Ana səhifə

Kindumbwendumbwe saa 30am mombasa pamoja twaweza tournament frere town


Yüklə 29 Kb.
tarix18.07.2016
ölçüsü29 Kb.
KINDUMBWENDUMBWE SAA 7.30AM

MOMBASA

PAMOJA TWAWEZA TOURNAMENT FRERE TOWN

Tukielekea kule Frere Town Kisimani ni kwamba mechi za soka kungangania taji la Frere Boy Mikaya zinazidi kushika kasi huku miamba ya soka ikiwewesuka na kuuramba mchanga.


Alasiri ya leo vijana waliotitimuka misuli Soujar Boys watajibwaga katika uchanjaa huo kuchubuana na Mishomoroni United,kipute kitakachochakazwa mbele ya lukuki ya mashabiki.
Hapo kesho katika uga huo huo chipukizi wa Bakarani watawaandaa Taifa Stars kisha siku ya jumapili itakuwa ni zamu ya Kisimani wakijaribu kuwasalimisha Spyn Youth.
Kumbuka kwenye matokeo ya mechi iliyopita Randa Fc walidhihirisha weledi wao wa kusakata ngozi kerengende iliyoambwa kufumwa na kuundwa mpira kwa kuwachachafia Nyali States kibano cha magoli 4-2.
Tuelekee kule Bilima ambapo Freretown Fc walizidi kutamba kwenye ligi ya Twaha
KILULU SHIMBA HILLS.

mechi za kirafiki kujipiga msasa kwa ligi ya diwani zinazidi kushika kasi katika maeneo ya shimba hiils pwani kusini.


Hapo kesho kikosi kinachobeba neema na kudura za Kilulu kite Arsenal Fc kitajibwaga ugani kuchubuana na Valencia ya Eshu.
Aidha kwa mujibu wa kocha wa Arsenal Joseph Mshisho,atatumia wanasoka hofdari kama vile Swaleh atakayekuwa mlinda lango,Joseph,Asuu,Joseph Mlandi,Msilu Timothy,Jacob Thomas,Moddy,Mody Bakari,Duncun Masha,Mwambi,Musyoka na Musyoki.
Kikosi cha Valencia kwa uapande wake kimetishia kuwafunga Arsenal endapo watajilegeza.
Aidha tukisalia kuko huko Shimba Hills ni kuwa katika uwanjan wa shule ya upili ya Mwaluvanga,mwalimu mkuu wa shule hiyo anapania kuanzisha ligi hivi karibini kwa kauli mbiu ya kukuza talanta za chipukizi.
Kilulu imekuwa ikizua upinzani mklai kwenye mataji mengi hususan kwenye ligi ya Masemo walipobanduliwa mapema.

Uwanjani Ali Sami Yen huko Istanbul, Uturuki, Liverpool yawewesuka na kuuramba mchanga kwa kichapo cha pili mfululizo cha mabao 3-0 mikononi mwa Galatasaray kwenye ngarambe ya kirafiki.

Kumbuka wikendi iliyopita miamba wawa hawa walichunwa mabao 3-0 na Hull City Uwanjani KC.

Hadi kufikia hatua ya mapumziko miamba wa Galasaray walikuwa kidedea kwa mabao 2-0 yote yakizamishwa kimiani na moto wa kuotea mbali zamani akiisakatia Liverpool mwite Milan Baros.

Baros alicheka na wavu kuako dakika ya 7,39.

Jahazi la Liverpool lilizidi kudidimia kunako kipindi cha pili pale mshambulizi wa kutegemewa Johan Elmander zamani akiichezea Bolton Wanderers alipofyatua zinga la kwaju dakika ya 84 lililozaa bao la tatu.Na kumbuka Elmander amehamia Galatasaray yapata mwishoni mwa mwezi Mei Mwaka huu.Elmander alipachika bao hilo dakika ya 84.Sasa Liverpool wana kibarua cha ziada siku ya jumatatu Agosti mosi kwani watajibwaga ugenini kuchumuana na Valerenga ya Norway na kisha kufuatiwa na mechi ya nyumbani ugani Anfield watakapowakabili Valencia ikiwakilisha taifa la Uhispani

Kabla ya mipigo hiyo mara mbili The reads ilijumuika kwenye ngarambe mbili na kushinda kwa kuichabanga Guandong ya Uchina mabao 4-3 mnamo Julai 13 kisha kuandikisha ushindi wa 6-3 mikononi mwa Kombaini ya Malaysia mnamo Julai 16


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət