228,133,555.00



7

Kuimarisha Utawala Bora – Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)

641,190.10


833,547,130.00



8

Menejimenti ya Programu

1,908,024.33

2,480,431,629.00





JUMLA


21,543,396.72


28,006,415,736.00

Kiwango cha kubadili fedha ni Dola 1 ya Marekani = Sh. 1,300/=
Washirika wa Maendeleo waliochangia Programu hii ni UNDP, DFID(UK), Sweden, Denmark, Netherlands, CIDA na Norway.


  1. Shughuli zilizotekelezwa na Tume chini ya Programu ya DDTP

Kati ya fedha zote zilizotolewa na DDTP kwa Tume za Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipata kiasi cha Dola za Marekani 11,106,974.49 (Sh.14,439,066,837/=). Fedha hizo zilitumika kwa ajili ya kuijengea uwezo Tume, kugharamia Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuiwezesha Tume kuandaa Mpango Mkakati, kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja na Mkakati wa Utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura.


  1. Mchanganuo wa matumizi ya Fedha zilizotolewa na DDTP kwa Tume

Fedha zilizotolewa na DDTP zilitumika kwa shughuli zinazooneshwa katika Jedwali Na. 5.
Jedwali Na. 5: Mchanganuo wa Fedha za DDTP Mwaka 2007 – 2009



Na.

Shughuli

Mwaka

Kiasi

Dola za Marekani

Sh.

1

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza

2008

3,056,209.62


3,973,072,506.00



2

Uboreshaji wa Sheria za Uchaguzi, Elimu ya Mpiga Kura, mafunzo kwa watumishi, Ununuzi wa Vifaa, kuendesha mikutano na warsha.

2007

198,685.49

258,291,137.00

2008

189,917.00

246,892,100.00

2009

302,056.30

392,673,190.00

3

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili

2009

7,360,106.08

9,568,137,904.00




JUMLA




11,106,974.49

14,439,066,837.00

Kiwango cha kubadili fedha ni Dola 1 ya Marekani = Sh. 1,300/=
Programu hii ilimalizika mwezi Juni, 2010. Kufikia Desemba 2009, shughuli zilizokuwa zinaendelea kutekelezwa na Tume za Uchaguzi (NEC na ZEC) zilijumuishwa kwenye shughuli za ESP.
      1. Mradi wa Kusaidia Uchaguzi (ESP)


Mradi wa Kusaidia Uchaguzi (ESP) ilizinduliwa tarehe 15/06/2010 na kuendeleza kazi mbalimbali zilizoanza na kutekelezwa na Programu ya DDTP ambazo zililenga zaidi kufanikisha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Mradi huu tofauti na DDTP ulisimamiwa na kutekelezwa na UNDP kwa njia ya Direct Execution (DEx) ambapo baada ya kukubaliana shughuli/kazi hutekelezwa moja kwa moja na UNDP kwa kufuata Sheria na Kanuni za UNDP.
Mradi huu ulichangiwa Jumla ya Dola za Marekani Milioni 28 na Washirika wa Maendeleo mbalimbali wakiwemo; UNDP, DFID(UK), Sweden, Finland, European Union, Denmark, Netherlands, Switzerland, Ireland, Canada, Germany, Norway, na Belgium.
Mgawanyo wa Fedha zilizotolewa na ESP ni kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 6.

Jedwali Na. 6: Mgawanyo wa Fedha za Mradi wa ESP



Na.

Shughuli

Kiasi

Dola za Marekani

Sh.

1

Kuzijengea uwezo Tume za Uchaguzi (NEC na ZEC).

9,382,000


13,556,990,000



2

Asasi za Kiraia zilitoa Elimu ya Mpiga Kura.

6,025,000

8,706,125,000

3

Kujengea Uwezo Vyombo vya Habari.

1,470,000

2,124,150,000

4

Kujenga uwezo kwa kutoa Mafunzo mbalimbali kwa Vyama vya Siasa.

1,920,000

2,774,400,000

5

Uanzishaji wa Kituo cha kusajili Watazamaji wa Uchaguzi.

2,150,000

3,106,750,000

6

Kusaidia Taasisi zinazosimamia Amani na Utulivu.

2,770,000

4,002,650,000

7

Ufuatiliaji na tathimini (M&E).

2,056,000

2,970,920,000

8

Dharura.

1,000,000

1,445,000,000

9

Malipo ya Menejimenti ya Programu.

1,874,110

2,708,089,000




JUMLA

28,647,110

41,395,074,000

Kiwango cha kubadili fedha ni Dola 1 ya Marekani = Sh. 1,445/=

  1. Shughuli zilizotekelezwa na Tume chini ya Mradi wa ESP

Kati ya fedha zote zilizotengwa na ESP kwa Tume za Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipata kiasi cha Dola za Marekani 3,104,070.00 (Sh.4,485,381,150/=) kabla ya Uchaguzi Mkuu. Fedha hizo zilitumika kwa:- Ununuzi wa Vifaa vya Uchaguzi kama vile: Masanduku ya Kura, Lakiri na Wino usiofutika; Kuboresha Mifumo ya Kompyuta; Mafunzo kwa Watumishi; Kuweka vifaa vya usalama katika majengo ya Tume; na Kuboresha maghala ya Tume.
Aidha, baada ya Uchaguzi Mkuu, 2010 jumla ya Dola za Marekani 2,393,000.00 (TSh.3,457,885,000) zimetengwa kwa ajili ya shughuli zifuatazo:- Kuendeleza TEKNOHAMA, Mafunzo kwa Watumishi, Matengenezo ya vifaa vya Upigaji wa Picha na Nishati ya Jua, kuweka vifaa vya Usalama katika Kituo cha Maandalizi ya Daftari na maghala, na Ukarabati wa maghala.


  1. Mchanganuo wa matumizi ya Fedha zilizotengwa na ESP kwa Tume

Fedha zilizotolewa na ESP zilitumika kwa shughuli zinazooneshwa katika Jedwali Na. 7.

Jedwali Na. 7: Mchanganuo wa Fedha za ESP Mwaka 2010 – 2011



Na.

Shughuli

Kiasi

Dola za Marekani

Sh.

A

Kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2010

1

Ununuzi wa Vifaa vya Uchaguzi kama vile Masanduku ya Kura na Lakiri

927,983

1,340,935,435

2

Ununuzi wa Wino usiofutika

744,877

1,076,347,265

3

Kuendeleza TEKNOHAMA – Kuimarisha Mfumo wa Menejimenti ya Matokeo ya Uchaguzi

465,000

671,925,000

4

Mafunzo kwa Watumishi wa Mfumo wa Matokeo ya Uchaguzi

203,000

293,335,000

5

Kuimarisha mahusiano na Wadau, Kuchapisha Zana za Elimu ya Mpiga Kura, Kutoa Ushauri wa Kitaalamu katika Tume, Mawasiliano ya moja kwa moja na Wapiga Kura (Hotline), Malipo ya sehemu ya Kusajili Watazamaji wa Uchaguzi na kutangaza Matokeo.

763,210

1,102,838,450




Jumla Ndogo

3,104,070

4,485,381,150

B

Baada ya Uchaguzi Mkuu Novemba, 2010 – Juni, 2011

1

Kuendeleza TEKNOHAMA (Storage, Generator, Oracle and Window)

414,000

598,230,000

2

Mafunzo kwa Watumishi

58,000

83,810,000

3

Matengenezo ya Vifaa vya upigaji Picha na Nishati ya Jua

321,000

463,845,000

4

Kuweka vifaa vya usalama katika Kituo cha maandalizi ya Daftari na maghala

400,000

578,000,000

5

Ukarabati wa maghala

1,200,000

1,734,000,000




Jumla Ndogo

2,393,000

3,457,885,000




Jumla Kuu

5,497,070

7,943,266,150

Kiwango cha kubadili fedha ni Dola 1 ya Marekani = Sh. 1,445/=

(c) Mafanikio ya Mradi wa ESP

Kwa ujumla Programu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu malengo yaliyotarajiwa katika kuzijengea uwezo Tume za Uchaguzi za NEC na ZEC, Vyombo vya Habari, Vyama vya Siasa na Asasi za Kiraia yalitimizwa. Aidha, Mradi huu ulisaidia kuhamasisha makundi maalumu kushiriki katika Uchaguzi hususan Wanawake, Vijana na watu wanaoishi na Ulemavu.


1   ...   4   5   6   7   8   9   10   11   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət