Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə10/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   6   7   8   9   10   11   12   13   ...   33

Mikutano, Warsha, Semina, Mafunzo na Kamati za Tume


Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Uchaguzi, ilifanya Mikutano na Wadau wa Uchaguzi, Warsha kwa Watumishi wake, Semina na Mafunzo kwa Watendaji Mbalimbali.
      1. Mikutano na Wadau wa Uchaguzi


Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kutambua mchango na umuhimu wa Wadau wa Uchaguzi na nafasi waliyo nayo katika kuboresha na kufanikisha Uchaguzi na kukuza Demokrasia na kuimarisha Utawala Bora, imekuwa na utaratibu wa kuwashirikisha Wadau mbalimbali kwa nyakati tofauti katika hatua za mchakato wa Uchaguzi.
Tume ilitumia njia mbalimbali za kuwashirikisha, kushauriana na kupata maoni ya Wadau katika hatua mbalimbali za Uchaguzi kwa njia ya kufanya nao mikutano na warsha za kuwaelimisha kuhusu Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi pamoja na nafasi yao katika mchakato wa Uchaguzi. Wadau wa Uchaguzi pia walipewa taarifa mbalimbali zilizohusu maendeleo ya Maandalizi ya Uchaguzi, Mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi, Ugawaji wa Majimbo ya Uchaguzi, Maadili ya Uchaguzi, Uteuzi wa Wagombea, Kampeni za Uchaguzi, Maandalizi na usambazaji wa vifaa na Elimu ya Mpiga Kura.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya mikutano kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ili kupata maoni ya Wadau yatakayoboresha utekelezaji wa majukumu yake.
      1. Warsha kwa Watumishi


Tume iliendesha Warsha ya kuandaa Maelekezo kwa Maafisa Waandikishaji, Wasimamizi wa Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Wagombea, Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura, Makarani Waongozaji, Waandishi Wasaidizi na Wapiga Picha.
Vile vile iliendesha Warsha kwa Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo yote tarehe 13 Julai, 2010 na 07 Oktoba, 2010 Dar es Salaam.
      1. Semina na Mafunzo


Kabla ya utekelezaji wa zoezi la Uchaguzi kulikuwa na utoaji wa Mafunzo kwa Watendaji ambayo yalifanyika kama ifuatavyo:-
(a) Wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Watendaji katika kila Kanda walipewa Semina/Mafunzo yaliyohusu usimamizi wa Uboreshaji wa Daftari, Ugawaji na Usambazaji wa Vifaa, Ufuatiliaji katika Vituo, Utumiaji wa Kamera za kupigia picha Wapiga Kura na Vifaa vyake, Ujazaji wa Fomu mbalimbali na Urejeshaji wa Taarifa za waliojiandikisha/waliojioboresha taarifa zao Makao Makuu ya Tume, Dar es Salaam.


(b) Wakati wa Uchaguzi

Watendaji wa kila kanda walipewa Semina/Mafunzo juu ya hatua mbalimbali za Uchaguzi katika mada zilizohusu Maelekezo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, Maelekezo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea, Maelekezo kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura, na Maelekezo kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura.


      1. Kamati za Tume


Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ili kushirikisha Wadau katika kazi zake, ilihuisha Kamati nane (8) za Ushauri. Kamati hizi zilikuwa zikikutana na kujadili mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijitokeza kwa lengo la kuisaidia Tume kufanikisha Uchaguzi Mkuu. Kamati hizo ni:-

  1. Mamlaka na Taratibu za Uendeshaji Uchaguzi.

  2. Elimu ya Mpiga Kura na Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

  3. Upatikanaji na Ugawaji wa Vifaa.

  4. Mahusiano ya Serikali na Vyama vya Siasa.

  5. Habari na Mawasiliano.

  6. Watazamaji wa Uchaguzi na Mashirika ya Kimataifa.

  7. Maadili ya Uchaguzi.

  8. Uratibu.
    1. Elimu ya Mpiga Kura


Kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kinaipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jukumu la kutoa, Kusimamia na Kuratibu Watu au Taasisi zinazotoa Elimu ya Mpiga Kura kwa nchi nzima. Kwa ajili hiyo Tume iliandaa Mwongozo wa Uendeshaji wa Elimu ya Mpiga Kura na kuzipatia Taasisi zilizohusika.
Tume ilipitia, kuhariri na kuidhinisha zana za Elimu ya Mpiga Kura na pia kutoa Kibali kwa watu au Taasisi zinazojihusisha na kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchini. Tume iliweza kutekeleza jukumu hilo kutokana na upatikanaji wa fedha kutoka Serikalini na Washirika wa Maendeleo kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) chini ya Mradi wa Kusaidia Uchaguzi (ESP).
      1. Elimu ya Mpiga Kura Wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Wakati wa Uchaguzi Mkuu


Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulifanyika kwa awamu mbili. Katika awamu zote, Elimu ya Mpiga Kura ilitolewa kwa kutumia mbinu na nyenzo mbalimbali hususan mabango, vipeperushi, machapisho/vijitabu, michezo ya kuigiza, vyombo vya habari, vikundi vya sanaa, mtandao wa kompyuta, matangazo yaliyotolewa katika nyumba za ibada na magari yenye vipaza sauti. Vyote hivi vikiwa na ujumbe mbalimbali kwa ajili ya Uboreshaji na Uhamasishaji wa wananchi kwenda kujiandikisha/kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Asasi za Kiraia zilizopewa ufadhili na UNDP kupitia Mradi wa Kusaidia Uchaguzi (ESP), zilitoa Elimu ya Mpiga Kura katika kipindi cha Uchaguzi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya ufuatiliaji katika maeneo ambayo Asasi hizo zilipanga kutoa Elimu ya Mpiga Kura, kama kinavyoonesha kiambatisho C.
Tume kwa kushirikiana na UNDP ilianzisha Chombo cha Ushauri kuhusu Elimu ya Mpiga Kura (Voter Education Reference Group) ambacho kilikuwa na Wajumbe ishirini na sita (26). Wajumbe wa Kundi hili walikuwa wakikutana kila mwezi kupeana taarifa, kutoa maoni na ushauri wao juu ya hali ya Utoaji Elimu ya Mpiga Kura nchini. Matangazo na Machapisho mbalimbali yalipitiwa na ushauri ulitolewa kuhusu mbinu ambazo zingeweza kutumiwa ili kuwafikia wananchi wengi zaidi hususan maeneo ya Vijijini.
Tume ilianzisha Kituo cha Mawasiliano ya Simu (Call Centre) ili kutoa fursa kwa Wapiga Kura kuuliza maswali yaliyohusu Uchaguzi na majibu yalitolewa papo hapo. Miongoni mwa Maswali yaliyoulizwa na kujibiwa mara kwa mara yalikuwa ni juu ya:-

  1. Kutokuwepo kwa majina ya Wapiga Kura kwenye Daftari

  2. Waliopoteza kadi zao za kupigia kura kutaka kuruhusiwa kupiga kura

  3. Wanafunzi wa Vyuo kutaka kuruhusiwa kupiga kura kwenye vituo vingine kwa kuwa Vyuo vilichelewa kufunguliwa

  4. Namba za Wapiga Kura kwenye Daftari kutofautiana na kadi za kupigia kura

  5. Vituo vya kupigia kura kuwa mbali na makazi ya Wapiga Kura

  6. Kuchelewa kutolewa Matokeo ya Uchaguzi kwa baadhi ya majimbo

Taarifa na Ujumbe mbalimbali wa Uchaguzi viliwekwa kwenye Tovuti (Website) ya Tume ambapo wananchi waliweza kupata taarifa mbalimbali za Uchaguzi Mkuu na namna ya kushiriki kikamilifu.


1   ...   6   7   8   9   10   11   12   13   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət