Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə2/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   33

ORODHA YA MAJEDWALI




ORODHA YA VIAMBATISHO





Kiambatanisho A: Orodha ya Kata Zilizofanya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 89

Kiambatanisho B: Asasi za Kiraia Zilizoruhusiwa Kutoa Elimu ya Mpiga 93

Kiambatanisho C: Hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi 96

Kiambatanisho D: Asasi za Kiraia Zilizoruhusiwa kuwa Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Mkuu, 2010 100

Kiambatanisho E: Risala ya Mwenyekiti Kuhusu Siku ya Upigaji Kura 106

Kiambatanisho F: Orodha ya Majimbo ya Uchaguzi Mkuu, 2010 110

Kiambatanisho G: Kata Ambazo Wagombea Udiwani Walipita bila Kupingwa 116


ORODHA YA MICHORO



VIFUPISHO

ARO - Assistant Registration Officer/Assistant Returning Officer

AFP - African Farmers Party

APPT-Maendeleo - African Progressive Party of Tanzania

APRM - African Peer Review Mechanism

AU - African Union

CCM - Chama cha Mapinduzi

CCT - Christian Council of Tanzania

CHADEMA - Chama cha Demokrasia na Maendeleo

CHAUSTA - Chama cha Haki na Ustawi Tanzania

CIDA - Canadian International Development Agency

CMS - Candidate Management System

CUF - Civic United Front (Chama cha Wananchi)

Daftari - Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

DDTP - Deepening Democracy Tanzania Programme

DFID (UK) - Department For International Development (UK)

DP - Democratic Party

ECF – SADC - Electoral Commissions Forum of SADC Countries

EOG - Ecumenical Observer Group

ESP - Election Support Project

EU - European Union

EU – EOM - European Union – Election Observation Mission

GIS - Geographical Information System

GPS - Global Positioning of Satelite

ICR - Intelligent Character Recognition

IGP - Inspector General of Police

IT - Information Technology

JWTZ - Jeshi la Wananchi wa Tanzania

MAKINI - Demokrasia Makini

NACTE - National Council for Technical Education

NBS - National Bureau of Statistics

NCCR-Mageuzi - National Convention for Construction and Reform

NEC - National Electoral Commission

NGO - Non-Governmental Organization

NLD - National League for Democracy

NRA - National Reconstruction Aliance

OCR - Optical Character Recognition

OMR - Optical Mark Recognition

OWM-TAMISEMI - Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

PNVR - Permanent National Voters’ Register

PNVRS - Permanent National Voters’ Registration System

RMS - Result Management System

RO - Registration Officer/Returning Officer

SAU - Sauti ya Umma

Sh. - Shilingi ya Tanzania

SMS - Short Messages System

TADEA - Tanzania Democratic Alliance Party

TCD - Tanzania Centre for Democracy

TEMCO - Tanzania Election Monitoring Committee

TEKNOHAMA - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

TLP - Tanzania Labour Party

Tume - Tume ya Taifa ya Uchaguzi

UDP - United Democratic Party

UMD - Union for Multi-Party Democracy

UNDP - United Nations Development Programme

UPDP - United People’s Democratic Party

WLMS - Warehouse and Logistics Management System

ZEC - Zanzibar Electoral Commission




SHUKRANI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na kuwa ndicho chombo pekee chenye mamlaka ya kisheria ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi, inaamini kwamba ufanisi wake unachangiwa na misaada ya namna moja au nyingine kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.


Kwa mantiki hiyo, Tume kwa njia ya pekee, inapenda kutoa shukrani zake za moyo wa dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha. Pia inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha, Tume inawashukuru Watendaji wote wa hatua mbalimbali kuanzia ngazi ya Taifa hadi Kituo na Wadau Mbalimbali vikiwemo Vyama vya Siasa na Wagombea, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Washirika wote wa Maendeleo hasa walioko chini ya Basket Group, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi Tanzania na Vyombo vingine vya Usalama na Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini.
Mwisho, Tume inavishukuru Vyombo vya Habari, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Watazamaji wa Uchaguzi, Wapiga Kura na Watanzania wote kwa ujumla.

BARUA YA UWASILISHAJI




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


Anuani ya Simu: “UCHAGUZI”

Simu Na: 2114963 – 6,

Nukushi Na: 2113382/2116740,

Barua pepe: uchaguzitanzan@yahoo.com

Tovuti: www.nec.go.tz



Posta House,

Ohio/Ghana Street,

S. L. P 10923,



Dar es Salaam.

Unapojibu tafadhali taja:

Kumb. Na. EA.74/183/01/...... .... June, 2011

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Ikulu,

S. L. P. 9120,



DAR ES SALAAM.
Mheshimiwa Rais,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa Januari, 1993 chini ya Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Wajumbe wote saba wa Tume iliyosimamia Uchaguzi wa Rais, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uchaguzi wa Madiwani Tanzania Bara mwaka 2010 waliteuliwa nyakati mbalimbali na wewe Mhe. Rais. Wajumbe hao ni Mhe. Jaji (Mst.) Lewis M. Makame ulimteua tena kuwa Mwenyekiti tarehe 15 Juni, 2006, Mhe. Omar O. Makungu ulimteua tena kuwa Makamu Mwenyekiti tarehe 26 Juni, 2010. Vile vile uliwateua tena Waheshimiwa Prof. Amon E. Chaligha tarehe 20 Aprili, 2010, Mhe. Hilary J. Mkatte tarehe 21 Septemba, 2010, Mhe. Mchanga H. Mjaka tarehe 26 Juni, 2010. Pia uliwateua Mhe. Jaji (Mst.) John J. Mkwawa tarehe 1 Juni, 2007 na Mhe. Jaji (Mst.) Mary H. C. S. Longway tarehe 15 Juni, 2008. Kila Mjumbe wa Tume huteuliwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe ya uteuzi wake.
Majukumu ya Tume, chini ya Ibara za 74 (6) na 78 (1) ya Katiba, na Sheria za Uchaguzi ni:


  1. Kusimamia na kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara;




  1. Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani katika Tanzania Bara;




  1. Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Majimbo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge;




  1. Kuwatangaza wanawake waliotimiza masharti kwamba wamechaguliwa kuwa Wabunge au Madiwani wa Viti Maalum vya Wanawake;




  1. Kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchini kote na kuratibu na kusimamia Watu/Taasisi zote zinazoendesha Elimu hiyo; na




  1. Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Mheshimiwa Rais, Tume ilitekeleza majukumu yake wakati wote kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sheria za Uchaguzi, Kanuni na Maadili ya Uchaguzi.


Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Tume imefanikiwa kutunza na kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Uboreshaji wa Daftari uliwezesha kuandikishwa Wapiga Kura ambao hawakuandikishwa hapo awali kwa sababu moja au nyingine. Vilevile, wale waliohitaji kufanya masahihisho au marekebisho ya taarifa zao za awali waliweza kufanya hivyo, wale waliopoteza sifa waliondolewa kutoka katika Daftari hilo na waliohamia maeneo mengine taarifa zao zilihamishiwa katika vituo vyao vipya.
Mheshimiwa Rais, mwaka 2010 Tume ilisimamia na kuendesha Uchaguzi Mkuu kwa mafanikio ambayo pia yalichangiwa na kushirikisha Wadau mbalimbali katika mchakato wa Uchaguzi.
Mheshimiwa Rais, kwa heshima tunaomba kuwasilisha kwako Taarifa yetu kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Asante,

................................

(Mst. Jaji Lewis M. Makame)

Mwenyekiti
........................................

(Jaji Omar O. Makungu)



Makamu Mwenyekiti
............................... ..................................

(Prof. Amon E. Chaligha) (Hilary J. Mkatte)



Mjumbe Mjumbe

................................... ................................

(Mchanga H. Mjaka) (Mst. Jaji John J. Mkwawa)

Mjumbe Mjumbe
................................

(Mst. Jaji Mary H. C. S. Longway)



Mjumbe

………………………………………..

(Rajabu R. Kiravu)

Mkurugenzi wa Uchaguzi

na Katibu wa Tume

1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət