Ana səhifə

Idara ya umoja wa mataifa inayohusika na wakimbizi


Yüklə 6.82 Kb.
tarix26.06.2016
ölçüsü6.82 Kb.
IDARA YA UMOJA WA MATAIFA INAYOHUSIKA NA WAKIMBIZI.

UNHCR
UJUMBE WA IDARA YA UMOJA WA MATAIFA YA WAKIMBIZI KWA WAKIMBIZI NA WANAOTAFUTA MAKAO HAPA NCHINI AFRIKA KUSINI.
Idara Ya Umoja wa Mataifa inayohusika na shughuli za wakimbizi na wanaotafuta makazi, inahusika kwa undani kuhusu mavamizi ya hivi karibuni kati ya mengine mengi, yanayoelekezwa kwa wakimbizi na watu wanaotafuta makazi hapa Afrika Kusini kutoka Nchi zingine. Mavamizi haya yamesababisha maafa, uharibifu wa mali na kukimbia kwa maelfu ya watu kutoka sehemu walikoishi. Idara Ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi inakemea mavamizi haya na inahimiza serikali ya Afrika Kusini kuendelea na jitahada zake za kuwasaidia wahadhiriwa na kumaliza mavamizi haya.
Kwa muda wa wiki zilizopita, Wakimbizi na watafutaji wa makao hapa Nchini, wameendelea kuuliza maswali yanayohusiana na uwezekano wa wao kurudi nchini mwao, kuunganishwa na jamii za hapa Afrika Kusini walikoishi au kuhamishwa kwenda Nchi zingine zinazoendelea. Idara Ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi, imejibu haya maswali bila kusita kwa kutoa maelekezo yake kama ifuatavyo.
Wanaopenda kurudi makwao kwa hiari, Idara Ya Umoja Wa mataifa ya wakimbizi, itawasaidia. Hizi jitihada zitatimizwa kwa njia zilizosalama. Uamuzi wa kurudi lazima ufanywe na watu Binafsi kwa hiari. Idara Ya Umoja wa Mataifa ipo tayari kutoa ujumbe uliopo kwa wote ambao wangependa kurudi makwao, ili waweze kufanya maamuzi yanaofaa. Idara Ya Umoja wa Mataifa haitasaidia watu kurudi kwenye Nchi au sehemu ambazo sio salama.
Kupewa Makao mapya, sio njia mwafaka ya kuweza kutatua tatizo hili, ikizingatiwa idadi kubwa ya watu walioadhirika na janga hili, kama inavyofanyika hapa afrika kusini, ambapo mahitaji muhimu ni usalama na mali. Idara Ya Umoja wa mataifa ya wakimbizi haitaruhusu au kukubali au kupitisha uandikishaji wowote wa wakimbizi na wanaotafuta makao, unaofanyika katika makao ya muda wanamoishi ambayo ni salama.
Kuunganishwa na Jamii za Afrika kusini, Idara ya Umoja wa Mataifa inaunga serikali mkono, katika jitihada zake za kuwahimiza, wakimbizi na wanaotafuta makao kurudi kwenye Jamii za hapa Nchini kwa njia zilizo salama. Kufanikisha mpango huu, Idara Ya Umoja wa Mataifa itaangalia, kupitia kwa wahusika wake wakuu na kuomba kusaidia kifedha wakimbizi kulingana na shida zao.
Idara Ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi itaendelea kujihusisha na serikali ya Afrika Kusini, katika jitihada zake zakukabiliana na athari zilizotokana na mavamizi haya, haswa za wakimbizi na wanaotafuta makao kutoka nchi zingine.Idara Ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi pia ingependa kuwahimiza wakimbizi na wanaotafuta makao kuzingatia na kuheshimu sheria za Afrika kusini, Pia inawahimiza kushirikiana na serikali.
Kwa maelekezo zaidi: piga simu kwa idara ya mkoa waa umoja wa mataifa jijini Pretoria, Nambari ya simu ni: 012-354 8303 au nambari ya simu ya haraka ni:071 687 3091


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət