Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə18/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   14   15   16   17   18   19   20   21   ...   33

Changamoto Zilizojitokeza


  1. Katika baadhi ya Majimbo ya Uchaguzi uamuzi wa Watendaji wa Uchaguzi kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi yalichangia kujenga mitazamo ya kutoamini Watendaji wa Uchaguzi. Hata hivyo Tume ilitoa ufafanuzi mara kwa mara juu ya masuala mbalimbali ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.

  2. Baadhi ya Wagombea wa Vyama mbalimbali vya Siasa kujitoa kuwa Wagombea na baadaye tena kuomba kurejea kuwa Wagombea, jambo ambalo kisheria halikukubalika.

  3. Matukio machache ya fujo katika baadhi ya maeneo ambayo yalihusisha mashabiki wa Vyama vya Siasa, kiasi cha kusababisha uvunjifu wa amani.

  4. Baadhi ya Wagombea kujitoa katika nyakati tofauti baada ya uteuzi, kulisababisha usumbufu kwa Tume katika maandalizi ya Karatasi za Kura.

  5. Wagombea na Wasimamizi wa Uchaguzi kuchelewa kupata Mfano wa Karatasi za Kura ambazo zilihitajika kwa madhumuni mbalimbali.

  6. Baadhi ya Wadhamini wa Wagombea kuamua kujitoa kumdhamini Mgombea baada ya Mgombea kuteuliwa.

  7. Baadhi ya Vyama vya Siasa na Wagombea kukiuka Ratiba za Kampeni na hata kuingilia mikutano ya Vyama vingine.

  8. Baadhi ya Vyama vya Siasa kutozingatia muda wa kumaliza mikutano ya Kampeni yaani saa 12.00 jioni.

  9. Baadhi ya wafuasi na mashabiki wa Vyama vya Siasa kuwa na jazba kupita kiasi na kuchana bendera na Mabango ya Vyama vingine.

  10. Baadhi ya Wagombea kutumia lugha za Kienyeji badala ya Kiswahili kinyume na Maadili ya Uchaguzi.

  11. Baadhi ya Vyama vya Siasa kutumia mabango ambayo hayakuidhinishwa na Tume.

  12. Baadhi ya Vyombo vya Habari kutotoa taarifa sahihi na zisizoegemea upande wowote na hivyo kukiuka Maadili ya Vyombo vya Habari kuhusu utoaji wa habari kwa kuzingatia haki.

  13. Kujitokeza kwa msukumo wa kutoka kwa baadhi ya Vyama vya Siasa na Wagombea wa kubadilisha Ratiba za Kampeni kila mara na matokeo yake kusababisha taarifa husika za mabadiliko hayo kutofika kwa wakati kwa Watendaji wa Uchaguzi na Jeshi la Polisi na kusababisha usumbufu usio wa lazima.

  14. Baadhi ya Vyama vya Siasa hususan vilivyokuwa na Wagombea Urais, kufanya mikutano yake pasipo kufanya utaratibu mzuri wa makubaliano na mamlaka husika hususan Wamiliki wa Viwanja vya kufanyia mikutano na badala yake kutumia njia zisizokubalika kufanya mikutano na kusababisha usumbufu.

  15. Vyama vya Siasa kutofautiana sana kiuwezo na kifedha.

  16. Baadhi ya Wagombea kughushi taarifa na saini za waliowadhamini.

  17. Baadhi ya Vyama vya Siasa kutoa lugha ya vitisho kwa Wapiga Kura.


SURA YA TANO




UPIGAJI KURA NA UHESABUJI WA KURA VITUONI




    1. Maandalizi ya Siku ya Uchaguzi


Tarehe 31 Oktoba, 2010 ilikuwa ni Siku ya Uchaguzi ambayo ndiyo Siku ya Kupiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara ambazo husimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Pia, tarehe hiyo ilikuwa ni Siku ya Uchaguzi wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wa Zanzibar, Chaguzi ambazo husimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Siku ya Uchaguzi ilitanguliwa na maandalizi kadhaa muhimu ya jumla yaliyokuwa yakifanywa kuanzia ngazi ya Tume, Mikoa, Halmashauri/Wilaya hadi ngazi ya Kata. Maandalizi hayo ni pamoja na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Upatikanaji na Usambazaji wa vifaa vya Uchaguzi, Uteuzi na mafunzo kwa Watendaji mbalimbali wa Uchaguzi, Uteuzi wa Wagombea, Kampeni za Uchaguzi na maandalizi ya vituo vya Kupigia Kura.
    1. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Baada ya kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika Vituo vya Kujiandikisha/Kuboresha Taarifa za Wapiga Kura, Tume huandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura ambalo huwekwa wazi kwa ajili ya kukaguliwa ili kuhakiki iwapo taarifa za Wapiga Kura zimerekodiwa kwa usahihi. Hatimaye, Tume huandaa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kila Kituo cha Kupigia Kura kwa ajili ya kutumika Siku ya Uchaguzi.
    1. Uchapishaji wa Karatasi za Kura


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza Zabuni ya Wazi ya Kimataifa ili kumpata Mchapishaji wa Karatasi za Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, Bunge na Madiwani.
Baada ya kupokea, kuchambua na kufanya tathimini ya Wachapishaji wa Karatasi za kura waliojitokeza, Tume ilitoa Zabuni ya Kuchapisha karatasi za Kura kwa Kampuni ya Kalamazoo Secure Solution ya Uingereza.
    1. Usafirishaji wa Vifaa vya Siku ya Uchaguzi kwenda Majimboni


Tume ilianza kupeleka Majimboni vifaa vya Siku ya Uchaguzi tarehe 15 Agosti, 2010 na kukamilisha siku moja kabla ya Uchaguzi kwa baadhi ya Majimbo. Wasimamizi wa Uchaguzi waligawa vifaa vya Kupigia Kura kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura na kuvisambaza baada ya kukamilisha mafunzo kwa Watendaji hao.
    1. Uteuzi na Mafunzo kwa Watendaji


Wasimamizi wa Uchaguzi katika ngazi ya Halmashauri na Wilaya walifanya Uteuzi wa Wasimamizi wa Vituo na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo kwa kufuata Sheria za Uchaguzi na Maelekezo yaliyotolewa na Tume. Vyama vya Siasa vilishirikishwa katika mchakato wa Uteuzi wa Watendaji wa Vituo vya Kupigia Kura kwa kutoa maoni yao kabla ya Uteuzi rasmi kufanyika. Watendaji hao walipatiwa mafunzo ya siku mbili ambayo yalihusu majukumu na wajibu wa Watendaji hao, taratibu za Upigaji Kura na Kuhesabu Kura vituoni.
Aidha, Wasimamizi wa Uchaguzi waliteua Makarani Waongozaji wa Wapiga Kura na kuwapa mafunzo ya siku moja kuhusu wajibu na utaratibu wa kazi zao.
Kwa Mkoa wa Dar es Salaam Makarani Waongozaji wa Wapiga Kura waliopangiwa vituo vyenye idadi kubwa ya Wapiga Kura walipatiwa mafunzo kwa siku moja nyingine kuhusu namna ya kutumia mashine ya kuwezesha kutambua Mpiga Kura na Kituo alichopangiwa Kupiga Kura (Zip-Zip Machines).
1   ...   14   15   16   17   18   19   20   21   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət