Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə27/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   23   24   25   26   27   28   29   30   ...   33


Kiambatisho B: Maombi ya kugawa Majimbo ya Uchaguzi mwaka 2010

Na.

Mkoa

Idadi ya maombi yaliyowa-silishwa na Halmashauri

Idadi ya Halmashauri zilizoomba kuchunguza/ kugawanya Majimbo

Majimbo yaliyoomba kurekebisha mipaka kufuatia kugawanywa Majimbo

Idadi ya Majimbo yaliyoomba kubadilisha majina

Idadi ya Majimbo mapya yanayoo-mbwa

1

Ruvuma

2

2







2

2

Singida

1

1







1

3

Lindi

1

1







1

4

Mwanza

2

2







2

5

Rukwa

6

3




3

1

6

Shinyanga

6

6







6

7

Iringa

1

1







1

8

Kagera

2

2







2

9

Manyara

2

1

1




1

10

Mtwara

2

2







2

11

Tabora

5

5







5

12

Mara

1

1







1

13

Dar es Salaam

4

3

1




4

14

Arusha

1

1







1

15

Morogoro

4

4







4

16

Mbeya

6

6







7

17

Kigoma

4

3




1

3

18

Dodoma

3

3







3

19

Kilimajaro
















20

Tanga
















21

Pwani






















53

47

2

4

47


Kiambatanisho B: Asasi za Kiraia Zilizoruhusiwa Kutoa Elimu ya Mpiga



NA.

Jina la Asasi

Maeneo ya kutoa Elimu ya Uraia au Elimu ya Mpiga Kura

1

Ngo Network for Dodoma (NGONEDO)

Dodoma

2

Education Development Foundation (EDFO)

Mwanza, Kagera na Shinyanga (Lake Zone)

3

Inades Formation Tanzania

Dodoma na Singida

4

CHAWATA DODOMA

Dodoma Mjini

5

Iringa Development of Youth, Disabled and Children Care (IDYDC)

Iringa Mjini, Vijijini, Kilolo, Mufindi

6

Jikomboe Intergrated Development (JIDA)

Tabora, Shinyanga na Singida

7

AFNET Dodoma

Dodoma, Singida, Iringa, Arusha na Manyara

8

Kisamabantu Arts Promotions

Ruvuma, Lindi na Mtwara

9

TCCIA RUVUMA

Wilaya ya Songea

10

Manyara Region Civil Society Organization Network (MACSNET)

Manyara

11

Ngara Umoja

Ngara

12

Kagera Community Development Fund

Muleba

13

Tanzania Women of Impact Foundation

Kata ya Handeni

14

Diocese of Kigoma – Justice and Peace Commission

Kigoma na Kibondo

15

Community Development and Relief Trust (CODERT)

Geita

16

Mbulu Environmental Society (MBESO)

Mbulu

17

Women’s Savings and Credit in Muleba District (WOSCA)

Wilaya ya Muleba

18

Lawyers Environmental Action Team (LEAT)

Kata ya Bukene, Hobo, Ijanija, Nzega.

19

The Good Samaritan Social Service Tanzania Dsm

Maili Moja, Tumbi, Mkuza, Kibaha, Kongowe, Misugusugu, Pangani na Visiga

20

The Citizen Development Network

Mkuranga na Mafinga

21

Umoja Wa Wanawake wa Kiislam Maswa

Maswa

22

Grace Community Development and Education (GCDE)

  1. Sumbawanga Vijijini-Ilemba, Kilyamatundu, Sndulula, Milepa Kasesha, Matai, Mtowisa, Muze, Mfinga, Miangalua, Laela, Mwimbi na Ulumi.

  2. Sumbawanga Mjini – Mandela Stadium na Kisumba.

23

Dhahabu Arts Group

Kinondoni – Ubungo, Bunju, Mbweni, Kunduchi, Sinza and Kawe

24

Christian Education and Development

Kata Za Bukene, Mwangoye, Itobo, Ijinija, Nzega

25

Universal Federation (UFP)

Tanzania Bara tu


26

Women’s Economic Groups Co-ordinating Council (WEGCC)

Arusha, Singida, Shinyanga Na Tabora

27

Buturi Community Fund Non-Governmental Organization

Ilala, Mkuranga na Bagamoyo

28

Mtwara Action For Self Help Activities (MASHA)

Mtwara, Nanyamba na Mtumbuka

29

OMGP’s Forum

Nkasi, Mvomero, Simanjiro, Hanang’, Mbulu, Longido, Meatu na Monduli

30

Southern Africa Extension Unit

Kigoma, Kilimanjaro, Iringa, Mbeya, Morogoro, Pwani na Tanga

31

Friends For Social Change

Dar es Salaam, Morogoro na Pwani

32

Tanzania Muslim Proffessionals Association (TAMPRO)

Mwanza, Ukerewe, Bunda, Shinyanga na Kahama

33

Chama Cha Wasioona Tanzania

Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Tabora, Tanga, Mwanza, Kigoma na Rukwa

34

The International Good Samaritan Mission (MIBOS)

Wilaya ya Kigoma

35

Tumaini University Iringa College

Iringa, Ruvuma, Lindi na Mtwara

36

Union of Non Governmental Organization Morogoro

Morogoro

37

New Chapter Save The Children Of Mwanza

Mwanza

39

Ilala Mitumba Cooperative Society

Dar es Salaam

39

M M Associate, Advocates

Dar es Salaam, Tanga na Lushoto

40

Konrad Adenauer Stiftung

Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara

41

Tanzania Youth New Fashion

Tabora

42

Women Legal Action

Ruvuma

43

Baraza Kuu La Waislamu Tanzania (BAKWATA) Dar Es Salaam

Mkuranga, Rufiji, Kilwa, Pangani, Nachingwea, Tandahimba na Lindi

44

Music Mayday

Dar es Salaam, Morogoro, Arusha, Mwanza na Shinyanga

45

Rulu Arts Promoters

Rufiji, Mafia, Bagamoyo, Mkuranga, Arumeru, Longido

46

Campaign For Good Governance

Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kilwa, Songea, Chunya, Sumbawanga, Lushoto, Simanjiro, Sengerema, Magu, Kwimba, Nzega, Dodoma, Kilombero na Mvomero

47

Youth Partnership Countrywide

Mlandizi, Kwala, Ruvu Kongowe, Tumbi, Maili Moja na Pangani.

48

Tumaini University Dar Es Salaam College

Sengerema, Tarime na Karagwe

49

Kalambo Social Development Foundation (KASODEFO)

Sumbawanga Vijijini

50

Concern For Development Initiative In Africa (FORDIA)

Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Mara, Ruvuma na Lindi


51

TGNP – Tanzania Gender Networking Program

Tanzania Bara

52

United Nations Association Of Tanzania

Kagera, Mara, Shinyanga na Mwanza

53

Wete Invironmental Conservation Club

Pemba na Unguja

54

Woman In Social Enterpreneurship (WISE)

Newala, Lindi Vijijini, Temeke, Kinondoni na Kibaha

55

Hearing Tanzania

Pwani na Tanga

56

Tanganyika Law Society

Tanzania Bara

57

Iritongo Conflicts Resolution and Development Initiative Movement (CORDIM)

Bunda, Musoma Vijijini, Rorya, Serengeti na Tarime

58

Lake Victoria Disability Centre

Mkoa wa Manyara

59

Tanzania League Of The Blind

Dar es Salaam, Tabora, Pwani, Kigoma, Singida, Manyara na Tanga

60

Pamoja Trust

Kilimanjaro, Arusha na Manyara

61

Singida Yetu

Singida

62

Pastoralists Indigenous Non-Government Organization Forum ( PINGOs)

  • Arusha – Monduli, Longido

  • Manyara – Hanang, Mbulu, Simanjiro

  • Shinyanga – Meatu

  • Rukwa - Mpanda, Nkasi

  • Morogoro – Kilosa, Mvomero

63

Pemba Investment and Youth Development Organization ( PIYDO)

  • North Pemba – Wate, Micheweni

  • South Pemba – Chakechake, Mkoani

64

Organization of Women with Disabilities Zanzibar ( JUWAUZA)

  • Mjini Magharibi

  • Kusini Unguja (Kaskazini A na Kaskazini B)

  • Kaskazini Unguja (Kaskazini A na Kaskazini B)

65

White Star Society ( WSS)


Kiambatanisho C: Hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi


HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, MHE. JAJI MST. LEWIS M. MAKAME KATIKA HAFLA YA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAREHE 05 NOVEMBA, 2010

UKUMBI WA KARIMJEE, DAR ES SALAAM
Waheshimiwa Wagombea Kiti cha Urais na Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Waheshimiwa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Viongozi wa Madhehebu ya Dini;

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi mbalimbali;

Waheshimiwa Wageni waalikwa;

Ndugu Wananchi;

Mabibi na Mabwana.


Kama mnavyofahamu, kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria za Uchaguzi, nchi yetu imefanya Uchaguzi wa Urais, Wabunge na Madiwani tarehe 31 Oktoba, 2010 chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, natoa shukrani za dhati kwa Wapiga Kura na Vyama vya Siasa kwa kushiriki katika Uchaguzi huu. Aidha, natoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wadau wa Uchaguzi na Washirika wa Maendeleo ambao kwa namna moja au nyingine wameiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendesha na kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kwa kuzingatia Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura 292, Matokeo ya Uchaguzi wa Bunge na Madiwani, nchi nzima yamekwishatangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaohusika isipokuwa kwa Majimbo saba (7) na Kata 23.
Kwa mujibu wa Vifungu vya 35E, 35F(8) na 81B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, baada ya kujumlisha kura zote za Uchaguzi wa Rais zilizopokelewa kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo yote 239, inatakiwa kutangaza rasmi Matokeo ya Uchaguzi wa Urais. Kazi hii ndiyo inayotujumuisha leo katika Ukumbi huu.
Waheshimiwa Wagombea wa Kiti cha Urais, Waheshimiwa Viongozi, Waheshimiwa Mabalozi, Wageni waalikwa na Ndugu wananchi, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu Vyama vya Siasa saba (7) vilisimamisha Wagombea wa Kiti cha Urais na Umakamu wa Rais. Vyama hivyo kialfabeti pamoja na Wagombea wake ni kama ifuatavyo:-


NA.

CHAMA

MGOMBEA URAIS

MGOMBEA UMAKAMU WA RAIS

1

APPT-MAENDELEO

Mhe. Mziray Kuga Peter

Mchenga Rashid Yusuph

2

CCM

Mhe. Kikwete Jakaya Mrisho

Bilal Mohammed Gharib

3

CHADEMA

Mhe. Slaa Willibrod Peter

Said Mzee Said

4

CUF

Mhe. Lipumba Ibrahim Haruna

Duni Juma Haji

5

NCCR - MAGEUZI

Mhe. Rungwe Hashim Spunda

Ali Omar Juma

6

TLP

Mhe. Mgaywa Muttamwega Bhatt

Mgaza Abdallah Othman

7

UPDP

Mhe.Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa

Hamad Mohammed Ibrahim

Yafuatayo ndiyo Matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 31 Oktoba, 2010:-



  1. Idadi ya Wapiga Kura waliojiandikisha ni 20,137,303.

  2. Idadi ya waliopiga kura 8,626,283 ambao ni sawa na asilimia 42.84(%) ya Wapiga Kura wote waliojiandikisha.

  3. Idadi ya Kura zilizoharibika ni 227,889 ambazo ni sawa na asilimia 2.64(%) ya Kura zote zilizopigwa.

  4. Idadi ya Kura halali ni 8,398,394 ambazo ni sawa na asilimia 97.36(%) ya Kura zote zilizopigwa.

  5. Idadi ya Kura halali alizopata kila Mgombea ni kama ifuatavyo:-

(i) Mhe. Mziray Kuga Peter wa Chama cha African Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) amepata Kura 96,933 ambazo ni sawa na asilimia 1.12(%) ya Kura zote halali;

(ii) Mhe. Kikwete Jakaya Mrisho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amepata Kura 5,276,827ambazo ni sawa na asilimia 61.17(%) ya Kura zote halali;


(iii) Mhe. Slaa Willibrod Peter wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepata Kura 2,271,941 ambazo ni sawa na asilimia 26.34(%) ya Kura zote halali;
(iv) Mhe. Lipumba, Ibrahim Haruna wa Chama cha ‘The Civic United Front’ (CUF) amepata Kura 695,667 ambazo ni sawa na asilimia 8.06(%) ya Kura zote halali;
(v) Mhe. Rungwe Hashim Spunda wa Chama cha ‘National Convention for Construction and Reform’ (NCCR – MAGEUZI) amepata Kura 26,388 ambazo ni sawa na asilimia 0.31(%) ya Kura zote halali;
(vi) Mhe. Mgaywa Muttamwega Bhatt wa ‘Tanzania Labour Party’ (TLP) amepata Kura 17,482 ambazo ni sawa na asilimia 0.20(%) ya Kura zote halali;
(vii) Mhe. Dovutwa Yahmi Nassoro Dovutwa wa Chama cha ‘United Peoples Democratic Party’ (UPDP) amepata Kura13,176 ambazo ni sawa na asilimia 0.15(%) ya Kura zote halali.
Kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Mgombea wa Kiti cha Urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko Mgombea mwingine yeyote. Aidha, kwa mujibu wa Ibara ya 47(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Mgombea wa Kiti cha Urais akichaguliwa basi na Mgombea Mwenza wake atakuwa amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais.
Kwa kuwa Mheshimiwa JAKAYA MRISHO KIKWETE wa CCM amepata kura nyingi zaidi kuliko Mgombea mwingine yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa Vifungu vya 35E, 35F(8) na 81B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi Matokeo ya Uchaguzi wa Urais wa 2010 kwamba:-


  1. Mheshimiwa KIKWETE JAKAYA MRISHO amechaguliwa kuwa RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
1   ...   23   24   25   26   27   28   29   30   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət