Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə5/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   33

Chaguzi Ndogo Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005


Baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka, 2005 zilifanyika Chaguzi Ndogo 6 za Bunge katika Majimbo ya Tunduru, Kiteto, Tarime, Mbeya Vijijini, Busanda na Biharamulo Magharibi ambazo zilisababishwa na vifo vya waliokuwa Wabunge wa Majimbo hayo.
Aidha, jumla ya Chaguzi ndogo sabini na tano (75) za Madiwani zilifanyika. Kata zilizohusika katika Chaguzi hizo ni kama inavyooneshwa katika kiambatisho A.

SURA YA PILI




MAANDALIZI YA UCHAGUZI


Maandalizi ya Uchaguzi yanajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo Kuchunguza na Kugawa Majimbo ya Uchaguzi/Kutangaza maeneo ya Uchaguzi, Kupitia na kupendekeza marekebisho ya Sheria za Uchaguzi, Kuandaa na kuwasilisha Bajeti ya Uchaguzi Serikalini, Kuboresha Mifumo ya Kompyuta, Kutoa Elimu ya Mpiga Kura, Kuteua na kutoa mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi, Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Kununua na kusambaza vifaa vya Uboreshaji na vya Uchaguzi hadi Vituoni.


    1. Ugawaji wa Majimbo na Kutangaza Maeneo ya Uchaguzi (Kata)

Kugawa Majimbo ya Uchaguzi na kutangaza Maeneo ya Uchaguzi (Kata) kwa kawaida hufanyika kabla ya mwaka wa Uchaguzi ili shughuli za awali kama vile Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ufanyike kwa kuzingatia mipaka mahsusi na Bajeti iweze kuandaliwa kwa kutilia maanani hali halisi.


Tume haina budi kuzingatia, pamoja na mambo mengine, matakwa ya sheria, vigezo na taarifa za Kata kutoka OWM-TAMISEMI.
      1. Msingi wa Kisheria


Kwa mujibu wa Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa Mamlaka ya kuchunguza Mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge. Tume inatakiwa kufanya Uchunguzi wa Mipaka na kugawa Majimbo mara kwa mara, na angalau kila baada ya miaka kumi.
Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume inatangaza Maeneo ya Uchaguzi (Kata) baada ya kupata Orodha ya Kata kutoka OWM-TAMISEMI.
Kanuni za Uchaguzi Mkuu za Mwaka 2010 zinaelezea utaratibu utakaotumika katika kupata na kuwasilisha maombi ya kugawa, kubadili majina au kurekebisha mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
      1. Ugawaji wa Majimbo Kabla ya Mwaka 2010


Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuundwa mwaka 1993, Tume ilifanya Uchunguzi wa mipaka ya Majimbo, kwa mara ya kwanza, mwaka 1995 ambapo jumla ya Majimbo mapya hamsini na mbili (52) yaliongezwa kutoka katika Majimbo 180 yaliyokuwepo na kufanya jumla ya Majimbo ya Uchaguzi kuwa 232.
Mwaka 2000 Tume ilifanya Uchunguzi wa Mipaka ya Majimbo kwa kiwango kidogo ambapo ilifuta Jimbo la Mitema kwa sababu lilikuwa katika Halmashauri mbili tofauti za Newala na Tandahimba. Kwa hiyo, Majimbo ya Uchaguzi yakawa 231 badala ya 232.
Aidha, mwaka 2005 Tume iliongeza jimbo moja la Kibaha Mjini kutokana na kuanzishwa kwa Halmashauri mpya ya Mji wa Kibaha, ilifanya marekebisho ya Mipaka ya Majimbo ya Halmashauri za Babati na Korogwe kutokana na kuanzishwa kwa Halmashauri mpya za Miji katika Wilaya hizo na ilifanya Mabadiliko katika majina ya Majimbo ya Uchaguzi katika Jiji la Mwanza kutokana na Mabadiliko ya baadhi ya Kata kuhamishiwa katika Jimbo jingine, kuongezwa kwa Kata mpya na kuanzishwa kwa Wilaya mpya za llemela na Nyamagana. Mipaka ya majimbo ya Uchaguzi ya Tanzania Zanzibar ilifanyiwa marekebisho bila kubadili idadi ya Majimbo ambayo ni hamsini (50). Kwa hiyo, idadi ya Majimbo ya Uchaguzi kwa ujumla ikawa 232 badala ya 231 ya mwaka 2000.
      1. Vigezo vya Kugawa Majimbo


Kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Tume iliamua kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo ya Uchaguzi. Katika kufanya zoezi hilo, Tume iliweka Vigezo vitakavyotumika kuchunguza Mipaka na kugawa Majimbo ya Uchaguzi.
Vigezo vilivyobainishwa ni vile vilivyopo katika Katiba ya Nchi ambavyo ni Idadi ya Watu, Upatikanaji wa Mawasiliano na Hali ya Kijiografia. Aidha, Tume baada ya kujifunza kutoka Nchi za Zambia, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini na Botswana na pia kupata ushauri kutoka kwa Wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Vyama vya Siasa iliongeza vigezo vingine ambavyo ni:- Mgawanyo wa Wastani wa Idadi ya Watu (Population Quota), Hali ya Kiuchumi ya Jimbo, Ukubwa wa Eneo la Jimbo husika, Mipaka ya Kiutawala, Jimbo moja lisiwe ndani ya Wilaya/ Halmashauri mbili, Kata moja isiwe ndani ya Majimbo Mawili na Mpangilio wa Maeneo ya Makazi ya Watu yaliyopo (Existing Pattern of Human Settlement), Mazingira ya Muungano, Uwezo wa Ukumbi wa Bunge na Idadi ya Viti Maalum vya Wanawake.
      1. Taratibu za Ugawaji wa Majimbo


Tume iliweka utaratibu ambao Wadau walitumia kutoa na kuwasilisha Tume Maombi/Mapendekezo ya kuchunguza Mipaka na kugawa Majimbo. Utaratibu ulioelekezwa ni huu ufuatao :-

  1. Maombi/mapendekezo ya kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo kuwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na kujadiliwa katika vikao rasmi vya Halmashauri husika.

  2. Mkurugenzi wa Halmashauri husika kuwasilisha maombi/mapendekezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa.

  3. Katibu Tawala wa Mkoa kuwasilisha maombi/mapendekezo hayo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ili kupata maoni zaidi.

  4. Katibu Tawala wa Mkoa kuwasilisha maoni/mapendekezo kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  5. Tume kuchambua maombi na kufanya maamuzi, kisha kuomba kibali cha kugawa Majimbo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba.

Mwisho wa kupokea maombi ilikuwa tarehe 28 Februari, 2010. Halmashauri arobaini na saba (47) ziliwasilisha jumla ya maombi hamsini na tatu (53). Maombi hayo yalihusisha: kugawa Majimbo maombi arobaini na saba (47), kubadili majina ya Majimbo maombi manne (4) na kurekebisha mipaka ya Majimbo maombi mawili (2). Miongoni mwa maombi arobaini na saba (47) ya kugawa Majimbo, maombi arobaini na mbili (42) yalikidhi vigezo na maombi matano (5) hayakukidhi vigezo. Aidha, maombi manne (4) ya kubadili majina yalikubaliwa na maombi mawili (2) ya kurekebisha mipaka yalikataliwa; kama inayooneshwa kwenye Kiambatisho B.


      1. Mgawanyo wa Majimbo ya Uchaguzi


Baada ya kupokea na kuchambua maombi Tume ilibaini kuwa ni Majimbo arobaini na mbili (42) ndiyo yaliyokidhi Vigezo kwa ajili ya kufikiriwa kugawanywa. Kati ya Majimbo hayo therathini na tatu (33) yalikuwa Majimbo ya Vijijini na tisa (9) yalikuwa Majimbo ya Mijini.
Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilizingatia, pamoja na mambo mengine, taarifa zifuatazo katika kugawa Majimbo ya Uchaguzi:

  1. Uwezo wa Ukumbi wa Bunge kuhusu idadi ya Wabunge wanaoweza kukaa ambayo ni 360, kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  2. Serikali kuongeza idadi ya Wabunge wa Viti Maalum vya Wanawake kutoka 30% hadi 40% ya Wabunge wote.

  3. Makubaliano yaliyofikiwa katika mikutano kati ya Tume na Wadau wa maeneo yaliyokusudiwa kugawanywa.

  4. Kibali cha Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara ya 75(1) ya Katiba ya Nchi.

Kutokana na hayo Tume iliamua kugawa majimbo saba (7) tu. Kati ya Majimbo hayo Majimbo sita (6) yalikuwa kutoka Halmashauri za Wilaya na Jimbo moja (1) lilikuwa la Halmashauri ya Manispaa. Majimbo yaliyogawanywa ni yale tu ambayo kwa mujibu wa Vigezo yalipata alama nyingi kuliko Majimbo mengine. Hivyo, Majimbo yaliyoshika nafasi ya kwanza mpaka ya sita (6) kwa upande wa Majimbo ya Vijijini ndiyo yaligawanywa. Jimbo lililoshika nafasi ya kwanza kwa upande wa Majimbo ya Mjini ndilo liligawanywa. Majimbo hayo ni Nkasi, Tunduru, Maswa, Kasulu Mashariki, Bukombe na Singida Kusini kutoka Halmashauri za Wilaya. Jimbo la Ukonga kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ndilo lililogawanywa. Mgawanyo ulikuwa kama unavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.




Jedwali Na. 1: Majimbo yaliyogawanywa Mwaka 2010



Na.

Halmashauri

Jimbo Lililogawanywa

Majimbo Mapya

1

Nkasi

Nkasi

  1. Nkasi Kaskazini

  1. Nkasi Kusini

2

Tunduru

Tunduru

3. Tunduru Kaskazini

4. Tunduru Kusini

3

Maswa

Maswa

5. Maswa Mashariki

6. Maswa Magharibi

4

Kasulu

Kasulu Mashariki

7. Kasulu Vijijini

8. Kasulu Mjini

5

Bukombe

Bukombe

9. Bukombe

10. Mbogwe

6

Singida

Singida Kusini

11.Singida Magharibi

12. Singida Mashariki

7

Ilala

Ukonga

13. Ukonga

14. Segerea

Kwa hiyo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iligawanywa katika Majimbo 239 badala ya 232 ya awali. Tume ilitangaza Majimbo yote kwenye Gazeti la Serikali Na. 271 la tarehe 30 Julai, 2010.


      1. Majimbo yaliyobadilishwa Majina


Baadhi ya Majimbo yalibadilishwa majina kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.
Jedwali Na. 2: Orodha ya Majimbo yaliyobadilishwa Majina Mwaka 2010


Na.

Mkoa

Halmashauri

Jina la Awali

Jina Jipya

1.


Rukwa


Mji wa Mpanda

Mpanda Kati

Mpanda Mjini

Wilaya ya Mpanda



Mpanda Mashariki

Katavi

Mpanda Magharibi

Mpanda Vijijini

2.

Kagera

Wilaya ya Chato

Biharamulo Mashariki

Chato







Wilaya ya Biharamulo

Biharamulo Magharibi

Biharamulo

Jimbo la Biharamulo Magharibi lilibadilishwa jina baada ya Jimbo la Biharamulo Mashariki kuomba na kukubaliwa kubadili jina na kuwa Chato.



1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət