MAPENDEKEZO
Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa mwaka 2005, Tume iliandaa Taarifa yake na kuiwasilisha Serikalini. Katika Taarifa hiyo Tume ilitoa mapendekezo kadhaa ya jinsi ya kuboresha chaguzi zitakazofuata. Tume inaishukuru Serikali kwa kutekeleza baadhi ya mapendekezo, hata hivyo kutokana na mapendekezo mengine kutotekelezwa Tume inapenda kuikumbusha Serikali mapendekezo yake ya awali na kuongeza mapendekezo mapya kama ifuatavyo:-
A. MAPENDEKEZO YA MWAKA 2005 AMBAYO HAYAJATEKELEZWA
(i) Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyoanza kufanyiwa kazi na Serikali ikamilishwe mapema.
(ii) Bajeti ya Uchaguzi Kila Mwaka
Kwa kuwa Uchaguzi Mkuu unafanyika kila baada ya miaka mitano na Sheria inaitaka Tume kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Chaguzi Kuu mbili, ni vema kuwepo na mfuko wa Kudumu wa Uchaguzi ambao utakuwa unatengewa fedha kutoka Bajeti ya Serikali ya kila mwaka. Hii itaepusha kuathiri utendaji wa Wizara na Taasisi za Serikali inapofikia mwaka wa Uchaguzi. Aidha, itaiwezesha Serikali kuzidi kujitegemea kifedha katika kuendesha chaguzi nchini.
(iii) Ukomo wa Mgombea Kujitoa
Kutokana na Wagombea wengi kuendelea kujitoa baada ya Uteuzi, Tume ilipendekeza Sheria irekebishwe ili kuweka ukomo wa Mgombea kujitoa na kuwepo na ada ya kulipa endapo Mgombea atajitoa baada ya ukomo uliowekwa kupita. Jambo hili litasaidia Wapiga Kura kutopoteza Kura zao kwa kumpigia Mgombea aliyejitoa ambaye jina lake linaendelea kuwepo kwenye Karatasi ya Kura.
(iv) Sheria Kuhusu Kampeni
Sheria ya Uchaguzi kuhusiana na Kampeni za Uchaguzi iangaliwe upya na kuhakikisha haikinzani na sheria zingine, kwa mfano Police Force Ordinance Act, Sura ya 322 na Sheria ya Nembo ya Taifa ya mwaka 1971 Sura ya 10.
(v) Tume Kuwa na Ofisi ya Uchaguzi Katika Halmashauri
Ili uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uweze kufanikiwa na shughuli nyingine za Uchaguzi kuendeshwa kwa ufanisi zaidi ilipendekezwa kuwa na Ofisi za Uchaguzi katika kila Halmashauri.
(vi) Jengo la Kudumu la Ofisi ya Tume
Tume hadi sasa haina Jengo la Kudumu la Ofisi linalokidhi mahitaji yakiwemo ya utunzaji wa vifaa na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Tume ilipendekeza ipatiwe fedha za kujenga Jengo la Kudumu la Ofisi litakalokidhi mahitaji yake.
(vii) Tume Kuwa na Ofisi Ndogo Tanzania Zanzibar
Ilipendekezwa kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe na Ofisi ndogo Tanzania Zanzibar ili kuboresha uendeshaji wa chaguzi za Muungano.
(viii) Elimu ya Mpiga Kura
Tume ilipendekeza kuwa ili Elimu ya Mpiga Kura iweze kutolewa kwa ukamilifu kwa kipindi chote, Tume itengewe fedha za kutosha kwa ajili ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura kila mwaka.
(ix) Elimu ya Uraia
Tume ilipendekeza Serikali iangalie uwezekano wa kuunda Chombo cha kutoa, kusimamia na kuratibu Elimu ya Uraia.
B. MAPENDEKEZO MAPYA
(i) Chombo cha Kugawa Majimbo na Kata Kiwe Kimoja
Kwa sasa Tume ina mamlaka ya kugawa majimbo ya Uchaguzi na kuyatangaza. OWM- TAMISEMI ina mamlaka ya kugawa Kata na Kuzitangaza. Tume inatangaza Maeneo ya Uchaguzi baada ya kuletewa orodha ya Kata na OWM – TAMISEMI. Majimbo ya Uchaguzi yanajumuisha maeneo ya Uchaguzi ambayo katika Halmashauri husika ni Kata. Inapotokea OWM – TAMISEMI kutangaza Kata baada ya Tume kutangaza Majimbo ya Uchaguzi inajitokeza haja ya kurekebisha mipaka ya Majimbo na hivyo kuathiri Ratiba Rasmi ya Uchaguzi. Hivyo, Tume inapendekeza chombo cha kugawa Majimbo na kata kiwe kimoja.
(ii) Serikali Kutoa Miadi ya Kiasi cha Fedha za Kugharamia Chaguzi Mapema
Shughuli za Uchaguzi zinagharamiwa na Serikali na Washirika wa Maendeleo. Mara nyingi Washirika wa Maendeleo wanapenda kufahamu mapema kiasi ambacho kitatolewa na Serikali kabla wao kuahidi kiasi watakachotoa. Hivyo, Tume inapendekeza Serikali itoe miadi yake mapema baada ya kupokea makadirio ya gharama za Uchaguzi kutoka Tume.
(iii) Tume Kuwa na Maghala Katika Halmashauri
Shughuli za Uchaguzi zinahusisha matumizi ya vifaa vingi, ambavyo vinatakiwa kutunzwa kwenye Halmashauri husika vikisubiri Uchaguzi mwingine. Kwa kuwa Halmashauri zina vifaa vingine vingi inakuwa vigumu kupata maghala ya kutosha kutunza vifaa vyote vya Uchaguzi.
Tume inapendekeza iwezeshwe kujenga maghala katika kila Halmashauri kwa ajili ya kutunza vifaa vya Uchaguzi.
(iv) Sheria ya Gharama za Uchaguzi Iangaliwe Upya
Tume inapendekeza Sheria ya Gharama ya Uchaguzi, ya mwaka 2010 iangaliwe upya ili kuviainisha na kuvirekebisha vifungu vinavyokinzana na Sheria za Uchaguzi.
(v) Tume Kuandikisha Wapiga Kura Wote Tanzania Zanzibar
Ili kuwa na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura moja Tanzania, Tume inapendekeza ipewe mamlaka ya kuandikisha nchi nzima. Hivyo, Tume inapendekeza kifungu cha 12A kifutwe katika Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ili kuiwezesha Tume kuandikisha Wapiga Kura wote Tanzania Zanzibar – kwa Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano.
(vi) Serikali Kutangaza Maeneo ya Kiutawala Mapema
Tume inapendekeza ugawaji wa Mikoa, Wilaya, Kata, Vijiji , Mitaa na Vitongoji ufanyike mapema ili kuiwezesha Tume kujiandaa kwa Uchaguzi.
(vii) Tume Iwe na Ofisi Katika Kanda, Mikoa na Majimbo
Tume ina Watendaji wa Kudumu Makao Makuu tu. Lakini shughuli za Uchaguzi ni endelevu. Ili kutekeleza shughuli za Uchaguzi kwa ufanisi Tume inapendekeza iwe na Ofisi za Kanda, Mikoa na Majimbo.
VIAMBATISHO
Kiambatanisho A: Orodha ya Kata Zilizofanya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010
Na.
|
Halmashauri ya
|
Kata
|
Sababu
|
1
|
Wilaya ya Ludewa
|
1
|
Lupingu
|
Kifo
|
2
|
Wilaya ya Rufiji
|
2
|
Ngorongoro
|
Kifo
|
3
|
Wilaya ya Mkuranga
|
3
|
Shungubweni
|
Kifo
|
4
|
Wilaya ya Bukoba
|
4
|
Kasharu
|
Kifo
|
5
|
Wilaya ya Hai
|
5
|
Masama Kusini
|
Kifo
|
|
Wilaya ya Serengeti
|
6
|
Busawe
|
Kifo
|
|
|
7
|
Kisangura
|
Kifo
|
7
|
Mji wa Korogwe
|
8
|
Old Korogwe
|
Kifo
|
8
|
Manispaa ya Sumbawanga
|
9
|
Kizitwe
|
Kifo
|
|
|
10
|
Matanga
|
Kifo
|
9
|
Wilaya ya Kasulu
|
11
|
Nyamidaho
|
Kifo
|
10
|
Wilaya ya Nkasi
|
12
|
Kabwe
|
Kifo
|
|
|
13
|
Namanyere
|
Kifo
|
11
|
Wilaya ya Sumbawanga
|
14
|
Katazi
|
Kifo
|
12
|
Wilaya ya Maswa
|
15
|
Nguliguli
|
Kifo
|
|
|
16
|
Ipililo
|
Kifo
|
13
|
Manispaa ya Songea
|
17
|
Majengo
|
Kifo
|
14
|
Wilaya ya Muheza
|
18
|
Masuguru
|
Kifo
|
15
|
Wilaya ya Tunduru
|
19
|
Marumba
|
Kifo
|
|
|
20
|
Muhuwesi
|
Kifo
|
16
|
Manispaa ya Arusha
|
21
|
Sombetini*3
|
Kufukuzwa na Kuhama Chama
|
|
|
22
|
Kati
|
Kifo
|
17
|
Wilaya ya Moshi
|
23
|
Kilema-Kaskazini
|
Kifo
|
18
|
Jiji la Tanga
|
24
|
Ngamiani Kati
|
Kifo
|
|
|
25
|
Chongoleani
|
Kifo
|
19
|
Wilaya ya Ukerewe
|
26
|
Bukindo
|
Kifo
|
20
|
Wilaya ya Sengerema
|
27
|
Bupandwa
|
Kifo
|
|
|
28
|
Nyamazugo
|
Kifo
|
|
|
29
|
Busisi
|
Kifo
|
21
|
Wilaya ya Muleba
|
30
|
Kibanga
|
Kifo
|
22
|
Wilaya ya Ngara
|
31
|
Kabanga
|
Kifo
|
23
|
Wilaya ya Mpanda
|
32
|
Katuma
|
Kifo
|
24
|
Wilaya ya Nachingwea
|
33
|
Nditi
|
Kifo
|
|
|
34
|
Naipanga
|
Kifo
|
25
|
Manispaa ya Tabora
|
35
|
Ng’ambo
|
Kifo
|
|
|
36
|
Malolo
|
Kifo
|
26
|
Wilaya ya Urambo
|
37
|
Ushokola
|
Kifo
|
27
|
Wilaya ya Songea
|
38
|
Wino
|
Kifo
|
28
|
Wilaya ya Kigoma
|
39
|
Nguruka
|
Kifo
|
29
|
Wilaya ya Moshi
|
40
|
Uru-Mashariki
|
Kuhama Chama
|
30
|
Wilaya ya Tarime
|
41
|
Tarime Mjini
|
Kifo
|
31
|
Wilaya ya Korogwe
|
42
|
Mnyuzi
|
Kifo
|
32
|
Wilaya ya Ludewa
|
43
|
Lupingu
|
Kifo
|
33
|
Wilaya ya Magu
|
44
|
Sukuma
|
Kifo
|
34
|
Wilaya ya Mbarali
|
45
|
Rujewa
|
Kifo
|
35
|
Wilaya ya Morogoro
|
46
|
Mtombozi
|
Kifo
|
36
|
Wilaya ya Misenyi
|
47
|
Kitobo
|
Kifo
|
37
|
Wilaya ya Tandahimba
|
48
|
Mnyawa
|
Kifo
|
|
|
49
|
Mkundi
|
Kifo
|
|
|
50
|
Mahuta
|
Kifo
|
38
|
Manispaa ya Kigoma/Ujiji
|
51
|
Machinjioni
|
Kifo
|
39
|
Wilaya ya Mbinga
|
52
|
Utiri
|
Kifo
|
40
|
Manispaa ya Ilala
|
53
|
Upanga-Mashariki
|
Kifo
|
41
|
Wilaya ya Makete
|
54
|
Matamba
|
Kifo
|
42
|
Jiji la Mbeya
|
55
|
Forest
|
Kifo
|
43
|
Wilaya ya Iramba
|
56
|
Shelui
|
Kifo
|
44
|
Wilaya ya Ileje
|
57
|
Ngulugulu
|
Kifo
|
45
|
Wilaya ya Kahama
|
58
|
Mwalugulu
|
Kifo
|
46
|
Wilaya ya Masasi
|
59
|
Lipumburu
|
Kifo
|
47
|
Wilaya ya Chunya
|
60
|
Namkukwe
|
Kifo
|
48
|
Wilaya ya Iringa
|
61
|
Ulanda
|
Kifo
|
|
|
62
|
Ifunda
|
Kifo
|
49
|
Wilaya ya Kwimba
|
63
|
Mwandu
|
Kifo
|
50
|
Wilaya ya Magu
|
64
|
Mkula
|
Kifo
|
51
|
Wilaya ya Geita
|
65
|
Kagu
|
Kifo
|
52
|
Wilaya ya Mvomero
|
66
|
Langari
|
Kifo
|
53
|
Wilaya ya Bahi
|
67
|
Mundemu
|
Kifo
|
54
|
Manispaa ya Singida
|
68
|
Utemini
|
Kujiuzulu
|
55
|
Wilaya ya Monduli
|
69
|
Monduli Juu
|
Kufukuzwa kwenye Chama
|
|
|
70
|
Esilalei
|
Kifo
|
56
|
Wilaya ya Igunga
|
71
|
Bukoko
|
Kifo
|
57
|
Wilaya ya Mpwapwa
|
72
|
Lumuma
|
Kujiuzulu
|
58
|
Wilaya ya Mufindi
|
73
|
Ihowanza
|
Kifo
|
59
|
Wilaya ya Mbeya
|
74
|
Ulenje
|
Kifo
| |