Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə25/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   21   22   23   24   25   26   27   28   ...   33

Changamoto Zilizojitokeza


  1. Watazamaji wa Kimataifa kuchelewa kupata mwaliko wa kushiriki.

  2. Baadhi ya Watazamaji wa Ndani kutopata taarifa ya Tume kwamba haitawagharamia Watazamaji wa Uchaguzi.

  3. Baadhi ya Watazamaji kuchelewa kutoa taarifa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


SURA YA TISA

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

HITIMISHO


Taarifa ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ambao ni Uchaguzi Mkuu wa nne kufanyika chini ya Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa, imeelezea kwa undani juu ya Maandalizi na utekelezaji wa hatua mbalimbali katika mchakato mzima wa Uchaguzi. Hatua hizo ni pamoja na: Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Ugawaji wa Majimbo, Uteuzi wa Wagombea, Kampeni za Uchaguzi, Upigaji Kura, Kuhesabu Kura, Kujumlisha Kura na Kutangaza Matokeo.
Kwa ujumla Tume imeridhika na mafanikio yaliyopatikana katika Uendeshaji na Usimamizi wa Uchaguzi katika Chaguzi zote kwa ngazi zote. Mafanikio hayo yametokana pamoja na mambo mengine, ushirikiano ambao Tume ilipata toka kwa Wadau wote wa Uchaguzi, ikiwa ni pamoja na Serikali, Vyama vya Siasa, Washirika wa Maendeleo, Wapiga Kura, Asasi za Kiraia, Vyombo vya Habari, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Viongozi wa Dini na Wananchi kwa ujumla. Vile vile utendaji mzuri, kujituma na uadilifu uliooneshwa na Watendaji wa Tume katika ngazi zote umechangia sana mafanikio hayo.
Baada ya kuanzishwa na kutumika kwa mara ya kwanza Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2005, kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2010, taratibu za kuboresha zilifanyika katika Awamu Mbili. Aidha, kumefanyika marekebisho ya Sheria za Uchaguzi yaliyoelekeza Tume kufanya Uboreshaji wa Daftari mara mbili katika kipindi cha tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mmoja na kabla ya kufanyika Uchaguzi mmoja Mkuu mwingine.
Kufuatia mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi, Maadili ya Uchaguzi yalipewa nguvu ya kisheria. Tume ilipitia upya Maadili ya Uchaguzi yaliyokuwepo kwa kushauriana na Vyama vya Siasa na Serikali, na ndipo pande zote husika zikasaini Maadili hayo. Ni dhahiri kuwa hatua kubwa imefikiwa, ingawa maboresho yanahitajika hususan katika usimamizi na utekelezaji wa Maadili hayo.
Tume imeridhika na ushiriki wa Wadau mbalimbali na Wananchi kwa ujumla na kama ilivyojidhihirisha katika Kampeni za Uchaguzi katika maeneo mbalimbali watu wengi walijitokeza kuhudhuria mikutano ya Kampeni. Kampeni ziliendeshwa kwa kuzingatia taratibu ingawa katika baadhi ya maeneo kulikuwepo ukiukwaji wa taratibu na hata matukio ya fujo. Tume inasikitishwa na tukio la kuuawa kwa mtu mmoja katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambalo lilihusishwa na shughuli za kisiasa wakati Kampeni za Uchaguzi.
Kuanzishwa kwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 ambayo iligusa maeneo kadhaa ya Sheria za Uchaguzi ilileta changamoto kadhaa katika mchakato wa uchaguzi, jambo ambalo, Tume ina maoni kuwa yamkini Sheria yenyewe na chombo cha usimamizi wa Sheria hii viangaliwe upya ili kuleta ufanisi na kufikiwa kwa malengo ya kuwepo kwa Sheria hii.
Tume inaona kuwa yapo matatizo kadhaa yaliyojitokeza katika hatua mbalimbali za mchakato wa Uchaguzi ambayo yalichangia kupunguza ufanisi wa uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Uchaguzi, ikiwa ni pamoja na:-

  1. Ufinyu wa Bajeti ya Uchaguzi;

  2. Mabadiliko ya mipaka ya kiutawala hususan ongezeko la Kata katika kipindi kifupi kabla ya Uchaguzi;

  3. Kujitokeza kwa idadi ndogo ya Wapiga Kura Siku ya Uchaguzi;

  4. Baadhi ya Wagombea/Vyama vya Siasa kutozingatia Ratiba za Kampeni na Maadili ya Uchaguzi; na

  5. Baadhi ya Watendaji wa Vituo kutozingatia kikamilifu mafunzo na matokeo yake kutotekeleza ipasavyo majukumu yao katika ngazi ya Vituo.

Kwa ujumla, Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na changamoto zilizojitokeza, inaridhika kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika mwaka 2010 ulifanyika katika hali ya uwazi, huru na haki na hivyo kufanya Uchaguzi kuwa wa kuaminika. Ushiriki wa wananchi katika Uchaguzi ni dhahiri kuwa walipewa nafasi ya kuchagua viongozi wao waliowataka. Matokeo ya Uchaguzi kama yalivyojitokeza yamedhihirisha Sauti ya Wapiga Kura.


Baada ya Uchaguzi kwa kawaida Wagombea hususan walioshindwa hufungua Malalamiko ya Uchaguzi Mahakama Kuu kwa Uchaguzi wa Bunge na Mahakama za Mahakimu Wakazi kwa Uchaguzi wa Madiwani. Hadi sasa yamefunguliwa Malalamiko 44 ya Wabunge ambayo yanaendelea kusikilizwa. Malalamiko ya Uchaguzi ya Wabunge yanakadiriwa kuigharimu Tume kiasi cha Sh. Bilioni 1.2, kwa ajili ya kugharamia mashahidi na ufuatiliaji wa Malalamiko hayo.
Jedwali Na. 30: Idadi ya Malalamiko Yaliyofunguliwa Mahakama Kuu kila Kanda


Na.

Mahakama Kuu - Kanda

Idadi ya Malalamiko

1

Tabora

10

2

Dar es Salaam

7

3

Mwanza

7

4

Mtwara

5

5

Mbeya

4

6

Moshi

3

7

Iringa

2

8

Dodoma

2

9

Arusha

2

10

Bukoba

1

11

Rukwa

1




Jumla

44

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawashukuru Watendaji wote wa hatua mbalimbali kuanzia ngazi ya Taifa hadi Kituo kwa kufanikisha Uchaguzi. Pia inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; Wadau Mbalimbali vikiwemo Vyama vya Siasa na Wagombea; Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP); Washirika wa Maendeleo wote hasa walioko chini ya Basket Group, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC); Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ); Jeshi la Polisi Tanzania na Vyombo vingine vya Usalama; na Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini. Tume pia inavishukuru Vyombo vya Habari, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Watazamaji wa Uchaguzi, Wapiga Kura na Watanzania wote kwa ujumla walioshiriki kwa namna moja au nyingine kuiwezesha Tume kukamilisha Uchaguzi wa mwaka 2010 kwa mafanikio.



1   ...   21   22   23   24   25   26   27   28   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət