Ana səhifə

Taarifa ya tume ya taifa ya uchaguzi kuhusu uchaguzi wa rais, wabunge na


Yüklə 4.81 Mb.
səhifə12/33
tarix26.06.2016
ölçüsü4.81 Mb.
1   ...   8   9   10   11   12   13   14   15   ...   33

Ufuatiliaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Ili kuhakikisha shughuli za Uboreshaji wa Taarifa za Wapiga Kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura zinafanyika kwa ufanisi Tume ilifuatilia Zoezi la Uboreshaji katika mikoa yote.
Ufuatiliaji ulifanyika katika hatua zote za Uboreshaji kuanzia kwenye utoaji mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji (ROs) na Maafisa Waandikishaji Wasaidizi (AROs) ngazi ya jimbo mpaka kwenye hatua ya Uboreshaji Vituoni.
Wakati wa ufuatiliaji Tume ilihakikisha kuwa taratibu zote zilizingatiwa katika Vituo vya Uandikishaji. Kutokana na ufuatiliaji, Tume iliweza kutambua:-

    1. Wawezeshaji/Wakufunzi ambao kimsingi hawakuelewa mafunzo na kuwapa msaada wakati wa mafunzo hasa katika Mafunzo kwa Waandishi Wasaidizi na Wapiga Picha.

    2. Mapungufu ya vifaa vya uandikishaji vilivyotumika vituoni ambayo yalishughulikiwa ipasavyo.

    3. Makosa ambayo yalikuwa yakifanyika kwenye Vituo vya Uandikishaji na kuyarekebisha kabla ya kuleta athari katika zoezi zima la Uboreshaji.

    4. Maeneo ambayo mafunzo hayakutolewa kwa umakini na kwa usahihi.



    1. Teknolojia Zilizotumika Kuandaa Daftari


Tume ilitumia Teknolojia inayotumia fomu maalumu inayojulikana kama Medium Tech solution katika kuchukua Taarifa za Wapiga Kura na kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Teknolojia hii inahusisha matumizi ya Fomu Maalumu zinazosomwa na Mfumo wa OMR, ICR na OCR baada ya kufanyiwa scanning. Pia Teknolojia hii inawezesha kuwa na ulinzi wa kutosha wa taarifa za Wapiga Kura na ni rahisi pia kufanya audit-trail kwa kufuatilia jinsi Fomu zilivyoshughulikiwa katika hatua mbalimbali.
Katika Uboreshaji wa Awamu zote mbili Tume iliboresha mifumo iliyotumika awali kwa kubadilisha vifaa vya upigaji picha kwa sababu Teknolojia ya Kamera za Polaroid ilikuwa haitumiki tena na hivyo utengenezaji wa VIVA films ulisitishwa kote duniani.
Teknolojia iliyotumika katika Awamu ya Pili ni ya Digital Instant Photo Capturing Solution ambayo ilihusisha vifaa vya Kamera za digitali, printa, kifaa cha kupokea mionzi ya jua (solar panel), kihifadhi nishati ya jua (solar power pack), betri za printa, karatasi za kuchapishia picha na masanduku ya kubebea vifaa hivyo.
    1. Fomu Zilizotumika Katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Katika zoezi la Uboreshaji zilitumika fomu za aina kuu mbili ambazo ni Fomu maalumu za OMR ambazo husaidia kuingiza taarifa, kusahihisha au kubadili taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Voters Database) na Fomu za kusaidia Mchakato wa Uboreshaji ambazo siyo za OMR.
Fomu zote zilifanyiwa marekebisho ili kuweza kukamilisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari kwa ufanisi.

    1. Mifumo ya Kompyuta Iliyotumika


Tume ilitumia mifumo mbalimbali ili kurahisisha utayarishaji na utunzaji wa Daftari:-

  1. Mfumo wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (PNVR) ulisaidia kufanya uchambuzi wa Fomu za Wapiga Kura na kuandaa Daftari kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu na Chaguzi Ndogo ambazo zingejitokeza. Mfumo wa PNVR umeunganishwa na mifumo mingine na kufanya kazi kama mfumo mmoja (Intergrated System) ambao unasaidia hatua mbalimbali za Uchaguzi.

  2. Mfumo wa Maghala na Lojistiki (Warehouse and Logistics Management System).

  3. Mfumo wa Ramani (Geographical Information System) - GIS.

  4. Mfumo wa Mawasiliano na Utoaji wa Taarifa za Matukio (Communication and Incidence Management System).

  5. Mfumo wa kudhibiti usalama katika kituo cha kutunzia Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Access Control System).

  6. Mfumo wa Mpiga Kura kupata taarifa zake (Voter Interaction System).

  7. Mfumo wa Menejimenti ya Wagombea (Candidate Management System).

  8. Mfumo wa Menejimenti ya Matokeo ya Kura (Result Management System).



      1. Mtandao wa Mawasiliano


Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kituo cha Maandalizi ya Daftari pamoja na vituo vingine vya kutunzia kumbukumbu za Wapiga Kura vimeunganishwa na Mtandao wa Mawasiliano, ambao unahakikisha usalama kwa taarifa zote.

    1. Mabadiliko ya Vifaa vya Kupigia Picha


Vifaa muhimu katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari ni vifaa vya kupigia picha za papo kwa papo ili Tume iweze kutoa kitambulisho pindi Mpiga Kura atakapojiandikisha, na Fomu maalum za OMR zinazotumika kuingiza au kufanya marekebisho katika Database.
Katika Awamu ya Pili, Tume ililazimika kubadili Teknolojia ya upigaji picha kutoka Polaroid kwenda Digitali ambayo ilihusisha Kamera za Digitali, Printa, Vifaa vya Nishati ya Jua na Karatasi za Kuchapishia Picha ambavyo vilinunuliwa na (UNDP) kupitia Programu ya Kukuza Demokrasia Tanzania (DDTP).

    1. Watendaji Katika Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura


Watendaji waliotumika katika Zoezi la Uboreshaji ni wale walioteuliwa na Tume kwa mujibu wa Sheria ambao ni pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wilaya ambao ndiyo walikuwa Maafisa Waandikishaji. Watendaji wengine ni Waratibu wa Uandikishaji wa Mikoa, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo na Kata, Waandishi Wasaidizi na Wapiga Picha.


Watendaji wote walipatiwa mafunzo kwa njia ya mtiririko (Cascade Training) na Maelekezo mbalimbali yaliandaliwa kwa ajili ya kutumika wakati wa Zoezi la Uboreshaji. Watendaji waliweza kumudu kazi zao licha ya kuwa na matatizo machache.

    1. Kuchapisha na Kuweka Wazi Daftari la Awali

Baada ya uchambuzi kukamilika, Daftari la Awali lilichapishwa na kurudishwa kwa Wapiga Kura ili wakague taarifa zao.


Katika Uboreshaji wa Awamu ya Kwanza uwekaji wazi wa Daftari ulifanyika katika Ofisi za Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ambapo Wapiga Kura walitakiwa kwenda kwenye Ofisi hizo ili kukagua taarifa zao.
Awamu ya Pili ya Uboreshaji wa Daftari, uwekaji wazi wa Daftari la Awali ulifanyika katika Vituo ambavyo Wapiga Kura walijiandikisha. Hii ilipunguza umbali wa safari ya kwenda Ofisi za Maafisa Waandikishaji Wasaidizi wa Kata kama ilivyokuwa Awamu ya Kwanza. Lengo lilikuwa kuwawezesha Wapiga Kura wengi zaidi kukagua taarifa zao ili zisahihishwe kama zimekosewa.
Jedwali Na. 12: Ratiba ya Uwekaji Wazi Daftari kwa Awamu ya Kwanza na Awamu ya Pili



Awamu ya Kwanza

Tarehe

Kanda ya Kwanza

(Lindi na Mtwara)

8 – 14/06/2008



Kanda ya Pili

(Mbeya, Rukwa, Ruvuma na Iringa)

Kanda ya Tatu

(Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma)

28/7 – 30/08/2008




Kanda ya Nne

(Mwanza na Kagera)

Kanda ya Nne

(Shinyanga na Mara)

8 -14/12/2008

Kanda ya Tano

(Kilimanjaro,Arusha, Manyara na Tanga)



8 -14/12/2008

Kanda ya Sita

(Pwani na Morogoro)



14- 20/01/2009

Kanda ya Saba

(Dar es Salaam)



11 -17/04/2009







Awamu ya Pili

Tarehe

Kanda ya Kwanza

(Lindi, Mtwara, Iringa na Ruvuma)

22 – 27/01/2010

Kanda ya Pili

(Mbeya, Rukwa, Dodoma na Singida)

15 – 19 /02/2010

Kanda ya Tatu

(Kigoma, Tabora, Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga)

05 – 10/04/2010

Kanda ya Nne

(Arusha, Kilimanjaro na Manyara)

10 -14/05/2010

Kanda ya Tano

(Morogoro, Pwani na Tanga)

24 – 28/05/2010

Kanda ya Sita

(Dar es Salaam)

29/06 – 04/07/2010

Kanda ya Saba

(Tanzania Zanzibar)

19 – 23/07/2010



Muhimu:

  • Kata ya Ipililo, Halmashauri ya Maswa Uwekaji Wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura ulifanyika tarehe 5 – 10/09/2008 ili kufanikisha Uchaguzi Mdogo wa Udiwani uliofanyika tarehe 21/09/2008.

  • Jimbo la Tarime na Kata ya Kisangura Uwekaji Wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura ulifanyika tarehe 8 – 14/09/2008 ili kufanikisha Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani.

  • Kata ya Upanga Mashariki, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Uwekaji Wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura ulifanyika tarehe 9 -14/01/2009 ili kufanikisha Uchaguzi Mdogo wa Udiwani uliofanyika tarehe 25/01/2009



1   ...   8   9   10   11   12   13   14   15   ...   33


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət