Ana səhifə

Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahiim Harakati za Uislamu dhidi ya Ahmadiya Chungu Mosi, Rabiul Awwal 1430 Februari 24, 2009


Yüklə 0.51 Mb.
səhifə2/5
tarix26.06.2016
ölçüsü0.51 Mb.
1   2   3   4   5

"Umma wa Arya (Wahindu) unahamasika na kushawishika sana na ni umma wenye umoja ambao kwa jambo dogo tu ambalo halina msingi katika dini yao wanakuwa wamoja na maelfu ya rupia hukusanywa kwa muda mfupi tu". Hivyo, umma huo unaoweza kuhamasika na kushawishika kwa jambo dogo lisilo na maana, mtu anaweza kuhisi nini watu hao wangefanya kama lingekuwa jambo fulani kubwa. Waislamu wanaojitenga wajizike wenyewe wangali hai. Kama hawana mapenzi kwa Mungu na Mtume vipi tena wadai kuwa wao ni Waislamu. Je huu ndio Uislamu wao wa kutoa kiasi kisicho na ukomo katika mambo ya uovu na kuendekeza matamanio yao ya kimwili huku wakiwa na nia ya kuinua heshima zao, pasipo kutoa hata senti moja kwa mapenzi juu ya Mungu na Mtume na kwa huruma..." (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-i-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.51)
"Matajiri wengi wa Kiislamu hufikiri kuwa dini ni kitu fulani kinachohitaji msaada kutoka kwa masikini ambapo matajiri wanajitenga nayo, ambao hawawajibiki hata kuchangia mzigo huu." (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-i-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.51)
"Japo nilikuwa nimetangaza kwamba kwa sababu ya kuongezeka kwa ukubwa wa kitabu, bei ya

"Waislamu wabakhili na wabanizi ambao wanatajika kwa sifa na majina nao kama Qaruun wanabania mapesa mengi....." (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-i-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.52)


Hatimaye MGAQ alipotanabahi kuwa hatapata kingine chochote kutoka mifukoni mwa watu kwa ajili ya Brahiin-i-Ahmadiyya, akaamua kuacha. Licha ya kupokea malipo ya kubandika ya juzuu 50 kutoka kwa wateja wengi watarajiwa, aliacha kuchapisha kitabu na akatulia tuli kabisa akighafilika kuwa yeye si alidai kuwa katumwa na Mungu kuandika kitabu hicho. Kwa nini? Kwa sababu alitanabahi kuwa kwa kipindi kijacho cha miaka 20 angekuwa anachapisha kitabu bila malipo yoyote. Licha ya hicho alichodai, kumbe kuutumikia Uislamu hakukuwa lengo lake. Yeye alitaka pesa. Wateja walipochachamaa, akachapisha tangazo la kurasa 8 baada ya miaka 10, mnamo Mei 1 1893, tangazo hilo lilipewa jina, 'Brahiin-i-Ahmadiyya na Wateja wake." Zifuatazo ni baadhi ya sehemu:
"....hii ni kweli kwamba katika siku hizi 10 wateja wengi wamefariki dunia na wengi wamekata tamaa baada ya kusubiri kwa muda mrefu, lakini inabidi izingatiwe kwa haki kuwa kwani walizuiwa kabisa kukitazama kitabu? Je hawakuziona sura 36 za kitabu hiki zilizojaa ukweli na hekima? Na yabidi izingatiwe ni jinsi gani ilivyo vigumu kuukabili ulimwengu mzima na matatizo gani tunayokabiliana nayo?....mbali ya hilo wanunuzi hawa wenye shaka kama wanataka pia si wanaweza kufikiria kwani wananyimwa kitabu hicho baada ya kuchukua kwao hizo Rs 5 au 10?....japokuwa huu ni ukweli kuwa kumekuwa na ukawiaji usio wa kawaida katika kutoa sehemu iliyosalia ya kitabu lakini ni ukatili mkubwa kupindukia wa baadhi ya wanunuzi kwamba hawakuzingatia thamani ya kitabu hiki cha ajabu...Mimi najua fika kuwa wale ambao wamenicharukia kuwa nimefuja pesa zao na kwamba sehemu iliyosalia ya kitabu haijachapishwa hadi sasa, hawa hawakusoma kitabu cha Brahiin-i-Ahmadiyya kwa utashi na haki. Laiti wangelikiri kuwa wao ndio wamekula matunda zaidi ya Brahiin na wamepata faida kubwa zaidi kuliko pesa zao.....Mimi nahuzunishwa na hali hii ya Waislamu ukilinganisha na vijirupia 5 au 10 wanapata sura 36 za kitabu kilichojaa hikima ya Uislamu, eti wao wanapamba moto kuchafuana na kutukanana matusi namna hiyo kana kwamba pesa zao zimeibwa na mwizi au wameporwa na kana kwamba wameporwa kijambazi kwamba hakuna kitu kilichotolewa kwao....." (Tangazo la Mei 1 1983, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1uk.400-407)
Hili ni tangazo refu linalofaa kusoma. Yeye aliendelea kujigamba kuhusiana na jitihada zake za kishujaa za kuandika juzuu 4 na kuwalamu Waislamu kwa kutovutika nayo. Punde si punde kilichojiri kwa huyu aliyeitwa mteule wa Mungu ni kwamba angalau alichoweza kufanya ni alau kuwaomba radhi wateja wake kwa kuvunja ahadi yake. Akachapisha juzuu ya 5 baada ya miaka 23 ambapo, akiongeza maumivu kwenye donda, aliandika hivi katika dibaji ya juzuu hiyo:
"Mwanzoni nia ilikuwa ni kuandika juzuu 50, lakini kutoka hizo 50 nikawa radhi kuandika 5 na kwa vile tofauti ya 50 na 5 ni sifuri (ambayo kwa Kiurdu inaitwa dot-Rashid) basi kwa hizi juzuu 5 ahadi yangu ndio ishatimia." (Dibaji ya Brahiin-i-Ahmadiyya, juz. 5 uk.9, Roohani Khazain juz.21)
Wakati ule alipochapisha juzuu ya 4 ya Brahiin-i-Ahmadiyya alilivuta kundi kubwa la matajiri na waajiriwa wa serikalis, alikuwa na uhakika kuwa kusingekuwa na tatizo katika kupokea FUTUUHAAT. Hivyo, akaanza kuandika vitabu vingine na kuviuza.
*********************
MGAQ aanza kuandika na kuuza 'vitabu vingine vya Mungu'
"Kwa kuwa Risala Siraj-i-Muniir ambayo itakusanya bishara, itachapishwa kwa gharama ya rupia 1400, basi kabla ya kuchapishwa maombi kutoka kwa wateja hapana budi yapokelewe ili kusiwe na matatizo huko mbele. Bei ya kitabu hiki itakuwa Rupia 1 ukijumlisha na utumaji." (Roohani Khazain juz.2 uk.32. Sa'a Ishtehaar.)
Kijitabu hiki kidogo 'Kuhul al-Jawahir Surma Chasm Aarya' baada ya kukichapa kwa tahadhari kubwa, bei yake imepangwa kuwa Rs.1 na anna 12 kwa watu wa kawaida na watu maalum na wale wanaoweza kumudu, chochote watakachotoa kama msaada...." (Tangazo la Septemba 1886 Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.132)
"Kitabu kimoja maridadi kiitwacho 'Shuhna Haq' ambacho ndani yake ukweli kuhusu falsafa ya Vedic na dini ya Arya umebainishwa waziwazi na kikamilifu, tayari kishachapwa. Bei yake imepangwa kuwa annas 12 bila kujumuisha gharama za utumaji." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.136)
"Nimeandika kitabu chenye maelezo ya kina kiitwacho 'Izala-i-Auham', ambacho kipo tayari baada kukichapa.....na bei yake ni Rs.3.... wanunuzi wa Izala-i-Auham wakumbuke kuwa mimi nakaa Bazaar Billee-Maaraan, Nyumba ya Nawab Loharo na nakala za Izala-i-Auham zinapatikana kwangu. Yeyote atakayelipa Rs.3 anaweza kununua kitabu hiki..." (Tangazo la Okt. 2, 1891 Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk. 233-236)
"Kitabu hiki (Izala-i-Auham) chaweza kupatikana kutoka kwangu na Shirika la Habari la Punjab Press Sialkot kwa njia ya VP Posta." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.266)
"Ifahamike kuwa kitabu changu Izala-i-Auham kinapatikana hapa Patiala kwa Mir Nasir Nawab, Cartographer, Canal Department, Sirhind." (Tangazo wakati akiwa ziarani Partiala, tarehe 31 Okt. 1891, Majmuu-i-Ishtihaarat, mkusanyiko wa Matangazo, juz.1 uk.269)
"Tangu wakati wa uchapishaji wa kitabu Izala-i-Auham zaidi ya kiasi cha fedha cha kawaida kimetumika na pesa inahitajika kulipia haki za mmiliki wa shirika la uchapishaji na karani kwa hiyo marafiki wote wa kweli wanaombwa kusaidia kwa kiasi wanachoweza kwa kununua kitabu hiki haraka. Wale wanaoweza kununua nakala chache, badala ya nakala moja basi wanunue nakala nyingi kwani wana uwezo waliojaaliwa na Mungu..." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.1 uk.287)
"Ndugu yangu Mukarram Mulvi Nuruddin Sahib, Daktari wa Riyasat Jammu, msaada safi ambapo ametuma noti chache sasa yafaa utajwe....hali kadhalika ndugu yangu Mukarram Hakiim Fazal Din Sahib mbali ya ile Rs. 300 ambayo aliituma awali, sasa katuma Rs. 100 zaidi. Ni jambo la kufurahisha mno kwamba Hakiim Fazal Din amepambika kwa rangi ya Mwalimu wake Hakiim Nuruddin kwamba kwa kujitolea, kafanya kwa hamasa amali hizo njema; hivyo, hizi Rs. 100 kazituma baada kuuza kito fulani cha thamani..." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.287-288)
"Kwa dhati kabisa ndugu yangu Molvi Mardan Ali....Ndugu yangu Molvi Zahoor Ali Sahib na Molvi Ghazanfer Ali Sahib wamekubali kutoa mchango wa Rs.10 kila mwezi na wametuma Rs.72 kama msaada...." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo juz.1 uk.288)
"Kuhusiana na watu wote wakweli, ambao wamekula kiapo cha utii (ba'ait) kwangu, ifahamike wazi kwamba madhumuni ya kula kiapo hiki ni kuwa huba ya dunia hupungua na mapenzi kwa Mungu na Mtume (saw) ndiyo yanayotawala moyoni na kujitenga huko na dunia ndiko kunakopelekea njia ya kwenda Akhera isionekane kuwa ni ya kuchukiza.....(na pesa nyingi hupewa Mirza-Rashid...") (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.302)
"Ninazo nakala chache za Risala Fatih Islam na Tauziih-i-Maram ambayo bei yake ni Rs.1 na ninazo nakala chache mno za kitabu Izala-i-Auham ambacho bei yake ni Rs.3 kwa nakala moja." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.304)

"Baada ya uchapishaji wa kitabu hiki ambacho kinaitwa Nishan-i-Aasmani, kitabu Dafe-al-Wasawis nacho kitachapwa na baada ya hicho bila kukawia kitabu Hayat-un-Nabi wa Mamaat-al-Masiih nacho kitachapwa.....na baada ya hicho bila kuchelewa Brahiin Ahmadiyya sehemu ya 5.....lakini ili kudumisha utaratibu huu (wa uchapishaji) mimi naona inafaa kila kitabu nichapishacho, rafiki zangu matajiri wanisaidie kwa moyo wote kwa kukinunua, kwa mtindo huo wanunue nakala moja au zaidi ya moja.....
Iwapo katika Jumuiya yangu kuna watu wanaofaradhikiwa na Zaka kutokana na mali na utajiri na vito vya thamani n.k. Basi waelewe kuwa hivi sasa hakuna masikini na hakuna yatima na hakuna asiyejiweza kama Dini ya Uislamu......kwa toeni zaka kuisaidia dini hii, nunueni vitabu kutokana na zaka na vigaweni bure....na vipo vitabu vingine mbali ya hivi ambavyo navyo pia ni vya manufaa sana...." (Tangazo la tarehe 28 Mei 1892, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.325)
"Aina-i-Kamaalaat-i-Islam....kwa kutawakali kwangu kwa Mungu nimeanza kuchapa nakala 1400 za kitabu hiki.....Rs.1 tu ndiyo bei iliyipangwa kwa ajili ya kitabu hiki lakini gharama za utumaji ni nyingine....nduguzanguni! Leo ndiyo siku ambayo sala za masikini, ilimu ya wanazuoni, na mali ya matajiri vitumike kudhihirisha utukufu wa Uislamu.....Haya amkeni mfanye kazi kwa sababu uhai wa dunia ni siku chache tu na mwisho wake lazima tukutane na Mungu..... hivi sasa na katika zama hizi tajiri akiamka usingizini basi huu ndio wakati bora wa kumridhisha Mungu na Mtume (saw.)" (Tangazo la tarehe 10 Agosti 1892, Mnajmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.333-336).
"Enyi Jamaa wa Mukhlisiin....tunahitaji mno vitu vitatu....1. lazima tuwe na mitambo miwili ya uchapishaji. 2.karani mwenye mwandiko mzuri na 3. karatasi. Kwa vyote hivi vitatu, inakisiwa kuwa Rs.250 zitahitajika kwa mwezi......haya sasa hivi na haraka sana rafiki zangu wote washiriki katika kampeni hii ya mchango ambao mara zote ufike kila mwezi katika tarehe maalum.." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk. 367)
"Aina-i-Kamalaat-i-Islam...hiki kinakusanya takribani kurasa 600, karasi zenye ubora mkubwa, kimeandikwa vizuri na bei yake ni Rs.2, gharama za utumaji ni nyingine na hii ni sehemu ya kwanza tu na sehemu ya pili itachapwa peke yake na bei yake itakuwa tofauti.....kama mnunuzi hapendi kitabu hiki, basi mimi nakubali kuwa warudishe kitabu na mimi nitawarudishia fedha zao bila kukawia lakini kwa sharti kuwa kitabu kirejeshwe ndani ya majuma mawili na kusiwe na alama-alama za mikono au madoa madoa...." (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1. 369-370)
"Someni hii kwa makini kwani kuna habari njema kwenu.

Kwa, Watawala, Watakatifu, Matajiri, Serikali na Maafisa wa Ngazi za Juu
Enyi Viongozi wa Kiislamu! Namuomba Mungu atie nyoyoni mwenu nia zilizo njema zaidi kuliko mtu mwingine yoyote yule na katika nyakati hizi nafuu akajaalieni muwe watumishi wakweli wa Uislamu.Nakupeni taarifa hii muhimu kwa ajili ya MwenyeziMungu tu kwa Mungu kaniteua kuwa kiongozi wa karne hii ya 14 na kanituma kuhuisha Uislamu.....
Ninafanya kazi hii kwa miaka 10 kwa vile vitu vingi vinavyohitajika katika kuutangaza Uislamu vinahitaji kupata msaada wa fedha, hivyo nikiwa kama tabligh nikaona ulazima wa kukufahamisheni, kwa hiyo sikilizeni.......
Mosi, hakuna fedha kwa ajili ya mipango hiyo mikubwa, na hata kwa msaada wa baadhi ya watu wenye utashi wa dini sehemu ya kitabu ikachapishwa....ukiondoa nakala chake mno, kitabu hicho hakiuzwi, nakala nyingi zaidi ama zinafungiwa masandukuni kwa miaka mingi au zinagawanywa bure kwa ajili ya Allah... ingawaje Jumuiya inakuwa lakini bado hakuna mtu tajiri miongoni mwetu ambaye atabeba jukumu hili kubwa la kuitumikia dini. Na kwa kuwa mimi nimeteuliwa na Mungu kuhuisha dini ambapo Mungu amenipa habari njema kuwa atawajumuisha matajiri na wafalme katika jumuiya yangu....hivyo nikadhani nitawalingania baadhi ya matajiri na wenye hali bora kusaidia katika dini yangu... lakini kwa vile binadamu hawakosi kutuhumiana na kutiliana shaka na kufikiriana-fikiriana na bila kutambua kuaminiana nako kunashindwa kujengeka ambako ndiko kunakoleta ujasiri wa kufanya mambo makubwa, basi mimi natoa tangazo la jumla kwa Waheshimiwa wote kuwa kama wao wanasita kusaidia bila kupima (vipawa vyangu) basi wanitumie kwa maandishi matakwa yao, matatizo yao na shida zao, ili nami niwaombee dua watimiziwe matakwa yao, lakini waandike waziwazi kuwa pindi malengo yao yakifikiwa, je na wao watatoa msaada wa fedha kiasi gani na kwamba nyoyoni wametia nia thabiti na ya moja kwa moja kwamba kwa hakika watatoa msaada huo..." (Tangazo la Aprili 1893, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk. 387-389)
"Tangazo kuhusiana na kitabu 'Manan-ur-Rehman'........pia nimechapisha donge nono la Rs. 5000 pamoja na kitabu hiki.... hii itawekwa rehani mahali ambapo Arya au mtu mwingine yoyote ataridhika napo kabisa na ataelewa kuwa wakifanikiwa bila jitihada yoyote watapata fedha hizo.... lakini nao watoe kiapo cha maandishi kwa mtu atakayeweka rehani fedha hizo (yaani Mirza) kwamba baada ya yeye kuweka rehani Rs. 5000, mtu akiachana na shindano hili au akishindwa kutimiza majigambo yake, basi yeye ndiye atakayelipa gharama zote zinazoingiwa pale mtaji fulani wa biashara ukizuiliwa kwa kipindi fulani (Je Mirza hapa anataka riba juu ya kiasi hiki?-Rashid) (Tangazo la mwaka 1895, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.2 uk.134-137)

"Kitabu 'Sat Bachan' na 'Arya Dharam'.....bei ya vitabu vyote viwili ni Anna 6 ukijumlisha na gharama za utumaji." (Rs.1=Anna 16-Rashid) (Tangazo la tarehe 9, Septemba 1895,Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.2 uk.148)
"Kitabu 'Sat Bachan' na 'Arya Daram'.....kwa bei ya watu wa kawaida ni Rs. 1.50.....kwa watu wa hali ya juu...Rs. 5...." (Tangazo la Novemba 1895, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.2 uk.143).
"Vitabu vinne, 1.Anjam-i-Atham, 2.Khuda kaa Faislaa, 3.Daawat-i-Qaum Maktuub-i-Arabi ma'a Tarjuma Farsi.....bei Anna 8 ukijumlisha na gharama za utumaji." (Rs.1=Anna 16-Rashid) (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz. Uk 314)
"Kitab-ul-Bariyya......bei Rs.1 na anna 8 ukijumlisha na gharama za utumaji." (Rs.1=Anna 16-Rashid) (Tangazo la tarehe 5, Feb 1898, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3 uk.2)
***************************
CHANDA ya Jumuiya
Kwa hiyo, hali ikaendelea hivyo hivyo kwa miaka kadhaa. Mirza sasa akapata ufuasi mzuri na hakuridhika na maslahi madogo aliyokuwa akiyapata kutokana na vitabu vyake. Alitaka FUTUUHAAT zaidi. Akaanzisha mfumo wa MICHANGO (CHANDAS) ya mara kwa mara ya lazima kwa wafuasi wake, alihitaji harambee kwa ajili ya upanuzi wa nyumba yake, akahitaji harambee kwa ajili ya kujenga mnara na mengineyo mengi.
Chanda ya Msikiti
Moyoni mwangu kwa muda mrefu kulikuwa na wazo kuwa tukiweza kujenga nyumba katika kile kiwanja cha upande wa kulia wa msikiti huu na kuunganisha na msikiti....basi kwa kumwamini Allah mimi natoa taitolea tangazo sehemu hii ya msikiti na natumai kuwa kila jamaa na kila mwenye dhati atashiriki kusaidia nyumba ya Allah.....mwisho ifahamike kuwa makisio ya nyumba hii ni Rs 500." (Tangazo la tarehe 29, Julai 1898, Majmuu-e-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.2 uk.453).
Chanda kwa ajili ya Hazrat Molvi M Ahsan Saheb
"tunataka kuteua mhadhiri mmoja na washindani wa midahalo Bara Hindi yote....Kama Hazarati Molvi Mohammad Ahsan Saheb Amrohi akikubali, basi kazi hii atapewa yeye.....kila mtu mwenye kujiweza katika Jumuiya yangu kulingana na uwezo alionao ajipangie CHANDA ya kudumu kwa ajili ya masurufu yake...dunia ni makazi ya kupita tu ya siku chaches ambapo mtu ajiandae kwa amali njema kwa ajili ya Akhera." (Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1, uk. 323, tarehe 26 Mei 1892).
Chanda ya Minaret-ul-Masiih-Mei 1900
Baa la Njaa la India mwaka 1899-1900 (Imperial Gazetteer la India juz.III 1907 http://en.wikipedia.org/wiki/Indian famine of 1899†"1900) liliua watu milioni 1.25 hadi milioni 10. Lilianza kwa tatizo la majira ya kiangazi mnamo mwaka 1899 katika upande wa Magharibi na Katikati wa India ambapo, katika kipindi cha mwaka uliofuata, likaathiri eneo la maili za mraba 476,000 (sawa na kilometa 1,230,000) na idadi ya watu milioni 59.5. Njaa ilikuwa kali katika Majimbo ya Kati na Berar, Jimbo la Bombay, jimbo dogo la Ajmer-Merwara, na Wilaya ya Hissar ya Punjab; pia njaa hiyo ikasababisha dhiki kubwa katika Majimbo makubwa ya Rajputana Agency, Central India Agency, Hyderabad na Kathiawar Agency. Mbali na hayo, maeneo madogo-madogo ya Jimbo la Bengal, Jimbo la Madras na Majimbo ya Kaskazini-Magharibi nayo yaliathiriwa vibaya na baa hilo la njaa. Jamii za watu katika maeneo mengi ndio kwanza walikuwa wameponyeka-ponyeka na Baa hilo la njaa la Mwaka 1896 (http://en.wikipedia.org/wiki/Indian famine of 1896ậ??1897). Ilikuwa ni katika kipindi hiki ambapo watu walikuwa wanakufa njaa, Mtu huyu anayeitwa nabii wa Mungu bila kujali kabisa adha ya kushinda na njaa waliyokuwa nayo watu wengi, yeye akaanzisha changishachangisha (chanda) kwa ajili ya kujenga Minarat-ul-Masiih (Mnara wa Masihi), ikiwa ni jitihada ya kutumia bishara ya Mtume (saw) kujibashiri yeye mwenyewe.
...Imeamuliwa kuwa katika upande wa mashariki msikiti huu ujengwe mnara mrefu..” (Tangazo la tarehe 28 Mei 1900, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3 uk.283).
..mahali fulani pa juu ya ukuta wa mnara huu itawekwa taa kubwa ambayo itagharimu takriban Rs.100 au zaidi...” (Tangazo la tarehe 28 Mei 1900, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3uk.283).
.... saa kubwa itawekwa mahali pa juu ya ukuta wa mnara huu ambayo itagharimu, Rs.400 au 500....” (Tangazo la tarehe 28 Mei 1900. Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3 uk.383)
....gharama za Mnara huu wa Masihi hazitakuwa chini ya Rs.10,000. Sasa basi wale jamaa watakaosaidia ujenzi wake najuwa kwa hakika kuwa hao watakuwa wanaanya kazi kubwa.” (Tangazo la Mei 28, 1900, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3 uk.295)
Mwitiko wa tangazo hili haukuwa wa kutia moyo sana. Mirza akachapisha tangazo jingine mnamo Julai Mosi 1900 akiwahimiza wafuasi wake watiifu watoe zaidi Anatoa mano wa wachangiaji wawili wa jambo hili.
....mmoja wao ni Munshi Abdul Aziz...ambaye amechangia Rs.100 licha ya uwezo wake mdogo nami nadhani rupia hizi mia moja zilikuwa ni mdundulizo wa akiba yake ya miaka kadhaa na cha kupendeza zaidi ni kwamba ndio kwanza alitoka kuchangia jambo jingine na sasa bila kuijali familia yake katoa mchango huu.....” (Tangazo la Julai Mosi 1900, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3 uk.314)

.....mwingine mtiifu ambaye kaonesha utuuzima wake ni Mian Shadi Khan Lakree arosh....yeye ndio punde tu kachangia Rupia 150 kwa ajili ya jambo moja hivi na sasa katuma mchango wa Rupia 200 kwa ajili jambo hili......ukizitazama mali zote hizi basi hazitakuwa zaidi ya Rupia 50.....akaandika katika barua yake kwamba: haya ni masiku ya baa la njaa na biashara ya vitabu dunia inaonekana kudorora....” (Tangazo la tarehe Mosi Julai 1900. Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3 uk.315).



Mchango wa Upanuzi wa Nyumba-Mchango wa Tauni-Tauni Inakuja!-1902
Kwa mujibu wa Historia ya Tiba ya India ya Mwingereza (http://www.nls.uk/indiapapers/plague.html) ingawaje kuna rejea za maradhi yanayofanana na Tauni ya mtoki mnamo karne za 17 na 19, ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kukubalika rasmi kuwa kuna tauni ya mtoki hadi mwaka 1896. Yumkini tauni hii iliingia nchini kutoka Hong Kong, ambako mlipuko ulikuwa umepamba moto tangia mwaka 1894. Athari zake za mwanzo ziliishia kwenye miji ya bandari, hususan Bombay, lakini baadae zikaenea hadi Pune, Calcutta na Karachi. Hadi kufikia mwaka 1899, ugonjwa huo ukaonekana katika miji mingi midogo na ukawa na athari shamirishi za eneo kwa eneo kwani ulisambaa hadi pembezoni mwa nchi. Athari za kijamii za milipuko ya tauni zilionekana zaidi India magharibi na Kaskazini katika majimbo ya Bombay, Punjab na Majimbo yaliyoungana. India mashariki na kusini hakukuathirika sana. Mjini Punjab pekee ndani ya kipindi cha mwaka 1 kuanzia Oktoba Mosi 1901 hadi Septemba 30 1902 kati ya wagonjwa 318,933 wa Tauni, wagonjwa 220,389 walifariki dunia. (Ripoti ya Tauni Punjab kunzia Oktoba Mosi 1901 hadi Septemba 30 1902 iliyoandaliwa na Major E. Wilkinson, Afisa Mkuu wa Magonjwa ya Tauni, Punjab)
Mirza Ghulam akiwa mtu wa maslahi namna hiyo, kwa mara nyingine, akaona hii ni fursa adhimu ya kutumia hali hiyo. Akaanza kusema kuwa tayari alikwishachapisha bishara kuhusu Tauni katika Brahiin-i-Ahmadiyya miaka ishirini iliyopita. Akitumia hofu kama kama silaha akajaribu kuitilia mkazo hadhi yake aliyopewa kwa amri ya Mungu na akainasibisha Tauni hiyo na ukaidi wa kumkataa yeye kama ni nabii wa Mungu. Alidai kuwa ambao watamkubali yeye watakinbgwa na tauni na kwamba Mungu ameahidi kuikinga Qadian na hasa hasa nyumba yake dhidi ya ugonjwa huo. Kwa kisingizio hiki, akatangaza mchango (CHANDA) wa kupanua nyuma yake. Je Mirza aliitumai ahadi ya Mungu na je aliikinga Kadiani na na watu ndani ya nyumba yake? Je alifanya nini pale wagonjwa walipoonekana ndani ya nyumba yake. Maelezo kuhusu kadhia nzima ya Tauni yanatolewa katika makala nyingine (http://alhafeez.org/rashid/fatwa 27.html), hapa nataka kuonesha jinsi Mirza alivyolitumia jambo hili kwa manufaa yake.
Mirza aliomba dua ya Tauni:
Niliomba isambae tauni. Basi dua ikajibiwa na tauni ikaenea nchi nzima.” (Haqiiqat-ul-Wahi, Roohani Khazain juz.22 uk.235) (Na bado akadai kuwa yeye alitumwa awe Rehema kwa walimwengu wote!)
Mirza alipokea Wahyi kuhusu Tauni
....habari hii ya tauni nayo pia ilichapishwa miaka 22 iliyopita katik Brahiin Ahmadiyya.” (Dafe-al-Bala, Roohani Khazain juz.18 uk.226)
“wahyi wa Mungu ulionishukia mimi....ni kwamba Mungu kaamua kuwa katu Hataindosha adhabu hii mpaka watu waondokane na yale mambo yaliyomo ndani ya nyoyo zao kwamba kama hawamkubali yule ambaye kateuliwa na Mungu na Mtume Wake, basi tauni haitaondoshwa.” (Dafe-al-Bala, tarehe ya uchapishaji ni Aprili 1902, Roohani Khazain juz.18 uk.225-226).
Sababu ya Tauni hii
Kwa nini Punjab ndiyo inayokabiliwa na mlipuko wa Tanu? Kwa mtazamo wetu moja ya sababu ni kwamba Mungu kaanzisha Jumuiya hapa, ambapo hawa ndio walikuwa watu wa kwanza kabisa kukanusha na kutoa Fatwa ya kufuru”. (Malfuuzaat ya Mirza juz.3 uk.419).
Ni Watu wa Nyumba ya Mirza tu-Jahazi la Nuhu ndio watakaonusurika
Qur’an yatuambia kuwa pale mtoto wa Nuhu alipoanza kuzama katika mafuriko, Nuhu akamsihi njoo; yeye akasema sina shida yoyote ya kuja kwako, nitapanda mlima huu. Kwa maneno mengine, mpumbavu huyo alitaka kujinusuru kwa uwezo na njia zake mwenyewe, lakini Mungu akasema leo hakuna mtu atakayekunusuru na Mungu. Vivyo hivyo katika wahyi wangu inaelezwa kuwa: ‘unda meli Mbele ya Machoi Yetu na kwa wahyi wetu, na usiniombe chochote kwa niaba ya wale waliotenda dhambi, kwa hakika wao ni watu wa kuzamishwa. Na kwa ajili ya msikiti huu wenye baraka (njini Qadian) (Mungu) kasema: ‘na yeyote aingiaye humo yupo katika amani.’ Haya yanathibitisha kuwa dhoruba kubwa iko mbioni kutokea ambapo watakaonusurika ni wale tu watakaopanda jahazi langu...na dhoruba yenyewe ni Tauni.” (Malfuuzaat juz.3 uk.418).
Rupia 2000 zahitajika kwa ajili ya kupanua jahazi la Mirza
Kwa kuwa inelekea kabisa kuwa huko mbele tauni itasambaa nchini na nyumba yetu...nyumba yetu imekuwa na msongamano sana nanyi watu mmesikia Mungu katoa ahadi ya hifadhi maalum kwa yeyote atakayekuwa ndani ya mpaka wa nyumba hii...kwa rai yangu jumba hili linaweza kukamilika kwa Rupia 2000 (ambayo kwa thamani ya leo ni mamilioni ya rupia). Kwa vile inaelekea kuwa muda wa kuja tauni unakaribia na kwa mujibu wa habari njema za kufunuliwa, katika dhoruba hii ya tauni, nyumba hii itakuwa kama Jahazi la Nuhu, sijui nani atakayekuwemo katika ahadi hii ya habari njema, kwa hiyo kazi hii (ya kupanua nyumba ya Mirza) ini ya haraka. Mtawakali kwa Mungu ambaye ndiye Muumba na Mwenye kuruzuku na ndiye atazamaye amali njema, nanyi jitahidini. Nimeona kuwa ijapokuwa nyumba yangu hii inafanana na JAHAZI lakini kwa baadae hamna nafasi kwa mtu yeypte mwanaume au mwanamke na ndiyo sababu kuna haja ya kufanya upanuzi.” (Kishtee-i-Nuhu publication tarehe 5 Oktoba 1902, Roohani Khazain juz.19 uk.86)

Qadiani yakingwa kwa sababu ya nabii wa Mungu-Mirza Qadiani
Na kwamba MwenyeziMungu ataikinga Qadian na maangamizi ya tTauni, ili mfahamu kuwa Qadian inakingwa kwa sababu tu nabii na mtume wa Mungu yupo kule Qadian. Sasa hebu ona kuwa jambo hili linathibitika katika miaka mitatu ya mwisho kwamba mambo yote haya mawili yametimia; yaani kwa upande mmoja tauni likuwa imesambaa Punjab kote na kwa upande mwingine licha ya kwamba tauni imeenea ndani ya maili mbili za Qadian lakini bado Qadian ikasalimika na tauni, badala yake hadi leo mtu yeyote aliambukizwa tauni ambaye kaingia Qadian akitokea nje, naye pia hupona. Je kwaweza kuwa na ushahidi mwingine zaidi? Mambo yaliyotangulia kusemwa awli, yametimia, bali habari hii ya tauni pia ilichapishwa miaka 22 iliyopita katika Brahiin Ahmadiyya.” (Dafe-al-Bala, Roohani Khazain juz. 18 uk.225-226)
Sasa kutokana na ufunuo wote huu, mambo matatu yanathibitika: 1) Mosi tauni hiyo imekuja duniani kwa sababu Masihi aliyeahidiwa na Mungu si tu alikataliwa bali pia alipewa maumivu. ... 2) jambo la pili ambalo linathibitishwa na wahyi huu ni kwamba tauni hii itatoweka pale tu watu watakapomkubali mtume huyu wa Mungu ....3) Jambo la tatu ambalo linathibitishwa na wahayi huu ni kwamba Mungu kwa hali yoyote ile ataikinga Qadian na maangamizi haya ya kutisha muda wa kuwa tauni inabakia katika dunia hii, hata kwa miaka 70, kwa sababu hapa ni mahala penye kiti cha cha Mtume Wake na ni ishara kwa walimwengu wote.” (Dafe-al-Bala, Roohani Khazain juz.18 uk.229-230)
Mungu hayuko kama hivyo kwamba atawaadhibu watu mjini Qadian ilihali nyinyi mnaishi miongoni mwao. Atakikinga kijiji hiki na madhila na maangamizi ya tauni. Kama nisingekuwa na huruma nanyi na kama nisingekuwa na heshima kwenu, ningekiangamiza kijiji hiki.” (Ufunuo wa Mirza, Tazkirah uk.436;Roohani Khazain juz.18 uk.227)
Kama nisingelijali heshima yenu, ningekiangamiza kijiji hiki. Nitamnusuru kila mmoja ndani ya mipaka ya nyumba hii. Hakuna mtu miongoni mwao atakayekufa kwa tauni au tetemeko la ardhi. Mungu hayuko hivyo kwamba awaawadhibu huku nyinyi mkiwa miongoni mwako (Wahyi wa Mirza, Tazkirah uk.645)
Wakati moto wa tauni unapamba, je kuna mzushi yeyote anayeweza kusema kuwa ‘Kama nisingejali heshima yenu, ningekiangamiza kijiji hiki.’ Je isingewezekana kuwa huyu mzushi na yeye angekufa na kuwa muhanga wa tauni? Hivi sasa Qadian ni kama Maka, humo watu wanakufa wakiizunguuka na kwa Rehema za Mungu papa hapa ndipo penye amani kamili.” (Makhtoobaat-i-Ahmadiyya juz.5 uk.369)
Ooo!! Mungu kaamua kumvunjia heshima huyu aliyeitwa nabii
Licha ya madai yote haya yaliyotolewa na Mirza na huo unaoitwa wahyi wake, MwenyeziMungu akaamua kumdhalilisha mzushi huyu wa unabii. Si tu wale waliomkubali walikumbwa na tauni, bali hata wale waliokuwa wakiishi kwenye hifadhi salama ya Qadian na Jahazi la Mirza nao pia walipata ugonjwa huo.
Na halafu wakati wa masiku ya Tauni, wakati tauni ilipokuwa inapamba moto kule Qadiani, mwanangu Shariif Ahmad akawa mgonjwa, alipata homa kali ambayo ilisababisha mwanangu apoteze fahamu, na akaanza kuwa na kifafa katika hali hiyo ya kutojitambua.” (Haqiiqat-ul-Wahi-Ukweli kuhusu Wahyi, Roohani Khazain juz.22 uk.87 tanbihi)
Kipenzi changu Mpendwa Nawab Sahed.....nina huzuni baada ya kusoma kuwa Abdur Rahman Khan kapata tena homa. Namuomba Mungu ampe ponyo. ....mahali hapa tauni inasambaa vibaya. Mtu anapata homa na ndani ya saa chache anakufa. Mungu ndiye anayejua zaidi lini adha hii itakwisha. Umma unatishika mno. Matumaini ya kuishi yametoweka. Mayowe na vilio vinatokea pande zote. Ni maangamizi huku na kule. Sasa nisemeje, nitoe ushauri gani? Nachanganyikiwa sijui hata nifanyeje.” (Makhtuubaat-i-Ahmadiyya juz.5 Na.4 Barua Na.36 uk 112)
Hapa Qadiani, siku hizi tauni inaendelea kupamba moto. Karibu vijiji yote vinavyoizunguuka vimetoweka.” (Maktuubaat-i-Ahmadiyya juz. 5 Na.4 Barua Na. 36 uk 112-115)
Leo mtoto wa Mian Mohammed Fazal, mhariri wa gazeti, naye yuko katika kitanda cha sakarati-mauti, yeye ana tauni ya mapafu, inaonekana kuwa ndio anapumua pumzi ya mwisho. Kuna vilio kila mahali. Tunamuomba Mungu atupe Rehema Zake.” (Maktuubaat-i-Ahmadiyya juz.5 Na.4 Barua Na.53 uk.131)
Bwana wangu, Mheshimiwa Ndugu yangu Seth Saheb! (SubHanAllah! Eti Seth-Afisa wa fedha-naye ni Bwana wa Mirza!!!-Rashid)......Napata wasiwasi na kutatizika mno. Mungu akunusuruni na misiba. Hapa tauni inaendelea kucharuka kiasi kwamba inakuwa kama vile mwisho wa dunia.” (Maktuubaat-i-Ahmadiyyah juz.5 Na.1 Barua Na.91 uk.39)

Tauni imecharuka sana katika eneo hili, nimesikia kuwa tukio moja au mawili yalitokea kule Amritsar pia. Siku chache nyuma na mimi nilipata tezi mwilini mwangu, mwanzoni dalili fulani mbaya zilionekana. Lakini kwa Rehema za Mungu, makali yakapungua. Kisha katika mkono mwingine matezi yakatutumka. Tauni hii huathiri maungio ya viungo. Hivyo matezi fulani huonekana nyuma ya masikio au kinenani au kwapani au kwenye maungio kama vile ya mikono au miguu sanjari na homa.” (Maktuubaat-i-Ahmadiyya juz.5 Na.4 Barua Na 38 uk. 115)


Bwana wangu, Ndugu yangu Seth Saheb......hapa tauni imesambaa. Kwa sasa kuna vijiji 80 ambavyo vina dhahama kubwa. Ndani ya Qadian hali ya mambo ndiyo hii kwamba wavulana na vijana na wazee hupata homa ndogondogo, kisha siku inayofuata hupata matezi chini ya masikio, chini ya makwapa au kwenye kinena. Mimi pia nilipata tezi moja; awali pia nilipata tezi moja na mwanangu Bashiir Ahmad naye alipata homa siku moja na kisha akapata tezi mbele ya masikio. Mkwewe Molvi Sahib Hakiim Nuruddin Sahib naye alipata tezi chini ya kwapa, mtoto wa kiume wa Mir Nasir Nawab, Ishaq naye alipata mtoki kwenye kinena baada ya homa.”

(Maktuubaat-i-Ahmadiyya juz.5 Na.1 Barua Na.40 uk.15)
Mnamo Aprili 1904 Shule moja Ahmadiyya mjini Qadian ilifungwa kutokana na Tauni na katika Taaria Rasmi ya Kila siku (Taz. Ahle Hadith Newspaper la tarehe 27,Mei 1904) idadi ya vifo kwa miezi Machi na Aprili 1904 ilirekodiwa kufikia 1313 ambavyo vilitokea Qadian. Enzi hizo idadi ya watu wa Qadian ilikuwa ni 2800. Watu wakapata kihoro na kukihama kijiji ambapo mji mzima ulionekana kutelekezwa.” (Hur-i-Mehremana iliyoandikwa na Ghulam Jeelani Barq uk. 251-252).
Mwenendo wa Nabii wa Qadian wakati wa Kadhia

Na pale mtu ulani ndani ya hili lililoitwa Jahazi la Nuhu alipopata tauni, mwenendo gani aliokuwa nao huyu aliyetwa nabii?


Bi mkubwa Ghausan alipata homa. Akafukuzwa nyumbani, lakini mimi nadhani haugui Tauni, ni hatua ya tahadhari tu yeye kufukuzwa. Bwana Muhammed Deen naye alipata homa, tezi mtoki ukavimba. Naye pia kafukuzwa nyumbani. Basi tena hapa petu napo tauni imeanza kucharuka.” (Maktuubaat-i-Ahmadiyya juz.5 Na.4 Barua Na.38 uk.115)
1   2   3   4   5


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət