Ana səhifə

Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahiim Harakati za Uislamu dhidi ya Ahmadiya Chungu Mosi, Rabiul Awwal 1430 Februari 24, 2009


Yüklə 0.51 Mb.
səhifə3/5
tarix26.06.2016
ölçüsü0.51 Mb.
1   2   3   4   5

Hata hivyo Mirza akapata kile alichokitaka. Aliweza kupanua nyumba yake. Hakuona haya kuwa ahadi zake na funuo zake ziligeuka uongo mtupu badala yake akatoa visingizio vizivyokuwa na maana.
Akiwa ameomba kuja kwa Tauni, Mirza alifurahia matokeo:
Ni kheri kuwa Mungu ndiye aliyeshusha Tauni katika dunia hii ili tustawi na kumea na ili maadui zetu waangamie na kutoweka.” (Haqiiqat-ul-Wahi, Roohani Khazain juz. 22 uk.570)
Kila mwezi angalau watu 500 na wakati mwingine watu 1000 au 2000 huingia katika Jumuiya yetu kutokana na Tauni. Hivyo, kwetu sisi Tauni ni Rehema na kwa maadui zetu ni taabu na adhabu. Na kama (makali) hayo ya Tauni yakiendelea katika nchi hii kwa miaka 15, basi naamini kuwa nchi nzima itajaa Jumuiya ya Ahmadiyya.” (Haqiiqat-ul-Wahi, Roohani Khazain juz.22 uk.568-570)
Eti bado tu Jumuiya ya Ahmadiyya inapaza kauli mbiu ya ‘Upendo kwa wote, Hapana Chuki kwa yeyote’. Huu kama si unafiki, ni kitu gani!!
Michango (Chanda) Mingine Zaidi
Ndiyo kusema kuwa utaratibu wa kuchomoana fedha ndio uliobuniwa na Mirza Ghulam Ahmad Qadian kwa jina la Mungu na isingefaa kuiita hii kuwa ni harambee ya Jumuiya (Jamaat-i-Chanda). Kinachoifanya hii iwe chomoa-chomoa ni ule ukweli kuwa mchango huu ulikusanywa kwa kisingizio cha ‘fii sabiil Allah’-kwa ajili ya njia ya MwenyeziMungu, lakini sehemu ya mchango huu ilitumika kwa manufaa binafsi. Tutasoma ushahidi wa hilo huko mbele katika kitabu hiki lakini kwanza hebu tuone kile alichoandika Mirza kuhusiana na changishachangisha (Chanda) hii:
.. Tangazo hili si andiko la kawaida. Bali hii ndiyo hukumu yangu ya mwisho kwa wale wanaoitwa muriidi (wafuasi) wangu. Mungu kaniambia kuwa uhusiano wangu uwe na hao tu, yaani wao ndio walioandikwa kuwa ni wafuasi wangu katika kitabu cha Mungu, ambao hushughulika katika kutoa usaidizi na msaada.....hivyo, baada ya utaratibu huu mpya kila mmoja anapaswa kula kiapo na atoe taarifa kwa maandishi maalum kwamba, kwa shurti anaweza kutoa kiasi kikubwa cha MCHANGO wa mwezi, na pasiwe na majigambo.....” (Tangazo la tarehe 5 Machi 1902, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk.468-469)
Yeyote ambaye ni mfuasi wangu, anapaswa kutenga kiasi fulani kwa mwezi, hata paisa 1 au dhaila 1 na yule asiyetenga chochote na asiyetoa msaada wa kiwiliwili kwa jumuiya hii, huyo ni mnafiki na basi hataweza kubakia katika jumuiya hii.” (Tangazo la tarehe 5 Machi 1902, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo juz.3 uk.469)
(Nita)subiri jibu kutoka kwa kila mfuasi kwa miezi 3 baada ya kuchapisha tangazo hili kwamba ni kiasi gani cha mchango wa mwezi (chanda) katenga kwa ajili ya kusaidia jumuiya hii na kama hakuna jibu litakalopokelewa ndani ya miezi 3, jina lake litafutiliwa mbali katika baith..” (Tangazo la tarehe 5 Machi 1902, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk.469)
..na baada ya kula kiapo cha kutoa chanda ya kila mwezi, mtu yeyote akizembea kwa miezi 3 kutuma chanda (mchango), naye pia jina lake litafutiliwa mbali na baada ya hapo mtu mzembe na jeuri asiyeingia Ansar (kundi la wasaidiaji) kamwe hatakaa katika jumuiya hii.” (Tangazo la tarehe 5 Machi 1902, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk.469)

Watu wanapaswa kuisaidia jumuiya hii kwa kila njia. Na pasiwepo na uzembe katika kuihudumia kifedha. Zingatieni, hakuna jumuiya inayostawi bila michango (chanda) katika dunia hii.....Watu hawa wakitoa paisa1 mara kwa mara kila mwaka basi mambo mengi yanaweza kufanyika, lakini kama hachangii hata paisa 1 basi kwa nini abakie katika Jumuiya.” (Malfuuzaat juz.6 uk.38 tarehe 5 Julai 1903)


Kila siku mamia wanakula kiapo (kiapo cha utii) lakini baada ya kuchunguza ni wachache sana wanaotoa chanda ya mara kwa mara kila mwezi. Yule asiyeisaidia jumuiya hii kulingana na nafasi aliyonayo ya kifedha nini basi kingine kinachoweza kutarajiwa kwake? Na nini manufaa ya kuwemo kwake katika jumuiya?” (Malfuuzaat juz.6 uk.39 ya tarehe 5 Julai 1903)
Kama mtu anakula mikate 4, akiweka nusu mkate (kwa ajili ya jumuiya) basi huyo kaweza kutimiza kiapo chake.” (Malfuuzaat juz.6 uk.40 ya tarehe 5 Julai 1903)
Safari hii wakati wa safari kubwa ya Tabligh daftari lazima nalo lichukuliwe safarini, pale ambapo mtu yeyote anataka kula kiapo cha utii, jina na kiapo chake cha mchango (chanda) viorodheshwe. Kila mtu ale kiapo kuwa atatoa chanda hii kubwa kwa ajili ya madarsa na atatoa chanda hii kubwa kwa ajili ya jikoni.” (Malfuuzaat vol.6 uk.41 ya tarehe 5 Julai 1903)
Sheikh Raheel Ahmad ambaye zamani alikuwa ahmadiya wa kuzaliwa kutoka Ujerumani, aliita hii kuwa ni Kodi ya Jagga.
Kuna aina tofauti 35 hadi 50 za CHANDA ambazo Jumuiya hudai wafuasi wao watoe ambapo Ahmadiya wote wanaifahamu kwa hiyo hakuna haja ya kutoa rejea zozote. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya michango hiyo:
. CHANDA AAM, Ni wajibu kwa kila Ahmadia kutoa asilimia 6 ya kipato chake ukiwa ni mchango yaani Chanda Aam. Yeyote anayekosa kufanya hili, salio lake huoneshwa katika akaunti yake na akikataa kutoa, basi anakoma kuwa Ahmadia na hutupwa nje ya Jumuiya.
. CHANDA JALSA SALANA

.CHANDA TEHREEK JADEED. Kila Ahmadia mwanaume, mwanamke, kijana, mzee, mtoto hujumuishwa. Jumuiya husisitiza mno kuwa kila mtu aliye hai anapaswa kujumuishwa katika Tehreek Jadeed, hata baadhi ya wafu nao hujumuishwa katika changiachangia hii, hii ikiwa na maana kuwa kwa niaba ya watu waliokufa, mchango (chanda) huchukuliwa kutoka kwa ndugu zao.

. CHANDA WAQF JADEED

. CHANDA SAD SALA JUBILEE

. CHANDA KHUDDAMUL AHMADIYYA (CHANDA MAJLIS) ambayo inawahusu vijana.

. CHANDA TAMIIR HALL (Ukumbi huu ulijengwa mwaka 1973 lakini kusanya-kusanya ya michango bado inaendelea)

.CHANDA BOSNIA

.CHANDA AFRIKA

.CHANDA YA ANTENA YA DISHI (Mtandao wa TV wa Ahmadiya)

.CHANDA LAJNA AMA’ALLA (huu ni mchango unaowahusu wanawake)

.CHANDA AFTAAL (huu unawahusu watoto)

.CHANDA ANSAAR (huu unawahusu watu wanaovuka miaka 40)
Orodha hii inaendelea. Kila wakati huwa kuna wito wa kuchangia mradi na hapo Chanda (changishachangisha) huanza. Ahmadia mmoja wa zamani, Profesa wa Fizikia, Munawwar Ahmad Malik, kaandika hivi:
Katika Jumuiya, kuna msisitizo mkubwa wa michango. Chanda Aam ni ule mchango wa msingi ambao hutolewa na kila mtu mwenye kipato (badala yake sasa mchango huu umekuwa wajibu hata kwa watu wasioajiriwa). Ulipaji wake ni wa kulazimisha. Kila mtu aliyeajiriwa lazima atoe aslimia 6.25 ya mshahara wake ikiwa ni Chanda Aam. Kwa mwaka mzima, akili ya wanajumuiya huelekezwa kwenye jambo hili. Mara mbili tatu kwa mwaka wakaguzi huja kutoka kituoni na kuhakikisha makusanyo ya asilimia 100 ya mchango huu. Ili kufanikisha makusanyo yake, motisha za kidini hutolewa, kwamba wale watakaotoa malipo ya asilimia 100, majina yao yatapelekwa kwa ‘Huzuur’ (Mirza Tahir Ahmad Qadiani) kwa ajili ya kuombewa dua, na kwamba kwa nyakati fulani-fulani majina ya wanajumuiya hao pia yatakuwa yakitajwa-tajwa na kadhalika na kadhalika. Kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha, viongozi wa Jumuiya hutoa hotuba kadhaa juu ya umuhimu wa Mchango huu na hutilia mkazo makusanyo yake ambapo mwishoni mwa mwaka, maelezo ya mchango hutolewa,. Maelezo ya ahadi na bejeti ijayo hutangazwa.
Juu ya kila mtu awe kaajiriwa au hakuajiriwa, mchango wa ‘Tehreek Jadid’ ni lazima. Huko nyuma ulikuwa ni mchango wa hiyari, lakini sasa kidogokidogo ukawa wa lazima. Ili kupata makusanyo ya asilimia 100 ya Chanda Tahreek Jadid, wakaguzi mbalimbali huja kutoka kituoni, viongozi nao hutoa hotuba mbalimbali na mtandao mzima wa jumuiya huwa katika pilikapilika za kukusanya mchango huu.
‘Chanda Salana’ nayo pia ni mchango wa lazima ambao hukusanywa kwa mwaka kwa kiwango cha asilimia 10 ya kipato cha mwezi. Kwa ajili ya kusisitiza mchango huu pia hotuba maalum hutolewa. ‘Waqf Jadid’ nao pia ulianzishwa kama mchango wa hiyari lakini nao sasa ukaanza kuwa mchango wa lazima. Wakaguzi wa michango iliyotajwa hapo juu huja kutoka kituoni mara tatu kwa mwaka kuhakiki makusanyo ya michango. Wale ambao malimbikizo ya michango hii yanadaiwa kwao, wakaguzi huwaendea hadi majumbani mwao kukusanya michango hiyo.
Mbali na michango hii, kuna Michango Mingine (Chanda):
Mathalani kwa vijana (khuddam-ul-Ahmadiyya) kuna Chanda Majlis, Chanda Ta’amiir Hall, Chanda Ijtama’a; kwa watu wazima (Ansarullah), kuna Chanda Bosnia, Chanda Afrika n.k. Chanda ya Miaka 100 ya Jubelee ilikusanywa kwa miaka 16.
Ahmadia mmoja ambaye mshahara wake ni Rupia 3000 kwa mwezi, hulazimika kutoa angalau Rupia 300 kwa mwezi katika michango hii. Iwapo mkewe, wanawe na wazazi wako pamoja naye, basi malipo yao huchukuliwa kutoka kwenye mshahara huo huo. Ndiyo kusema mtu huyu hulazimika kulipa kati ya Rupia 300 hadi 500 kila mwezi. Asipotoa, basi italimbikizwa kwenye hesabu yake kiasi kwamba mwishoni wa mwaka atakuwa na deni la kati ya Rupia 3000 hadi 4000. Halikadhalika kama mtu anaingiza Rupia 10,000 kwa mwezi, basi kwa mwaka, hulazimika kutoa zaidi ya Rupia 12,000.”

(Prof. M A Malik on http://www.ahmedi.org/eart/ThoseWhoQuit?page=4)
Kwa kifupi, Ahmadia mmoja hulazimika kutoa takriban asilimia 10 ya mapato yake kila mwezi. Kuna utaratibu wa hiyari wa kukusanya Michango ambapo mkusanyaji hapati kamisheni (posho) yoyote. Hailekei kama kila mahali utaratibu wa aina hii utakuwepo. Mara mbili tatu kwa mwaka wakaguzi tofauti wa Michango (Chanda) mbalimbali huja kutoka kituoni kukagua mahesabu na kuhakikisha kuwa kiasi kinachopatikana kinapelekwa kituoni (Chanabnagar-Rabwah). Kwa sababu ya utaratibu huu pesa, Jumuiya inadaiwa kuwa ni Jumuiya imara, japo hakuna mfumo, hakuna sheria wala hakuna taratibu na wala hakuna kanuni. Uliopo ni utaratibu tu wa kukusanya michango. Lau kusingelikuwa na ukusanyaji madhubuti wa MICHANGO (CHANDA), basi leo hii familia ya WARITHI wa MIRZA SAHIB wasingemiliki miraba ya ardhi (kwa makisio muraba mmoja = ekari 25) wala wasingeishi maisha ya anasa na fahari.” (5 Million Baiths in 1999!What are the facts? Imeandikwa na Prof. M.A. Malik http://alhafeez.org/rashid/figures2.htm)

Si ajabu kuwa mgeni aliyeingia Ahmadiyya alimwambia Murabi/ Mubaligh wa Ahmadya mjini Cairo hivi:


....”Ustadh! Wewe ni Abul Ata (mtoaji) lakini mbona mara kwa mara unatukarahisha na MICHANGO (CHANDAS). Kwa nini basi usibadili jina lako liwe Abul Akhaz (mchukuaji)?” (Al-furqan, Rabwah, Juni 1971 uk.25-26 Alfazl International vol.15. no.46 tarehe 14 Nov.2008)
Mchango wa Eneo la Makaburi ya Peponi-Wasseyat System-1905
Mnamo Desemba 24, 1905, Mirza Ghulam Ahmad Qadiani (MGAQ) alichapisha kitini, Al-Wasiiyat, ambamo alitangaza kuanzisha eneo la Makaburi ya Peponi kwa kufuata maagizo ya Mungu na akaweka masharti kadha wa kadha ya kuzikwa katika eneo hili. Ingawaje aliandika kuwa lengo la eneo hili la makaburi ni kuwa wafuasi wake wa dhati na wema ndio watakaozikwa katika eneo hilo, lakini kwa kweli hiki kikawa kisingizio kingine cha kukusanyia MICHANGO (CHANDA). Yeye na familia yake wakajitoa katika masharti hayo hii ikiwa na maana ya kujitoa katika wema na katika kuchangia CHANDA!!! Sharti la kwanza lilikuwa ni kutoa MCHANGO (CHANDA) na kuwa kile kinachitwa MUSI!!!
Sharti la kwanza ni kwamba kila mtu anayetaka kuzikwa kwenye makaburi haya, kulingana na hadhi yake, anapaswa kutoa MCHANGO (CHANDA) kwa ajili ya gharama hizi.......Sharti la pili ni kwamba kutoka ndani ya Jumuiya nzima, atakayezikwa katika makaburi haya ni yule tu ambaye anayetia nia kuwa baada ya kifo chake asilimia 10 ya mali zake zote itatumika kwa ajili ya tabligh ya Uislamu yaJumuiya hii.....” (Al-Wasiiyat tarehe 20 Desemba 1905, Roohani Khazain juz.20 uk.218-319).
Mungu kanifanyia udhuru mimi na familia yangu, na kila mtu mwanaume au mwanamke hana budi kufuata masharti haya na yeyote anayenung’unika huyo atakuwa mnafiki.” (Al-Wasiiyat tarehe 20 Desemba 1905, Roohani Khazain juz.20 uk.327)
Majuma machache baadae kukawa na ufafanuzi wa ziada katika Wasiyaat yake: :
Wamiliki wa mashamba wa Punjab ambao wanakabiliwa na hali ngumu katika kutoa Wosia, ni heri zaidi kwao kwamba mali yoyote wanayotaka kurithisha , badala ya kuitolea Wosia, waitoe wakfu wangali hai....na katika mazingira hayo, wafanye hivyo hivyo tena na tena kwa mali nyinginezo wazichumazo.” (Al-Wasiyaat tarehe 29 Januari 1906, Roohani Khazain juz.20 uk.331)

......iwapo kuna tatizo fulani katika kuitoa wakfu mali hiyo, basi mali yoyote wanayotaka kurithisha au kutoa hidaya, baada ya kuipangia bei ya soko mali hiyo au baada ya kuiuza, wakabidhi fungu kwa Kamati Tendaji (Anjuman). Lakini katika mazingira hayo, wanapopata mali nyingine, basi wafanye hivyo tena na tena.” (Al-Wasiiyat tarehe 29 Januari 1906, Roohani Khazain juz.20 uk.331).


Yule asiyemiliki mali yoyote lakini ana njia nyingine ya mapato, basi watoe angalau asilimia 10 ya mapato yao kwa mwezi katika Kamati.....lakini watoe Wosia kuwa baada ya kufa kwao kamati itakuwa mmiliki wa asilimia 10 wa chochote wakiachacho nyuma yao.” (Al-Wasiiyat tarehe 29 Januari 1906, Roohani Khazain juz.20 uk.332)

Hivyo akaanzisha mfumo wa Wasia ambao kwa kurithishana vizazi na vizazi vya Makhalifa, ndio umekuwa chanzo kizuri cha mapato kwa familia ya Kuu ya akina Mirza. Kwa msingi wa maagizo /funuo za Mungu, eneo la Makaburi ya peponi likatengwa kule Kadiani lakini sasa kuna eneo la Makaburi ya Peponi kule Rabwa Pakistan. Musis wametawanyika dunia kote, iwe maiti zao zinapelekwa Kadiani au la, nani anayeweza kusema. Maiti huwa hazirudi tena kuja kuleta malalamiko yao. Lakini jambo moja ni la hakika. Punde baada ya kufariki dunia kwa MUSI, Kamati (Anjuman) iliyopewa jukumu la usimamizi wa Fedha huchukua mali za mtu huyo aliyefariki dunia. Katika kila hadhara Ahmadia huhimizwa wawe MUSI. Mapesa yote hukusanywa na hivyo kurundikwa kwenye mikoba ya Khalifa.


Ili kukupatia japo dokezo tu la jinsi utaratibu huu ulivyokuwa mbaya na kile kinachotokea hivi sasa, barua ya hivi karibuni kutoka kwa Ahmadia mmoja wa mjini Hamburg, nchini Ujerumani, anakaririwa hapa katika mtandao wa courtesy of Ahmedi.org (http://www.ahmedi.org/article/urdu/wassiyyat.php):
“..mkasa huu una zaidi ya miaka 50-60. Mmoja wa ndugu zangu wakubwa wa kike, Maryam Begum, alitoa wasiiyat (akawa MUSI). Yeye alikuwa akiishi katika kijiji kimoja kidogo. Kulikuwa na ugomvi kati ya akina mama fulani juu ya mambo fulani madogo-madogo ambapo mama mmoja alimlalamikia ndugu yangu huyo mkubwa wa kike. Idara ya Waasiyat ikaweka malalamiko haya kwenye jalada, lakini bado ikaendelea kupokea CHANDA ya kila mwezi kwa ajili ya WASIIYAT. Takribani miaka 50 baadae akafariki dunia. Pale alipoletwa Rabwa kwa ajili ya maziko, jalada lake likafunuliwa na barua ikakutikana humo, nao wakasema mwanamke huyo hawezi kuzikwa katika Makaburi ya Peponi. Walipoulizwa sababu, wakasema Barua ni ya Zamani......Mimi namuuliza Khalifa Sahib Mirza Masroor Sahib kwa heshima kuwa wakati barua ilipowekwa kwenye faili la mwanamke huyo miaka 50 iliyopita, halikuwa jukumu la Idara ya Wasiiyat kumwambia mwanamke huyo, lakini wao hawakufanya na wakaendelea kupokea CHANDA WASIIYAT. Mwanamke huyu alikuwa ni Ahmadia wa dhati kabisa. Mchango wake haukurejeshwa wala yeye mwenyewe hakuweza kuzikwa kwenye Makaburi ya Peponi. Watoto wake walikuwa katika nafasi nzuri za madaraka serikalini. Mwanawe mkubwa wa kiume, Meja Dkt. Abdul Ghafuur Zahid haraka sana akafutilia mbali Wasiiya wake na baadae mwanawe mdogo naye akafanya hivyo hivyo.”
Akaendelea kuandika:
“..tangia tuwe watu wazima, tumekuwa tukisikia Tashreek tu za Jumuiya (maombi ya Chanda mbalimbali), kila Khalifa alileta tashreek fulani mpya. Unapohudhuria hadhara za harusi au katika msiba wa mtu fulani, wajumbe wao (wa Jumuiya) huwepo hapo, wakisisitiza WASIYA. Chochote ambacho kimekusanywa zaidi ya miaka 100 iliyopita si kingepaswa kutumika kuwasaidia hao watu wanaostahili ....ni dini ya aina gani hii ambapo upanga wa pesa siku zote unapunga (juu ya vichwa vyetu). Ukitazama kwa uchache kuna Michango takribani 50. Je Michango hii (CHANDA) ni sehemu ya nguzo za Uislamu? Wao huwa hawaombi ZAKA hadharani...”
“Tusipopiga kelele za pamoja, dhuluma hii itaendelea na kasha la hazina ya Familia ya MIRZA litaendelea kujaa na sisi tutaendelea kukandamizwa kwa dhuluma hii. Kwa ajili ya Mungu tokeni kwenye matope haya.”
Kwa rejea zaidi, taz. Ahmadi.org. (http://www.ahmedi.org/article/urdu/wassiyyat.php)
Fungua hapa kwa ajili ya Fomu ya Waasiya iliyotumiwa na Jumuiya nchini Canada
Chanda ya Langerkhana (Jiko la Umma)
Wakati watu walipoanza kuja Mjini Qadian, likajengwa jiko la umma ili kuwalisha wao, ni dhahiri kutokana na michango ya umma. Ndiyo kusema Slyly akaanza chomoa-chomoa nyingine ya michango kutoka kwa ‘mukhlis muridiina’. Mnamo mwaka 189, aliandika kitabu, Fatih Islam, ambamo alitaja matawi matano ya Biashara ya Mungu, kitabu hicho akakabidhiwa Mirza Ghulam Ahmad Qadian-MGAQ. Tawi la 1. Kuandika vitabu. Tawi la 2.Matangazo. Tawi la 3. Kuwalingania Watu. Tawi la 4. Barua. 5. Kuchukua kiapo cha utii. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa ombi la jumuiya la kuchangia Chanda ya Jiko na aina nyingine za Chanda zitakazokuja huko mbele.
Ukumbusho: Chochote ambacho tumekieleza katika kitabu Risala Fatih Islam kuhusiana na matawi hayo matano ya Biashara ya Mungu ambayo imekabidhiwa kwetu na Mungu na hitajio la kupata msaada kutoka kwa Wahisani wa Kiislamu wenye Ikhilasi ya kidini, ndugu zetu wenye Ikhilasi na wenye hamasa waitikie haraka sana ili kazi hizi zianze kwa ufanisi..” (Tangazo lisilo na tarehe, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.1 uk 201).
...gharama zote husika za Langerkhana...wakati fulani zilifika Rupia 700 kwa mwezi au wakati mwingine zilifika 2000 kwa mwezi lakini mkono uliofichikana wa Mungu ulikuwa nasi kwamba hatukukabiliana na ugumu wowote ule. Sasa hali ya mambo ni kwamba kwa sababu ya njaa, gharama zimepanda mno.....(Inaonekana kuwa MGAQ alipoteza imani kwa mkono wa siri wa Mungu.!!! Rashid).” (Tangazo la tarehe 4, Oktoba 1899. Majmuu-e-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk.156).
“.....kwa hiyo kwanza kabisa Jumuiya lazima itilie maanani mpango huu (wa fedha za Jiko).....
...hivyo kwa utashi wa kibinadamu chukueni hatua ya kutoa msaada huu bila kukawia. Kila mmoja anapaswa kusaidia Langerkhana hii kulingana na rasilimali alizonazo......”
....na nataka kuwa mpango huu uwe hivi kwamba nami nipate nafuu ya kero hii ya Langerkhana na nishughulike na kazi yangu....”
(Tangazo la tarehe 4 Oktoba 1899, Majmuu-e-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo juz.3 uk.157)
Seth Abdur Rahman, mfanyabiashara wa Madras anastahili sifa....yeye ndiye anayesaidia jiko la umma...mara kwa mara hutuma Rupia 100 kila mwezi na mara nyingi ametuma Rupia 500...” (Tangazo la tarehe 4 Oktoba 1899, Majmuu-e-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk. 158)
Tangazo liitwalo “Maandalizi ya Langerkhana”
Kwa sababu ya wingi wa wageni na wingi watu wanaotafuta ukweli, matumizi ya jiko la umma yameongezeka mno na jana wakati nilipotafakari sehemu mbalimbali za jiko la umma na kila kitumikacho katika ukaaji na ulalaji wa wageni na taa na vitanda na vyombo na mikeka ya sakafuni na ukarabati wa majumba na wafanyakazi wanaohitajika na fundi bomba na mtu wa kufua na mtu wa kusomba takataka na kukusanya barua n.k. ...nikaona kuwa kwa wastani gharama zitakazoingiwa kila mwezi ni Rupia 800, na hadi hivi sasa, ni kwa baraka na rehema Zake Mungu hatujapata dhiki yoyote.....na pato la kawaida halifiki hata Rupia 60 kwa mwezi wakati ambapo gharama hazipungui Rupia 800 hivyo, mpango fulani wa ‘Tawakkulan ‘ala Allah’ (Kutawakali kwa Mungu) ni muhimu......kwa sababu hiyo, ni jambo la lazima kwa kila mtu kunifahamisha kwa barua maalum kwamba atatoa kiasi hiki cha Chanda ya kila mwezi ukiwa ni wajibu....” (Tangazo la tarehe 15 Machi 1902, Majmuu-e-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk.469).
Ndimi mbili gani hizi! Kwa upande mmoja anazungumzia Baraka na rehema za MwenyeziMungu, Kutawakal kwa MwenyeziMungu na kisha kuwataka watu watoe Chanda! Inaonekana kuwa MGAQ alipoteza imani kwa Mungu kuwa Atafanikisha mipango mingine yoyote ile!!!
Chanda ya Madrasa
Jamaa wote wanataarifiwa kuwa utaratibu huu wa Chanda Madrasa inaamuliwa utofautishwe na kwamba katika utaratibu huu ndugu yangu Mir Nasir Nawab ndiye kateuliwa kuwa muhasibu...” (Tangazo la tarehe 5 Februari 1898, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.2 uk.455).
Mimi naona inafaa kuwa shule ya Kati ijengwe mjini Qadian ambapo mbali ya elimu ya Kiingereza, sehemu moja ya elimu itakusanywa nami.....kila mwezeshaji mfahamisheni kuhusiana na mchango wake wa kudumu kwamba nini anachoweza kuchangia katika njia hii ya kheri kila mwezi..” (Tangazo la tarehe 5 Septemba 1897, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.2 uk.455).
Kuanzishwa kwa Madrassa na kuendelezwa kwake nako pia kwategemea sababu kadhaa za msingi. Kwa hiyo ni lazima kwamba kila mtu ajiwekee wajibu wa kutoa kila mwezi kulingana na uwezo alionao....” (Tangazo lisilo na tarehe, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk.470).
Chanda ya Koh-e-Nauman na Kabul (Afghanistan)
Manabii wa kweli wa MwenyeziMungu hutupa habari zilizofikishwa kwao na MwenyeziMungu kwa njia ya Wahyi. Ingawaje MGAQ alidai kuwa chochote ambacho kakisema au kukiandika kimetoka kwa Mungu, lakini bado wakati akiandika kitabu, Masihi Hindustan Mein, alijaribu kukusanya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali. Hivyo akapanga makundi fulani mawili kwenda Afghanistan hadi Nassebain (mji wa jirani na mpaka wa Syria) kukusanya ushahidi fulani. Na kama kawaida aliwataka wafuasi wake kutoa mchango (Chanda) ili kumudu gharama za safari ya makundi haya.
“Nimesikia kwamba katika kiriri cha Mwana Nabii kule Kpoh-e-Nauman, kuna mali kadha wa kadha kwa jina lake mjini Kabul. Kwa lengo hili, isiwe bure bila maslahi kwa marafiki kwenda Koh-e-Nauman na marafiki kadhaa kwenda Kabul na kuchukua nakala za nyaraka za mali hii ofisi....hivyo, ni muhimu kuandaa masurufu ya safari zao....” (Tangazo la tarehe 4 Oktoba 1899, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk. 163-164)
Chanda ya Safari ya Nasiibain
“...na la pili imethibitika kuwa Sayidina Isa alaihi salaam alikuja Afghanistan kupitia Nasiibain na jambo hili limo katika Kitabu, Raudha-as-Safa ambacho wakati wa mateso ya Msalabani mfalme wa Nasiibain akamwalika Sayidina Masihi ambapo Mwingereza mmoja amethibitisha hili kwamba Sayidina Masihi kwa hakika amepokea barua hii....kwa hali hiyo, ni jambo la hakika kuwa kule Nasiibain mnara fulani wa safari hii ya Sayidina Masihi alaihi assalam ungeweza kuwepo hapo na haingeshangaza kuwa mawe fulani ya kumbukumbu nayo yangekuwepo hapo....kwa hiyo ikaonekana yafaa kutuma watu watatu wenye maarifa na uitashi kutoka katika Jumuiya... kwa hiyo ni muhimu kuwaandalia masurufu yao ya safari...hivyo, yule anayetaka kutii maandiko yetu, asingoje hata kidogo katika kutii tangazo langu....na chochote awezacho kufanya na chochote awezacho kuandaa... atume bila ngojangoja.....” (Tangazo la tarehe 4 Oktoba 1899, Majumuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk. 164-165).
Chanda ya Sherehe za Jubilee ya 60 ya Malkia Victoria, Mtawala wa India

“Mara kwa mara tumeeleza katika vitabu vyetu kuwa kuwepo kwa Mama Malkia wa India, Mungu daima amuweke juu yetu, ni neema ya Mungu kwetu....hivyo lazima tumuombee Malkia wa India ndani kabisa ya nyoyo zetu apate maisha marefu na heshima na mali, Mungu daima amuweke juu yetu, na tuuombee utawala wake upate utulivu na udumu.....kwa maoni yangu jamaa na wanachama wa jumuiya yetu ambao wanakaa Punjab na katika miji mingine ya India wakusanyike tarehe 19, Juni, 1897 mjini Qadiani.....Ni wajibu kuwa kila mtu ashiriki kwa gharama zake mwenyewe...hivyo yeyote anayelipata tangazo hili, bila kukawia watoe MCHANGO (CHANDA) kwa ajili ya mkusanyiko huu (Jalsa)....jina wote waliotoa CHANDA pamoja na jitihada zao za kuandaa sherehe hizi litaandikwa katika kumbukumbu na kupelekwa katika Kamati Kuu.....” (Tangazo la tarehe 7 Juni 1897, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.2 uk.420-421).


Chanda ya Askari wa Uingereza waliojeruhiwa katika Vita ya Pili ya Makaburu
Sehemu mbalimbali za Bara la Afrika zilitiwa utumwani kwa karne nyingi na Wakoloni waliotoka Ulaya kwa minajili ya kujipatia rasilimali. Hasa zaidi walikuja kama wafanyabiashara na wakageuka kuwa Watawala. Waingereza wakatwaa himaya ya kudumu ya Koloni la Cape mnamo mwaka 1806 na kidogo kidogo Makaburu waliokuwa wakiishi ndani na walioizunguuka Cape wakahamia Kaskazini. Mnamo mwaka 1877, Transvaal ikavamiwa na kugeuzwa himaya ya Mwingereza jambo ambalo lilisababisha Vita ya Kwanza ya Makaburu mwaka 1880 ambapo Waingereza walishindwa. Na Transvaal ikapata tena uhuru wake. MGAQ ndio kwanza alikuwa ameanza kazi yake kipindi hicho, ndiyo kusema hakuna rejea ya jambo hili katika maandiko yake. Mnamo mwaka 1886, hazina nyingi za dhahabu zilivumbuliwa mjini Transvaal jambo lililosababisha mmiminiko mkubwa wa watu waliosaka utajiri, hasahasa Waingereza. Hali ilitokea katika Vita ya Pili ya Makaburu ambayo ilidumu kwa miaka 3 kuanzia 1899-1902. Hatimaye Makaburu wakalazimishwa kuhama na kwenda kwenye kambi mchanganyiko ambako mazingira magumu yalipelekea kufa kwa maelfu ya watu miongoni mwao kutokana na maradhi na utapiamlo. (http://en.wikipedia.org/wiki/Second Boer War).
Bado mtu huyu aliyeitwa nabii wa Mungu, ambaye alitangua jihad na ambaye Jumuiya yake ilipaza kaulimbiu ya Upendo kwa Wote, Chuki isiwe kwa Yeyote, alidhihirisha utii wake kwa Malkia kwa kuomba Michango (Chanda) kutoka kwa wafuasi wake kwa ajili ya askari wa Uingereza waliojeruhiwa:
Katika wakati huu wa Idi Mubaraka baada ya kueleza ukarimu wa serikali ya (Mwingereza) tuliyoielekezea usikivu wetu, yule anayedumisha utii thabiti kwa serikali hii na anayeona dhambi kubwa kuishi maisha ya kinafiki kama watu wengine, kwamba kila mtu anapaswa kuomba ndani ya moyo wake kwamba Mungu ampe ushindi mkubwa katika hii vita inayoendelea mjini Transvaal.....watu wa jumuiya yetu vyovyote walivyo, kulingana na uwezo na rasilimali zao, watoe CHANDA kwa ajili ya (askari) waliojeruhiwa katika Vita ya Transvaal ya Serikali ya Mwingereza....Jumuiya yetu inapaswa kulichukulia jukumu hili kuwa ni la muhimu na ilitekeleze upesi sana.” (Ad tarehe 10, Februari 1900, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.3 uk.218-219).
Pendekezo la Biashara ya Jarida la Kiingereza
Mnamo mwaka 1901 Mirza Ghulam Ahmad Qadiani (MGAQ) aliamua kuanzisha jarida Jarida la Kiingereza la kuchapisha makala zake. Alipendekeza kuwa hapana budi kuwe na mfuko wa kudumu wa fedha wa jarida hilo, kuwe na wadau wa kuwekeza katika mradi huu ili uwe kama biashara na fedha ziwekwe benki. Cha kuvutia yeye mwenyewe akaandika kuwa asingelihusika chochote na mfuko huo, yumkini alitanabahi kuwa watu wengi sasa walikuwa wakinong’ona kuhusu matangazo yasiyokwisha ya michango (CHANDA).
“Fedha hizi zitakusanywa na kuwekwa benki na ni muhimu kueleza kuwa mimi sitahusika chochote na usimamizi wa mfuko huu....na kumbukeni kuwa CHANDA hii itakuwa kama biashara....” (Tangazo la tarehe 15, Januari 1901, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz. 395).
Pendekezo hili muda si mrefu likawa ombi la CHANDA nyingine (Mchango mwingine)!!
“Hadi sasa kwa ajili ya uchapishaji wa jarida hili, hakuna mfuko wa kuridhisha wa kudumu....hivyo, kwa kulazimisha, nataka usikivu wa watu wa Jumuiya yangu waliohamasika kikwelikweli waonyeshe utashi wa kuliwezesha jambo hili kifedha.....Mungu mara kwa mara kanifunulia wahyi kwamba kwa ukweli na kwa utakaso mtu atakayehesabiwa kakubalika katika Jumuiya ni yule ambaye atatumia mali yake aipendayo mno katika njia hii.....ukiitumikia kwa kiasi kikubwa cha kuuza mali zako zote zisizohamishika na kuitumia katika njia yake, bado itakuwa kinyume na lengo kudhani kuwa umefanya ibada....iwapo watu 10,000 katika Jumuiya hii watakuwa wateja wa jarida hili basi jarida hili litanusurika.” (Tangazo la tarehe 16 Oktoba 1903, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz. 3 uk.496-499)
Chanda ya Madrasa Taliim-ul-Ombi jingine
“....Kwa kifupi mbali ya Jiko la Umma na Jarida lichapishwalo kwa Kiurdu na Kiingereza ambalo jamaa wengi wameonyesha kuwa na hamasa nalo, Madrasa moja pia imwanzishwa mjini Qadian kwa ajili ya watoto wadogo....nimefikiria sana jambo hili...sasa nalazimika kutoa mwito kwa watu wanyofu wa Jumuiya yangu kwamba kama wanaweza basi watenge kiwango fulani cha CHANDA ya kila mwezi kwa ajili ya Madrasa hii...” (Tangazo la tarehe 16 Oktoba 1903, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyiko wa Matangazo, juz.3 uk. 507)
Mifano mbalimbali ya Biashara ya MGAQ
Mbinu ya Propaganda
“Katika zama za Masihi Muwuud, ombaomba mmoja wa Kiarabu alikuja hapa (Qadian). Mirza Ghulam Ahmad Qadian (MGAQ) akampa kiasi kidogo. Baadhi ya watu wakapinga jambo hili, MGAQ akasema: kokote nitakakokwenda, atatutangaza, hata akitutangaza ili kupata kingi zaidi kutoka kwa wengine, yeye ataufikisha utajo wetu hadi sehemu za mbali kabisa.” (Al-Fazl Akhbar Qadian juz.22 Na 103 uk.9 ya tarehe 26, Januari 1935, iliyotajwa katika Qadian Mazhab ka Iimi Mahaseba uk. 494).
Swala Yauzwa kwa thamani ndogo
Wakati mmoja mnamo mwaka, mtu mmoja tajiri kutoka Wilaya ya Kanpur, kwa jina Wali Mahammed, ambaye aliwahi kuwa Ahmadia kwa muda mrefu na alikuwa akimuandikia barua Masihi Muwuud kwa ajili ya afya ya mwanawewa kiume. Alimwandikia Huzuur kwamba nimekuwa nikiomba dua kwa ajili ya mwanangu kwa muda mrefu, lakini hadi sasa dua hazijajibiwa kumsaidia mwanangu, ingawaje Mungu kakuahidi wewe kuwa kila dua itajibiwa.....Masihi Muwuud...akasema, akamwandikia kuwa hii si kawaida ya Mungu kukubali dua zote...hakuna mwenye mamlaka mbele ya Mungu. Ikiwa mtu huyo tajiri ana hali mbaya sana basi atoe mchango wa hisani kwa jumuiya (silsila) yangu ambao uko ndani ya uwezo wake mkubwa, kisha anitaarifu na aendelee kunikumbusha.” (Mufti Mohammed Sadiq Qadiani, 20, Oktoba, 1937, imetajwa katika AlFazl Qadian tarehe 22 Oktoba 1922).
Nawab Saheb, Mtawala wa Maleer Kotla alipatwa na ugonjwa, ambapo ugonjwa wake ukamzidia. Wawakilishi wa Makadiani walioishi katika eneo hilo wakamwambia mamaake Nawab Saheb kwamba kama Mirza Saheb akiomba dua, atapona mara moja. Barua ikapelekwa kwa Qadian Saheb ambaye aliahidi kuomba dua na akawaandikia wamtumie Rupia 500. Hivyo akapokea Rupia 500 kutoka kwa mamaake Nawab Saheb, na akaendelea kuomba dua, lakini hakuna dua yoyote iliyopokelewa. Nawab Saheb hakupona na mwishowe akafariki dunia.” (Isha’at us Sunna juz.18 uk.146; imetajwa katika Raees-e-Qadian uk.427 iliyoandikwa na Rafiq Dilawari)
Dua kwa Malipo
“Soma hii kwa makini kwani kuna habari njema kwako ndani yake. Kwa, Watawala, Maliwali, Matajiri, Serikali na Viongozi wa ngazi za juu!!

....Enyi Viongozi wa Uislamu! Namuomba Mungu atie moyoni mwako nia njema zaidi kuliko mtu yeyote yule na katika nyakati hizi ngumu akujaalie uwe mtumishi wa kweli wa Uislamu. Ninakupa taarifa hii muhimu kwa ajili ya Allah kwamba Mungu kaniteua kuwa kiongozi wa karne ya 14, na kanituma kuuhuisha Uislamu.....


....Ninafanya kazi hii kwa miaka 10, lakini kwa vile vingi kati ya vitu vinavyohitajika kwa ajili ya kushajiisha Uislamu huhitaji kuwa na msaada wa kifedha, kwa hiyo, nikiwa kama tabligh, nililazimika kukuarifuni, hebu sasa sikiliza......Mosi, kwa ajili ya miradi hiyo mikubwa, hakuna fedha, na hata ikiwa kwa msaada wa baadhi ya watu wenye hamasa ya dini, sehemu ya kitabu ikichapishwa.... ukiacha nakala chache tu, kitabu hicho hakiuzwi, nakala nyinyi ama zifungiwe masandukuni kwa miaka au zitawanywe bure kwa ajili ya Allah...
....Ijapokuwa Jumuiya inastawi lakini bado hakuna mtu tajiri miongoni mwetu atakayechukua jukumu kubwa la kuitumikia dini. Na kwa kuwa mimi ndiye niliyeteuliwa na Mungu kuhuisha dini na Mungu akanipa habari njema kuwa atawajumuisha matajiri na wafalme katika jumuiya yangu....
1   2   3   4   5


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət