Ana səhifə

Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahiim Harakati za Uislamu dhidi ya Ahmadiya Chungu Mosi, Rabiul Awwal 1430 Februari 24, 2009


Yüklə 0.51 Mb.
səhifə1/5
tarix26.06.2016
ölçüsü0.51 Mb.
  1   2   3   4   5
Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahiim
Harakati za Uislamu dhidi ya Ahmadiya

Chungu Mosi, Rabiul Awwal 1430

Februari 24, 2009
"Basi adhabu kali itawathibitikia wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: "Hiki kimetoka kwa MwenyeziMungu." Ili wachukue thamani ndogo ya kilimwengu. Basi ole wao kwa yale waliyoyaandika kwa mikono yao. Na ole wao kwa wanayoyachuma." (Qur'an 2:79).
"Lakini akitaka pesa, basi huyo ni nabii wa uwongo" (Didache 11:9, Mafundisho ya Mitume Kumi na wawili)
"Waliochaguliwa na Mungu, ambao hutokea Mbinguni, wanayo dhamana ya kufanya biashara na jumuiya yao. Huchukua mali yao ya muda na hujiweka kuwa warithi wa mali ya milele..." Mirza Qadiani
Kumbe yote hii ni pesa, basi Upumbavu!
Mirza Ghulam A Qadiani- Nabii au Maslahi?
Jumuiya ya Ahmadiya- ni Jumuiya ya Nabii au Kampuni ya Biashara?
Mwandishi Dkt Syed Rashid

Mfasiri Shuaybu Kifea
(Kwa kuwa Jumuiya haijatafsiri vitabu vya Mirza kwa sababu wanazozifahamu vema wao wenyewe, nukuu zote za hapa chini zimetafsiriwa nami. Nimejitahidi kuziweka kwa mujibu wa matini halisi, na nisadikini kuwa ilikuwa ni kazi kubwa mno kuisawiri changanyikeni ya maneno chungutele ya kujirudia-rudia katika maandiko ya Mirza-Rashid).
Katika historia ya dini za ufunuo na Manabii kuanzia Adan (AS) hadi Muhammad (SAW), hutakuta hata mfano mmoja wa nabii aliyeuza wahyi kwa thamani ya dunia. Ni hakika kuwa Qur'an Tukufu imejaa mifano ambapo Manabii wa MwenyeziMungu waliwasilisha ujumbe wa Allah huku wakisema kwa kurudia-rudia:
"Na enyi watu wangu! Mimi sikuombeni mali juu ya (jambo) hili, sina ujira wangu ila kwa MwenyeziMungu." (Hud (11):29).

Sema: "Ujira niliokuombeni (kama nilipata kukuombeni), basi huo ni wenu nyinyi. Hauko ujira wangu ila kwa MwenyeziMungu tu, naye ni Shahidi juu ya kila kitu." (Saba (34):47).
Manabii wa kweli wa MwenyeziMungu waliwahimiza wafuasi wao kutoa katika njia ya MwenyeziMungu , kutoa zaka na sadaka kuwapa masikini na wenye kuhitaji lakini hawakuomba kulipwa kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa MwenyeziMungu. Na hapakuwahi kuwepo na tofauti ya ada hii katika historia ya Manabii wa MwenyeziMungu. Wao ndio waliokuwa vigezo vya tabia.
Lakini unapoitazama historia ya manabii wa uwongo na waliojimithilisha na manabii ili kuwahadaa watu, yote imehusiana na pesa na maslahi ya kidunia. Katika makala hii, nitajaribu kukuonyesha jinsi Mirza Ghulam Ahmad Qadiani na Jumuiya yake wasivyosalimika na ada hii.
Viongozi wengine wa dini kama vile mamula, makasisi, mapanditi, marabi huenda nao pia wanafanya biashara hii lakini hao si lengo la makala hii. Kamwe wao hawakudai kuwa ni manabii. Manabii hawakuuza Neno la Allah. Wale wanaofanya hivyo ni manabii wa kujipachika, na kuna onyo kali kwa watu hao ndani ya Qur'an Tukufu na katika Maandiko matakatifu.
**********************
Mirza Ghulam Ahmad Qadiani (MGAQ) adai yeye ni nabii wa Mungu
"Naapa kwa Mungu ambaye mikononi mwake upo uhai wangu, Yeye ndiye aliyenituma, Yeye ndiye aliyeniteua kuwa nabii na Yeye ndiye aliyenituma kama Masihi aliyeahidiwa." (Tatumma Haqeeqatul Wahi, Roohani Khazain juz.22. uk 503).
"Mungu wa kweli ni yule Mungu aliyemtuma nabii Wake kule Qadian." (Dafa al-Bala uk. 11, Roohani Khazain juz. 18 uk. 231).
Aya za MGAQ zinatoka kwa Mungu
"Na kama ninavyoamini aya za Qur'an ndivyo ninavyoamini ufunuo wa Mungu ambao umenishukia bila tofauti hata kidogo... Na naweza kusimama hata Ka'aba na kuapa kuwa wahyi huo mwema unaonijia, ni neno la Mungu yuleyule aliyeteremsha aya Zake kwa Musa na Yesu na Sayyidina Muhammad SallAllahu alaihi wassalam." (Aik Ghaltee kaa Izala uk.6, Roohani Khazain juz. 18 uk. 210).
"Naapa kwa MwenyeziMungu mimi naamini funuo hizi kama vile vile Qur'an na Vitabu vingine vilivyotoka kwa Mungu, na kama ninavyoiitakidi Qur'an Tukufu kuwa ni neno la hakika na lililokamilika la Mungu ndivyo ninavyoamini kuwa ule ufunuo unaonishukia mimi ni neno la Mungu." (Haqeeqat-ul-Wahi uk.211, Roohani Khazain juz. 22 uk. 220).
"Naamini WAHI wangu kama ninavyoamini Qur'an na Taurat." (Roohani Khazain juz. 17 uk. 454).
MGAQ adai chochote anachosema na kukitenda hufunuliwa kutoka kwa Mungu
"'Kullama qultu min amrahuu, wa maafa'altu un amrii, wa maa aftaraitu 'alaa Rabbi al'Alaa'- Chochote ambacho nimekisema, nimekisema kwa Amri Yake (Mungu) na sijafanya chochote kwa matakwa yangu na sijamsingizia chochote Mola wangu." (Mawahibur Rahman uk.3, Roohani Khazain juz.19 uk.221)
" 'wa maa untiqu unil hawa illa wahun yuuha'- yeye hasemi chochote kwa hiyari yake, bali chochote unachosikia ni wahyi wa Mungu." (Arba'iin Na.3, Roohani Khazain juz. 17, uk. 426-427)
MGAQ kamwe hafanyi kosa
"Bila shaka Mungu kamwe haniachi na kosa, hata kwa kitambo cha kupepesa jicho; na Ananikinga na kila kosa na ananikinga na mila za mashetani." (Nur ul Haq Last page, Roohani Khazain juz. 8 uk 372).
Kutokana na nukuu za hapo juu mahitimisho yafuatayo yanaweza kufikiwa hivi kwamba kwa mujibu wa MGAQ:
.Mirza ni Nabii wa Mungu

. Katika wahyi na anaitakidi unafanana na Qur'an na Vitabu vingine vitukufu vilivyoteremshwa kwa Manabii wengine wa Allah.

. Maneno na matendo yake yote yamefunuliwa na Mungu

. Mirza katu hajafanya chochote wala hajaandika chochote isipokuwa kile tu ambacho kimefunuliwa na Mungu.

. Mungu Kamwe hamuachi MGAQ na kosa hata kwa mpepeso wa jicho. Kwa maneno mengine hakuna hata kosa moja katika yale aliyoyaandika au kuyatenda.

Hali ya Familia huko nyuma na Maisha ya Awali ya MGAQ


Kabla hatujautazama kwa undani mwenendo wa Mirza kabla ya kuanza kwake kudai ile hadhi kubwa aliyodai kupewa kwa amri ya Mungu, ni vizuri zaidi kuitazama hali ya nyuma ya familia yake ili kuelewa kwa nini alikuwa na uchu wa maslahi ya kipesa. Yeye alitokana na familia ya wamiliki na wakodishaji wa ardhi ambao walikuwa raia watiifu wa Mwingereza kwa maslahi ya vizazi vyao.
Hata hivyo, kipato cha familia kilikuwa vinapungua hadi ulipofika wakati wa Mirza, kipato hicho kilikata kabisa. Kwa hiyo, wakati wote pesa ndiyo ikawa sababu iliyomtia wasiwasi.
"Katika kile kipindi cha awali cha Singasinga, babu yangu mkubwa, Mirza Gul Muhammed alikuwa chifu aliyetajika na kuvuma katika eneo lake. ...wakati huo wa babu yangu...dhahama kubwa ikawaangukia mababu zangu...ndipo tena katika siku za mwisho –mwisho za utawala wa Ranjit Singh, marehemu baba yangu, Mirza Ghulam Murtaza, akarudi Qadian, na akatwaa tena mashamba 5 kutoka katika mali za babaake...ikiwa bado familia kongwe, baba yangu ndio akawa chifu mashuhuri katika eneo hili." (Kitab ul Bariyah, Roohani Khazain juz. 12 uk. 175-176)
"Kwa kifupi, hali ya mashamba yetu ikashuka siku hadi siku, hadi mwishowe tukafikia hatua ambapo familia yangu ikawa mmiliki wa daraja la chini wa ardhi." (Tuhfa-e-Qaiseriya, Roohani Khazain juz.12 uk.271).
"Baada ya hilo pale walipokuja Waingereza, wakataifisha mashamba ya familia yetu, na wakaweka pensheni ya heshima ya Rs. 700 kwa mwaka ambayo ikapunguzwa hadi kufikia Rs. 180 alipofariki dunia babu yangu, na alipokufa ami yangu ikasitishwa kabisa." (Siirat-ul-mahdi sehemu ya 1riwaya na. 48, na Mirza Bashiir Ahmad s/o Mirza Ghulam Qadiani).
Tabia ya Nabii-Khulka ya MGAQ katika maisha ya awali:
"Mama (++ mke wa Mirza) aliniambia (mtoto wa Mirza) kuwa wakati mmoja enzi za ujana wake Masiiih Muwuud (Mirza Qadiani) alikwenda kuchukua pensheni ya babu yangu, kisha Mirza Imamdin naye akamfuata. Pale (Mirza) alipopokea pensheni hiyo, Imamdin akamrubuni (Mirza) ambapo badala ya kurudi mjini Qadian yeye akaondoka naye mbali. Akenda naye huku na kule. Halafu alipokuwa ametapanya pesa zote, (Imamdin) akamtelekeza na kwenda zake." (Siirat ul Mahdi sehemu ya 1 riwaya na. 49, na Mirza Bashiir Ahmad, mtoto wa Mirza Qadiani).
MGAQ alikwenda Sialkot kufanya kazi ya ukarani kwa ujira mdogo. Hili kwa kweli halikuwa jambo alilolitaka kwa maisha yake. Akitokea katika familia ya wamiliki wa mashamba, yeye alitamani aina ya maisha ya starehe. Muda wote akawa anahaha na mambo ya pesa Kiasi kwamba pale al;ipopokea ulioitwa wahyi wa kwanza kutoka kwa Mungu, hakuwa na jingine kichwani mwake ila starehe za dunia:
"Nilipopokea wahyi wa kwanza ukibashiri kifo cha baba yangu, udhaifu wa kibinadamu ukanifanya nidhani kuwa kwa vile baadhi ya vyanzo vya kipato cha familia yetu vitakata kwa kifo cha baba yangu, huenda tukatumbukizwa matatizoni." (Mirza Ghulam imenukuliwa kutoka "The Founder of Ahmadiyya Movement", na Muhammad Ali, uk. 7; pia tazama Roohani Khazain juz. 13 uk. 194).
Wakati akiwa Sialkot, almtembelea mtu mmoja mtukufu kumuomba amuombee dua:
"Katika siku siku zake za mwanzo, Mirza Sahib alikwenda Amritsar na kukutana na walii mmoja, Molvi Abdullah Ghaznawi. Mirza akaomba hivi: Mimi niliajiriwa katika mahakama ya Sialkot kwa mshahara mdogo. Kwa kuwa ilikuwa vigumu kuishi kwa mshahara huo mdogo, nikajiandaa kwa mtihani wa sheria lakini nikafeli. Molvi Sahib akamuuliza: Kwani kusudio lako ni nini sasa? Mirza Sahib akasema: Hvi sasa sina nia yoyote ya kufanya kazi. Ninataka kuishi kwa kutawakkal tu (imani kwa Mungu, kwamba Mungu atamtimizia mahitaji yake). Nakuomba uniombee Rajuu'at na Futuuhaat. Tafadhali nifanyie dua." (Masihi wa Karne ya 14 uk. 48)
(Rajuu'at ni neno ambayo kwayo mtu huomba kuwa watu wavutike kwake, na Futuuhaat ni neno lenye maana kuwa watu hao wamletee zawadi kwa fedha taslimu na kwa huruma kwake).
Hivyo basi, tunaona kuwa Mirza alitaka maisha ya raha kwa pesa ya kirahisi. Akizifahamu taasubi za Waislamu wa India, hilo halikuwa jambo gumu sana kwake. Alichofanya ni kujijengea sifa kuwa yeye ni mtu wa dini aliyetumwa na Mungu ambapo wafuasi mbumbumbu watafuata Bara Hindi lilitawaliwa na Waislamu kwa miaka 1000 (hivyo ndivyo alivyoishia babu yake mkubwa Mirza nchini India). Waingereza wakatwaa madaraka kutoka kwa Waislamu na sanjari na hilo likajiri wimbi la Wakristo na Wamishenari wa Kihindu. Mirza akaona hiyo ndiyo fursa ya kujijengea sifa. Akajitambulisha kuwa yeye ni mtumishi wa Uislamu na akaanza kuwachagiza kwa midahalo. Nini yakawa matokea ya midahalo hiyo, hilo liko nje ya upeo wa makala hii, yatosha tu kusema kuwa hilo ndilo lililomfanya awe mashuhuri na ndipo alipoanza kupata kundi, wengi wakiwa ni wanavijiji wasiojua lolote. Kama ilivyotarajiwa hakuna mtu aliyesumbuka kufuatilia kama alipata mafanikio katika midahalo hiyo au la, ilitosha kuwa mradi tu kiongozi wao anawapambana na maadui wa Uislamu. Ndipo alipotangaza kuwa yeye ni Mteule wa Mungu, na alikuwa mbioni kuandika kitabu kiitwacho Brahiin-e-Ahmadiyya kwa kukusanya aya (kama alivyotangaza MGAQ baadae), lakini bado Mirza hakuwa na hofu ya kukiuza kitabu hicho. Lakini kabla hatujautazama kwa undani mradi huo wa MGAQ, hebu tutazame mazingira ya kijamii na kiuchumi ya India katika kipindi cha mwishoni mwa Karne ya 19 ili kufahamu ni kiasi cha pesa alichokuwa anakitaka kutoka kwa watu.
Mazingira ya Jamii na Uchumi ya India 1880-1900
Katika kipindi (cha 1880) wakati MGAQ alipokuwa anauza kitabu chake kwa Rs. 5 au 10 au 25, hebu tutazame mazingira ya kijamii na kiuchumi ya Wahindi wa kawaida (Waislamu na wasio Waislamu). Wengi walikuwa ni vibarua mashambani au tuseme watumishi wa kilimo (ambao waliwatumikia mabwana zao kufa wakiacha urithi huo huo kwa vizazi vyao). Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwenye mtandao wa intaneti:
.Idadi ya watu wote wa India mnamo mwaka 1881 ilikuwa ni milioni 253.98. Waislamu walikuwa ni milioni 50.12, Wahindu walikuwa milioni 187.93 na Wakristo walikuwa ni milioni 1.86. (Vyanzo: Sensa ya mwaka 1881, British India 1876/7 hadi 188/6 London, Her Majesty's Stationary Office 1887).
. Kati ya Wahindi milioni 253, milioni 216 walikuwa hawajui kusoma wala kuandika. Milioni 107 walikuwa na umri wa chini ya miaka 20. Kati ya Waislamu milioni 50, Waislamu milioni 47 walikuwa mbumbumbu. (Chanzo: Sensa ya mwaka 1881. British India 1876/7 hadi 1885/6, Her Majesty's Stationary Office 1887)
. Wastani wa elimu ya kujua kusoma na kuandika ulikuwa ni asilimia 9.5 miongoni mwa Wahindu, na asilimia 6.7 miongoni mwa Waislamu. (Chanzo:Mukhtasari wa Takwimu unaohusu British India)
. Mwaka 1875 kulikuwa na Wafanyakazi 117 nchini India. (Chanzo: Heston, 'Pato la Taifa' kwa mwaka 1875).
. Asilimia 73.4 ya nguvu kazi hii ilikuwa katika sekta ya kilimo. (Chanzo: hicho hicho).
. Mwaka 1880 Pato la Mwaka la mfanyakazi asiye na ujuzi lilikuwa ni Rupia. 7.2 kwa kichwa kimoja (Mfanyakazi mmoja kwa familia moja, siku 180 kwa mwaka, familia ya watu wanne). Hii takriban inakuja Rs.0.04 kwa kipato cha siku. Mwaka 1900 patp la mwaka lilikuwa ni Rs.0.53 kwa siku. (Chanzo:Tirthankar Roy, Globalization, Factor Prices, and Poverty in Colonial India).
. Mishahara ya Mjini: Mwaka 1875 fundi mwenye ujuzi mdogo (mafundi chuma, mafundi seremala na mafundi waashi) walipata ujira wa kila siku wa Rs.0.314 na mwaka 1895 Rs.0.373. (Chanzo: Atkinson, 'Stastical Review' and Sivasubramonian, National Income).
. Ni kutoa tu ufahamisho wa bei za vyakula vya kawaida enzi hizo, Mchele uliuzwa kwa rupia moja kwa seer 10-12. (seer moja = 2.02 Ibs) (Chanzo: Sensa ya mwaka 1881, British India 1876/7 hadi 1885/6 London, Her Majesty's Stationary Office 1887) (Currently price of Basmati Rice is about Rs. 70).
***************
Neno la Mungu-Braheen-e-Ahmadiyya-yauzwa kwa fedha taslimu
MGAQ alidai kuwa Brahiin-e-Ahmadiyya ni neno la Mungu. Fungua Majmuua-e-Ishtihaaraat (Collection of Advertisements) juz. 1 ya MGAQ na utabaini kuwa matangazo ya mwanzo yaliyotolewa katika kipindi cha ile miaka aliyochapisha juzuu 4 za kitabu hiki yanahusiana na maombi kwa Waislamu kuchangia pesa au yanataka malipo ya kubandika (Advance payment) kutoka kwa wanunuzi watarajiwa. Mara zote alisononeka kwa kukosa mwitiko wa Waislamu. Katika nukta fulani alifikia hata kuwashutumu Waislamu wanaotumia pesa kujengea Misikiti na kutompelekea yeye pesa kuchapisha kitabu hiki.
"Kuchapisha kitabu kikubwa kama hicho ni vigumu sana bila ya msaada wa ndugu Waislamu. Na ujira wa kusaidia mradi huo muhimu hauna kificho hata kwa Muislamu wa kawaida. Kwa hiyo ni ombi kwa ndugu waumini kuwa washiriki katika kazi hii njema na kusadia uchapishaji wake Matajiri wakijitolea matumizi yao ya siku moja tu ya jikoni, kitabu hiki kitachapwa kirahisi, la sivyo mbaramwezi hii ing'arayo itabaki imefichikana. Au vinginevyo, wale watu wote wenye uwezo, wakiwa na nia ya kununua kitabu, watume Rs. 5 pamoja na maombi yao kwangu. Kitabu kikichapishwa, kitatumwa kwao." (Majmuu-e-Ishtihaaraat, Collections of Advertisements, juz. 1 uk. 11-12, Tangazo la Mei 1879)
Wakati alipokuwa anaomba Rs 5 kutoka kwa Waislamu wenziwe, rasilimali zake binafsi zilikuwa na thamani ya Rs. 10,000. Rs.1 ya mwaka 1880 ilikuwa sawa na Rs.15000 ya mwaka 2008. Hii ina maana kuwa kwa mahesabu ya leo, MGAQ alikuwa ni Milionea mkubwa (multimillionaire lakini bado alikuwa anaomba Rs 75,000 za kubandika kwa ajili ya vitabu, akijaribu kuwashawishi watu waamini kuwa alikuwa anauza kitabu kwa bei nafuu ya kutupa!! Katika tangazo hilo hilo aliandika hivi:
"Yeyote atakayekanusha dalili zilizotolewa katika kitabu hiki.....Nitatoa rasilimali zangu zote zenye thamani ya Rs.10,000 na kumkabidhi kila kitu." (Majmuu-i-Ishtihaaraat, Collection of Advertisements, juz.1 uk 11-12, tangazo la Mei 1879).
Mnamo Desemba 1879 alipandisha bei na kufikia Rs.10 kwa wateja wapya, ingawaje kitabu kilikuwa bado hakijachapishwa.
Mnamo mwaka 1880, alitangaza kuwa kwa wasio-Waislamu hakutakuwa na punguzo katika bei, watatozwa Rs.20!!
Mnamo mwaka 1882 alitangaza kuwa Rs.10 ni kwa Waislamu wa kawaida, lakini Rs.25 kwa Waislamu matajiri na wasioWaislamu matajiri.
Akalalamika:
"Bei halisi ya kitabu hiki ni Rs. 100 na badala yake Rs.10 au Rs.25 ndiyo ikawa bei maalum. Kwa hiyo, kama bei hii ndogo nayo inashindwa kulipwa na Waislamu kwa fedha za kubandika basi itakuwa kama vile wanajaribu kukwamisha kazi hii (ya kubainisha ukweli wa Uislamu)." (Tangazo la1882, Majmuu-i-Ishtihaaraat, Collection of Advertisements, juz.1 uk.35)
Mtu anayepokea nusu rupia kwa siku ili kuilisha familia yake anawezaje kulipa Rs. 5 kwa ajili ya Brahiin? Bado MGAQ alionekana kutojali kabisa hali hiyo ngumu ya mtu wa kawaida. Akaweka bei ya Rs. 10 kwa Waislamu wa kawaida na Rs.25 kwa wasioWaislamu. Ikiwa na anguko la thamani la asilimia 6-8 kwa sarafu, Rs. 10 huko nyuma mwaka 1880 ilikuwa sawa na Rs. 150,000 ya mwaka 2008 ambapo Rs.25 ni sawa na 375,000 ya leo. Je mtu huyu kweli alikuwa anafanya juhudi za kuutumikia Uislamu na kufikisha ukweli wake kwa wasioWaislamu!!!
Mirza Asikitika kukosa mwitiko
Kwa vile mwitiko wa Waislamu katika kununua kitabu hiki haukuendana na matarajio aliyokuwa Mirza, kadri muda ulivyokwenda sauti yake ikaanza kubadilika.
"Hapana budi ifahamike kuwa ndugu zangu wa kidini na Watukufu Waungwana na Wapenzi wa Dini ya Uislamu na Wafuasi wa Sunna ya Mtume (SAAW) kuwa mtu huyu mnyenyekevu kakusanya kitabu hicho kinachohusu ukweli wa Qur'an na ukweli wa Uislamu kuwa baada ya kukisoma yule anayetafuta ukweli hatakuwa na hiyari ila kufuata Uislamu.......kuchapisha kitabu hicho ni vigumu sana bila msaada wa ndugu Waislamu. Na ujira wa kusaidia mradi huu muhimu kama huo haufichikani hata kwa Muislamu wa kawaida. Hivyo inaombwa kwa waumini wa Kiislamu kuwa washiriki katika kazi hii njema na wasaidie uchapishaji wake. Matajiri wakitoa matumizi yao ya siku moja tu ya jikoni, kitabu hiki kitachapwa maramoja tu, la sivyo mbalamwezi hii ing'arayo itabaki kufichikana. Au vinginevyo, watu wote wale wenye uwezo, wakiwa nia nia ya kununua kitabu hiki, watume kwangu Rs.5 pamoja na maombi yao. Kitabu kikichapishwa tu, kitatumwa kwao." (Majmuu-i-Ishtihaaraat, Makusanyo ya Matangazo juz. 1 uk. 10-12, Tangazo la Mei 1879).
"....hati na uandishi maridadi na karatasi nzuri n.k. mahitaji na tahadhari ambavyo kwavyo kitabu hiki kitachapishwa, thamani halisi ya kitabu haiko chini ya Rs.20. Lakini kwa matumaini na kwa matazamio kuwa baadhi yaWaislamu matajiri na wenye utashi watatilia maanani na hivyo hasara iliyoingiwa kutokana na ushushaji wa bei ingefidiwa, bei iliyopangwa ni Rs. 5 tu. Lakini hilo halikutokea nami nimechoka kuandika....." (Tangazo la tarehe 3, Des. 1879, Majmuu-i-Ishtihaarat, Makusanyo ya matangazo, juz.1 uk.13)
"... sasa bei halisi ya kitabu ni Rs.100 na badala yake Rs. 10 au 2 ndiyo iliyopangwa. Hivyo, hata kiasi hiki kidogo Waislamu wasipotoa kwa kubandika basi itakuwa kama vile wanakwamisha kazi hii isikamilike…." (Tangazo la mwaka 1882 katika Brahiin-i-Ahmadiyya, sehemu ya 3, Majmuu-e-Ishtihaarat, Makusanyo ya Matangazo, juz. 1uk.34)
"....Lahaula! Wengi miongoni mwa Waislamu wameghafilika na jambo hili la baraka na (kazi) hiyo kubwa ambayo kuendelea na kunyanyuka kwa dini kuliitegemea, wameiacha kabisa na jamii nyingine ambazo maandiko yao matakatifu hayawafunzi suala hili, kutokana na matendo yao ya nyoyoni kuiinua dini yao kwa hamasa, kutekeleza jambo hili la 'kusaidia'...." (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-iAhmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.36)
"Ingawaje kuna kundi kubwa la Waislamu katika nchi hii ya Hindustan ambapo baadhi yao wana uwezo na baadhi yao haijambo, ukiondoa kikundi kidogo (cha matajiri, mawaziri na maafisa), wengi wao ni waoga, wana nyoyo zilifungika na kuwa ngumu kushiriki katika mambo ya kheri. Mawazo yao yanaishia katika matamanio ya kimwili tu na akili zao zinazongwa na ubinafsi usio na faida wa kujitoshelezea nafsi zao. Watu hawa hawaioni dini na shurti za dini kama ni kitu. Naam kwa ajili ya utajo na heshima yao wako tayari kupoteza maisha yao ya nyumbani." (tangazo la mwaka 1880 katika Brahii-i-Ahmadiyya Sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz. 1 uk. 36)

Kwa ajili ya dini kabisa, Waislamu wenye utashi (kama Bw. na Mwalimu wangu, Hazrat Khalifa Syed Mohammed Hasan Khan Sahib Bahadur, Waziri Mkuu, Patiala) ni wachache kiasi kwamba hakuna haja ya kuwahesabu kwa vidole" (Tangazo la 1880 katika Brahiin-i-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo. Juz. 1 uk. 36)


".... watu kadha wa kadha hata wakitoa kwa ajili ya mambo ya dini, huwa wanafanya hivyo kwa kitendo cha ibada, sio kwa nia ya kutimiza shurti fulani. Mathalani, ukiona mtu anajenga msikiti, mwingine ambaye ni mpinzani wake naye atajenga msikiti kushindana ama huo msikiti uwe unahitajika kweli au la, laki yeye hutumia maelfu ya rupia. Hakuna mtu anayetafakari kuwa katika zama hizi cha muhimu zaidi ni kuchapisha elimu ya dini, na hawatambui kuwa kama watu hawatabakia na dini nani atayeswali katika misikiti hii; wao wanataka nguvu na ustawi wa dini kwa minara mirefu tu ya mawe, na wanataka uzuri wa dini yao kwa marumaru za kurembea....kama Wayahudi wanaotaka tu kuwa waumini wa kuchapia-chapia tu. Hawataki kutekeleza faradhi za dini sawasawa wala hawajui kuzitekeleza, wala hawana habari ya kuzijua." (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-i-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo. Juz.1 uk. 36-37)
"Ijapokuwa inakubalika kuwa Umma wetu hutumia fungu lisilokadirika katika zile zinazoitwa sadaka na zaka lakini mbona watu hawafanyi amali njema ya kikwelikweli na katika ugawaji wa pesa, hawazingatii kipi kilicho bora zaidi na wapi panapofaa zaidi (kutoa), na wanaendelea kibubusa kutoa isivyostahili. Na wanapokuwa wamekinaisha matashi yao yote ya moyo katika kutoa sehemu hizo zisizozofaa, basi unapofika wakati wa kutimiza wajibu halisi, huwa wanashindwa kutoa.......hii ndiyo tabia ya wale ambao kwa sababu ya ukweli wa roho kutochochea nguvu ya ukarimu na hisani nyoyoni mwao, basi hubaki na choyo; kwa mfano baada ya kuzeeka tamaa huongezeka ya kupata udhuru wa kupata kirahisi Akhera kwa kujenga Msikiti na kupata nyumba iliyojengwa peponi. Na hisia zao za kutenda amali njema ni kwamba kama jahazi la Dini linazama mbele ya macho yao au kama dini nzima inahilikishwa, bado nyoyo zao haziguswi hata kidogo na hawana habari kama dini ipo au inatoweka. Kama wana uchungu, basi ni kwa ajili ya dunia, ikiwa uchungu ni kwa ajili ya dunia, ikiwa mapenzi ni kwa ajili ya dunia, ikiwa biashara ni kwa ajili ya dunia, na dunia yenyewe kama wengine walivyonayo, hawaimiliki." (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz. 1. 37-38).
"Kwa kuwa (kitabu) hiki ndio USHINDI MKUBWA dhidi ya maadui wa Uislamu, ndio lengo la moyo na maisha ya muumini, kwa sababu hiyo mimi nikawa na imani kubwa na matashi ya hamasa ya matajiri wa Kiislamu kwamba watanayojitokeza katika harakati za kukichapisha kitabu hicho, wataelekeza mazingatio makubwa katika kuondosha magumu hayo, lakini tuseme nini na tuandike nini. Allah ndiye msaidizi, Allah ndiye bora zaidi na ndiye atakayebakia. (Hiki ndicho kinachotokea wakati mtu anapoitazama mifuko ya Waislamu badala ya kumtegemea Allah) (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-i-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihahaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk.38)
"Nakala 150 za sehemu ya kwanza ambayo ilikuwa imechapishwa, Nilizituma kwa VIONGOZI na MATAJIRI na MABWANA WAKUBWA na ilitumainiwa kuwa matajiri wenye moyo watatanguliza malipo ya kitabu (ambayo ni madogo tu.....lakini ukiondoa mtu mmoja au wawili kulikuwa na ukimya kwa kila mtu." (Tangazo la mwaka 1880 katika Brahiin-i-Ahmadiyya sehemu ya 2, Majmuu-i-Ishtihaarat, Mkusanyo wa Matangazo, juz.1 uk. 38)
  1   2   3   4   5


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət