Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə6/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   33

Kutangazwa kwa Maeneo ya Uchaguzi (Kata)


Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi (Sura za 343 na 292), Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kutangaza maeneo ya Uchaguzi (Kata). Hata hivyo jukumu la kugawa Kata ni la Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM– TAMISEMI).
OWM-TAMISEMI ilichelewa kugawa Kata hivyo Tume nayo ilichelewa kutangaza maeneo ya Uchaguzi. Tume ilitangaza Kata 3,337 katika Gazeti la Serikali Na. 271 la tarehe 30 Julai, 2010.
Baada ya Kutangaza kata hizo, baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi walitoa taarifa kwamba kuna kata nne (4) kati ya zilizotangazwa hazipo au zimetangazwa kwa majina mawili tofauti. Kata ambazo hazipo ni Lisekese katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na Katumba katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Kata zilizotangazwa kwa majina mawili tofauti ni Mugumu Mjini na Mugumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Mwinkasi na Endakiso katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Kuna Kata tano (5) ambazo zilisahaulika wakati wa kutoa tangazo, Kata hizo ni:- Nduli katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mateves katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Lyambamgongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Majimoto na Nsekwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Vile vile Kata mbili (2) zilitangazwa mara mbili ambazo ni: Mkako katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Kiruruma katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
Aidha, katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ilionekana kama imetangazwa Kata moja (1) zaidi ambavyo sivyo.
    1. Marekebisho ya Sheria na Kutungwa kwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya mapitio ya Sheria za Uchaguzi ili kubaini maeneo yanayotakiwa kurekebishwa. Kutokana na mapitio hayo, Tume iliwasilisha mapendekezo Serikalini ya kuzifanyia Marekebisho Sheria za Uchaguzi kwa lengo la kuziboresha ili kuongeza ufanisi katika kusimamia, kuendesha na kuratibu mchakato wa Uchaguzi nchini.


      1. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292

Marekebisho yaliyofanyika katika Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ni haya yafuatayo:-



  1. Kuweka kipindi cha Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa mara mbili kati ya Chaguzi Kuu mbili zinazofuatana.

  2. Kutoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kuwateua Waratibu wa Uandikishaji wa Mikoa.

  3. Kuruhusu Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa na Maafisa wa Tume kuingia katika Vituo vya kupigia Kura.

  4. Kutoa ruhusa kwa Vyama vya Siasa kuweka Mawakala katika vituo vya kuandikisha Wapiga Kura.

  5. Kuipa Tume mamlaka ya kutayarisha Maadili ya Uchaguzi, na Maadili hayo kuwa na nguvu ya Kisheria.

  6. Kuondoa vifungu vya Sheria vinavyoruhusu utoaji wa Takrima.

  7. Kutoa jukumu kwa Mahakama ya Rufaa kuijulisha Tume matokeo ya Rufaa za Malalamiko ya Uchaguzi.

  8. Kuongeza muda wa siku za kufungua Malalamiko ya Uchaguzi kupinga matokeo ya Uchaguzi kwa Uchaguzi wa Wabunge katika Mahakama Kuu kutoka siku 14 hadi siku 30.

  9. Kupunguza ukomo wa muda wa kusikiliza na kuamua Malalamiko ya Uchaguzi katika Mahakama Kuu kutoka miaka miwili hadi mwaka mmoja.

  10. Kuweka Ukomo wa Muda wa kusikiliza na kuamua Rufaa za Malalamiko ya Uchaguzi katika Mahakama ya Rufaa kuwa ni mwaka mmoja.

  11. Kuweka Ukomo wa Muda wa kusikiliza na kuamua Malalamiko ya Madiwani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kuwa ni miezi 18.

  12. Kuipa Tume mamlaka ya kufanya Chaguzi Ndogo za Madiwani mara mbili kwa mwaka badala ya kufanya ndani ya siku 90 kila nafasi wazi zinapotokea.

  13. Kuweka taratibu za kuteua na kutangaza Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum.

  14. Kuongezwa kifungu kipya cha 124A kinachoipa Tume mamlaka ya kuandaa Maadili ya Uchaguzi.

  15. Kuongezwa kifungu kipya cha 50A katika Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu kipya cha 52A katika Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kuhusu Pingamizi ya Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya Mgombea kwa Tume na ukiukwaji wa Sheria ya gharama za Uchaguzi, 2010.

Baada ya Bunge kupitisha marekebisho ya Sheria za Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliandaa Matoleo ya Sheria za Uchaguzi (Sura za 343 na 292) yaliyojumuisha marekebisho yote yaliyofanyika mwaka wa 2010. Vile vile matoleo hayo yalitafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.


      1. Kanuni za Uchaguzi


Sheria za Uchaguzi zinaelekeza kutungwa kwa Kanuni zinazowezesha utekelezaji wa mchakato wa Uchaguzi kwa ufanisi zaidi. Hivyo, Tume iliandaa Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2010 zilizotoa ufafanuzi zaidi wa jinsi ya kutekeleza matakwa ya Sheria za Uchaguzi.
Aidha, Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2010 zimeelezea utaratibu wa kushughulikia Pingamizi za Msajili wa Vyama vya Siasa ambazo taratibu hizo ni sawa na zile za kushughulikia Pingamizi wakati wa Uteuzi wa Wagombea, isipokuwa Pingamizi za Msajili wa Vyama vya Siasa zinaweza kuwekwa wakati wowote baada ya muda wa kutoa pingamizi kupita.
Hivyo, Pingamizi ya Msajili inayohusiana na Uteuzi wa Diwani, inawasilishwa kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata husika. Pingamizi inayohusu Uteuzi wa Mbunge inapelekwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo husika na ya Uteuzi wa Rais inapelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Rufaa kuhusiana na Pingamizi za Msajili wa Vyama vya Siasa zinafuata utaratibu ule ule ulioainishwa katika Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake. Kama zilivyo kwa Pingamizi/Rufaa zinazohusiana na Uteuzi wa Wagombea uamuzi utakaotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi utakuwa ni wa mwisho.
    1. Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya Mwaka 2010


Madhumuni ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi ni kuweka utaratibu wa kisheria wa kudhibiti, kusimamia na kuratibu mapato na matumizi ya gharama za Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa na Wagombea wakati wa Uchaguzi, na kudhibiti vitendo vya rushwa.
Masuala yanayohusiana na mchakato wa Uchaguzi katika Sheria hiyo ni pamoja na:-

  1. Kumtaka Mgombea Uchaguzi kutoa taarifa kwa Chama chake kuhusu fedha alizonazo na anazotegemea kupokea kwa ajili ya matumizi katika Uchaguzi ndani ya siku saba (7) baada ya Siku ya Uteuzi. Maelezo hayo yanatakiwa yatolewe kwa Katibu Mkuu wa Chama endapo ni Uchaguzi wa Rais au kwa Katibu wa Chama wa Wilaya husika endapo ni Uchaguzi wa Mbunge au Diwani. Baada ya Makatibu wa Vyama kupokea taarifa hizo wanatakiwa ndani ya siku thelathini (30) baada ya Siku ya Uteuzi kuwasilisha taarifa hizo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

  2. Kukitaka kila Chama kinachoshiriki katika Uchaguzi kutoa taarifa ya fedha kitakazotumia.

  3. Mgombea au Chama cha Siasa ambacho hakitaeleza kuhusu kiasi cha fedha kinachotarajia kutumia katika Uchaguzi kitaondolewa kushiriki katika Uchaguzi.

  4. Kumpa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuweka Pingamizi dhidi ya Mgombea au Chama husika kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  5. Kubainisha vitendo vinavyokatazwa kufanywa na Wagombea au Vyama vya Siasa wakati wa Mchakato wa Uteuzi ndani ya Vyama vya Siasa na wakati wa Uchaguzi. kifungu cha 24 cha Sheria ya Gharama za Uchaguzi kinaeleza kwamba Mgombea au Chama cha Siasa kitakachofanya vitendo hivyo basi kitaondolewa kushiriki katika Uchaguzi.

  6. Kumpa Msajili wa Vyama vya Siasa mamlaka ya kuweka pingamizi kwa Tume dhidi ya Chama/Mgombea ambaye ametenda vitendo vilivyokatazwa, ili aondolewe kushiriki katika Uchaguzi.
1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət