Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə17/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   13   14   15   16   17   18   19   20   ...   33

Kampeni za Uchaguzi


Kampeni za Uchaguzi huwezesha Vyama vya Siasa na Wagombea kuwafikia Wapiga Kura na Wananchi kwa ujumla kwa njia ya Mikutano ya Hadhara na Nyumba kwa Nyumba.
      1. Taratibu za Kampeni


Kwa mujibu wa taratibu za Kampeni, Vyama vya Siasa ambavyo vinashiriki katika Uchaguzi hupaswa kuwasilisha Ratiba zao za Kampeni kwa mamlaka husika ambayo huratibu Ratiba hizo kabla ya siku ya Kampeni kuanza. Aidha, kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi na Kanuni za Uchaguzi; mabango na machapisho mbalimbali wanayotumia Wagombea Uchaguzi na Vyama vya Siasa, hutakiwa kuidhinishwa na mamlaka za Uteuzi kwa Uchaguzi husika.
      1. Kipindi cha Kampeni


Kampeni za Uchaguzi zilifanyika kuanzia tarehe 20 Agosti, 2010 hadi tarehe 30 Oktoba, 2010.
      1. Masharti ya Kampeni


Vyama vya Siasa na Wagombea sharti wazingatie Ratiba iliyoratibiwa na Mamlaka za Uchaguzi, muda wa kufanya Kampeni na Maadili ya Uchaguzi. Vyama vya Siasa na Wagombea wanatakiwa kupata kibali cha mmiliki wa Kiwanja au eneo watakalofanyia Kampeni na kukubaliana na wamiliki wa nyumba zinazobandikwa mabango ya Kampeni.
      1. Uratibu wa Kampeni za Urais


Ratiba za Kampeni za Uchaguzi wa Rais ziliratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Vyama vya Siasa baada ya kuwasilisha mapendekezo ya Ratiba zao, Mkurugenzi wa Uchaguzi aliitisha Mkutano na Vyama husika na kukubaliana Ratiba moja, ambayo ilitumwa kwa Wakuu wa Mikoa, Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini. Aidha, Ratiba hiyo ilipelekwa kwa Vyombo vya Habari ili kutangazwa.
Katika hatua mbalimbali za mchakato wa Kampeni, mabadiliko ya Ratiba ya Kampeni yalifanyika kutokana na maombi ya Vyama vya Siasa, ambapo Tume ilikutana na Vyama vyote vya Siasa vilivyoshiriki Uchaguzi kwa madhumuni hayo. Baada ya mabadiliko hayo Ratiba mpya ya Kampeni iliandaliwa na Nakala zilisambazwa kwa wadau wote waliohusika.
      1. Vikao vya Kupokea na Kujadili Maombi ya Kurekebisha Ratiba


Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea na kujadili maombi ya kurekebisha Ratiba ya Kampeni kutoka Vyama vya Siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi wa Rais katika mikutano iliyojumuisha Wawakilishi wa Vyama vyote vilivyokuwa na Wagombea.
Kwa upande wa Uchaguzi wa Bunge na Madiwani, Wasimamizi wa Uchaguzi/Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi walifanya mikutano ya kujadili na kurekebisha Ratiba kila ilipolazimu baada ya kupokea maombi ya Chama cha Siasa.
      1. Vyama vya Siasa na Wagombea Urais


Vyama vya Siasa na Wagombea Urais walipatiwa fursa ya kutumia Vyombo vya Habari vya umma kunadi Sera zao, kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Maelekezo ya Tume.
Vyama vya Siasa vilipewa vipindi ambavyo kila Chama kilipewa fursa ya kuvitumia kutangaza Sera zake kupitia Vyombo vya Habari vya Umma. Vipindi vilivyorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) vilikuwa kama inavyooneshwa katika jedwali Na.21.

Jedwali Na. 21: Ratiba ya Vipindi vya Matangazo Vilivyotengwa na Vyombo vya Umma kwa Ajili ya Vyama vya Siasa


Na.

Aina ya Kipindi

Idadi ya Vipindi

Muda

Muda Uliotumika

Siku

1

Matangazo ya UNDP

10

“Prime Time”

Saa 1

Kila Jumanne na Jumamosi

2

Vipindi vya Kapu la Uchaguzi

15

3.00 - 3.30 Usiku

Dakika 30

Kila Jumatatu

3

Vipindi vya Vijana

4

10.00 -11.00 Jioni

Saa 1

Kila Jumapili

4

Wasifu wa Viongozi

5

3.30 - 4.00 Usiku

Dakika 30

Kila Alhamisi

5

Tuambie Maalum

10

3.10 - 4.40 Usiku

Saa 1.30

Kila Alhamisi

6

Mchakato Majimboni

19

3.00 - 4.00 Usiku

Saa 1

Kila Jumanne

na Jumamosi



7

Acha Waseme

9

7.00-8.00 Mchana

Saa 1

Kila Jumamosi

Matangazo haya yalirushwa kwa miezi miwili na nusu kabla ya Siku ya Upigaji Kura, Oktoba 31, 2010. Aidha, Tume haikupokea malalamiko yoyote kutoka kwa Chama cha Siasa kuhusu kunyimwa fursa ya kunadi Sera zake.


      1. Uratibu wa Kampeni za Ubunge na Udiwani


Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa ngazi ya Kata kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi na Maelekezo ya Tume wanaratibu Kampeni kwa Uchaguzi wa Ubunge na Udiwani. Watendaji hawa walifanya mikutano na Vyama vya Siasa husika vilivyowasilisha Ratiba zao za mikutano ya kampeni kabla ya Siku ya Uteuzi. Baada ya makubaliano juu ya Ratiba husika, nakala ya Ratiba iliyoratibiwa ilipelekwa kwa Wakuu wa Wilaya husika na Makamanda wa Polisi wa Wilaya.
      1. Usimamizi na Utekelezaji wa Maadili ya Uchaguzi na Kamati za Maadili Ngazi Zote


Maadili ya Uchaguzi ni Makubaliano ya Wadau wakuu watatu wa Uchaguzi ambao ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Serikali yanayohusu taratibu za mambo ya kufanya na yasiyopaswa kufanywa na wadau hawa katika hatua mbalimbali za Uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kunakuwepo Uchaguzi huru, wa haki na unaokubalika.
Kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria yaliyofanywa katika Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, chini ya kifungu cha 124A, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kuandaa Maadili ya Uchaguzi baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa na Serikali.
Katika kuhakikisha Usimamizi na Utekelezaji wa Maadili hayo Sehemu ya V ya Maadili ya Uchaguzi inatoa mwongozo wa kuwepo Kamati za Maadili katika ngazi mbalimbali. Kamati ya Rufaa, Kamati ya Kitaifa, Kamati ya Jimbo na Kamati ya Kata. Kamati hizi zilijumuisha wawakilishi wa Vyama vya Siasa na Watendaji wa Serikali.

Kwa mujibu wa taratibu zilizoelekezwa, malalamiko yote yalipaswa kuwasilishwa kwenye Kamati za Maadili ya Uchaguzi katika ngazi husika ndani ya saa arobaini na nane (48) tangu kutokea kwa tukio linalolalamikiwa. Kamati husika ilimtaka aliyelalamikiwa kuwasilisha utetezi wake kwa maandishi ndani ya saa arobaini na nane (48) tangu kupokea malalamiko. Uamuzi uliotolewa katika kikao ulipaswa kutekelezwa na pande husika, na pale mhusika aliposhindwa kutekeleza uamuzi wa Kamati kulikuwa na adhabu mbalimbali yaani karipio la maandishi, kutozwa faini au kusimamishwa kufanya Kampeni.


(a) Malalamiko yalivyoshughulikiwa na Kamati za Maadili

          1. Kamati ya Maadili ya Kitaifa ilipokea malalamiko tisa (9) na kuyashughulikia.

          2. Kamati ya Rufaa ilipokea Rufaa moja (1) na kuishughulikia.

          3. Kamati za Majimbo na Kata nazo zilipokea malalamiko mbalimbali na kuyashughulikia kwa mujibu wa Maadili ya Uchaguzi.


(b) Maamuzi Kuhusu Malalamiko

Malalamiko mengi yaliyowasilishwa katika Kamati za Maadili yalihusu ukiukwaji wa Ratiba za Kampeni, baadhi ya Vyama vya Siasa kuingilia mikutano ya Kampeni ya Vyama vingine, lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya Vyama, baadhi ya Vyama kutozingatia muda wa Kampeni na baadhi ya Vyama kuchoma bendera na mabango ya Chama kingine.


Adhabu zilizotolewa na Kamati za Maadili ni onyo, karipio, faini na kusimamishwa kufanya Kampeni.
      1. Hali Iliyokuwepo Wakati wa Uendeshaji Kampeni


Kwa ujumla Kampeni za uchaguzi zilifanyika katika hali ya amani, usalama na zilizingatia Sheria, Kanuni na taratibu. Hata hivyo, kulikuwa na matukio machache ya fujo, kuingilia Kampeni za Vyama vingine, vurugu zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo na kwa upande wa Wilaya ya Maswa kusababisha kifo.
Vyombo vya Habari vilifanya kazi nzuri ya kuufahamisha umma juu ya Sera mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na vyama vya siasa na Wagombea mbalimbali.
Hali ya kujitokeza kwa wingi kwa watu katika mikutano ya Kampeni kwa ajili ya kuwasikiliza Wagombea ilikuwa ni sehemu muhimu sana ya mafanikio katika mchakato wa Uchaguzi.
1   ...   13   14   15   16   17   18   19   20   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət