Ana səhifə

П р е д и с л о в и е данный учебно-методический комплекс


Yüklə 2.19 Mb.
səhifə14/25
tarix26.06.2016
ölçüsü2.19 Mb.
1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   ...   25

13. Дайте синонимы следующим словам и выражениям или объясните их смысл на суахили:

-piga marufuku; -vumbua; -funua; -pasha habari; -pata idhini; -tia mashaka; -teka; mamlaka; -shuhudia; mtemi; -hifadhi; -enda taratibu; -kumpa mtu usia; -kumvamia mtu; -dhoofika; -toroka gerezani; -la kiapo; -toa kauli; -susia uchaguzi; -jinyakulia ushindi; -jiuzulu; vinginevyo; -leta dhiki; -rekebisha; halali; -kera; masafa marefu; mgogoro umezuka; -pewa fursa; madhubuti; -shika usukani wa nchi; -pata uhamisho kazini; -itikia ombi; -tabiri hali ya hewa; mtu wa makamo yangu; merikebu; -zuru, zama za ukoloni; -pata ujira; -dhibiti migogoro ya mabaharia.


14. Переведите:

  1. Дж. Ньерере – один из немногих лидеров Африки, отстаивавших справедливость и человеческое достоинство.

  2. Получив диплом об окончании Университета, он полностью посвятил себя политической борьбе.

  3. Ньерере использовал партию как инструмент объединения народа в борьбе за достижение национальной независимости.

  4. Перед ним стояла задача сформировать партию нового типа, которая смогла бы успешно вести борьбу с колонизаторами.

  5. Ньерере добровольно оставил преподавательскую деятельность и с головой ушел в политику.

  6. Губернатор обвинял его в подстрекательской деятельности и грозил заключить в тюрьму.

  7. Ньерере убедил своих последователей не бойкотировать выборы в Законодательное Собрание.

  8. Кандидаты от ТАНУ участвовали в выборах и одержали победу, получив все места в Национальном Собрании.

  9. Ньерере был тверд в своей решимости защитить национальную независимость.

  10. Танзания была одной из семи стран, разорвавших отношения с Великобританией.

  11. Победив большинством голосов на выборах, Дж. Ньерере был приведен к присяге как первый президент Республики Танзания.


Msamiati

-simamia стоять за что-л. (кого-л.) mgawo (mi-) деление,

-fuzu добиваться успеха распределение

-kunjufu дружелюбный, -gombea 1) бороться

радушный, искренний за что-л., претендовать



jasiri смелый, отважный 2) быть кандидатом

jasiri (ma-) смельчак, храбрец -jiuzulu уходить в отставку

ujasiri (ед.) 1) смелость, храбрость; -tia sahihi подписывать

самоотверженность 2) риск mhariri (wa-) редактор



hiari (-) воля; волеизъявление insha (-) очерк

kwa hiari добровольно kura (-) 1) голосование

-jitolea 1) вызываться; жертвовать 2) голос (избирателя)

собой; посвящать себя чему-л. -piga kura голосовать

2) делать что-л. добровольно -apisha приводить к

-itika отзываться, откликаться присяге

-iga, -igiza подражать; -tapanya разбрасывать;

имитировать рассеивать



mchezo wa kuigiza пьеса; спектакль ufidhuli (ед.) надменность;

-sita 1) колебаться 2) внезапно дерзость

прекращать (начатое) usukani (ед.) руль



-ajiri нанимать на работу katibu (ma-) секретарь

ujira (ед.) жалованье, hila (-) хитрость, уловка

оплата труда -miliki владеть, обладать



-laumu обвинять; критиковать gavana (ma-) губернатор

mgomo (mi-) забастовка; -tisha, -tishia пугать;

саботаж угрожать



merikebu (-) корабль; судно; -dhibiti контролировать

пароход zama (-) время; эпоха



mchochezi (wa-) подстрекатель -zuka появляться, возникать

-chochea подстрекать; korti kuu верховный суд

провоцировать -churupuka ускользать;



-nyakua выхватывать, вырывать вырываться

makamo, makamu (мн.) возраст mgogoro (mi-) 1) конфликт

-tabiri предсказывать; предрекать 2) кризис

masafa (мн.) расстояние, hotuba (-) речь; выступление

дистанция -tema резать, рубить;



-susa, -susia бойкотировать колоть

uhamisho (ед.) 1) выселение, ссылка idara департамент; отдел

2) перевод (на другую работу) fursa (-) возможность; шанс



* * *

Урок 19. Somo la kumi na tisa
Грамматика

Служебные слова kunako, panapo, mnamo в функции предлогов.


Служебные слова kunako, panapo, mnamo, состоящие из субъектного приглагольного согласователя одного из локативных классов, недостаточного глагола -na и локативного форманта -po-, -ko-, -mo-, могут выполнять функцию самостоятельных предлогов, обозначающих временные понятия:

kunako mwaka huu “в этом году”;

panapo mwezi uliopita “в прошлом месяце”;

mnamo wiki hii “на этой неделе”;

mnamo saa kumi “в 4 часа”.

Следует иметь в виду, что слово mnamo имеет чисто временное значение, а слова kunako и panapo могут выполнять функции предлогов, имеющих пространственное значение, и в этом смысле они близки по значению к предлогам kwenye, katika и др. Например:

Napenda kupumzika kunako (kwenye) milima “Я люблю отдыхать в горах”;

Tulikutana panapo (katika) kituo cha basi “Мы встретились на автобусной остановке”.

Слово panapo имеет свою отрицательную форму – pasipo или pasina. В этом случае оно выступает в функции русского предлога “без”:

pasina sababu “без причины” (сравните: bila ya sababu);

pasipo maji “без воды” (сравните : bila ya maji).
Mazoezi

1. Дайте эквиваленты на суахили, употребив все возможные варианты перевода предлогов:

в этом году; в 5 часов вечера; в прошлом месяце; на озере; в другом городе; в конце века; у моря; на остановке; в утренние часы; в половине седьмого; без четверти 11; на вершине горы; без цели; без радости; без образования.


BIASHARA YA WATUMWA

Mwanzo wa kukutana kwa babu zetu na watu waliotoka nchi za ng’ambo unaonyesha kuwa ulikuwa katika karne ya kumi na tatu. Lakini inawezekana jambo hili lilitokea hata karne mbili au tatu kabla ya karne ya kumi na tatu. Sehemu ambayo wageni na wananchi walianza kukutana ilikuwa Kilwa ambayo inaonyesha* ilikuwa imekwisha twaliwa tangu karne ya kumi, labda hata mapema zaidi. Kilwa ulikuwa mji wa biashara iliyositawi. Vitu vilivyokuwa vinauzwa kwa kupelekwa nchi za ng’ambo vilikuwa pembe za ndovu, dhahabu na lulu. Biashara ya watumwa pia ilikuwa inaendeshwa Kilwa, hasa na Waarabu ambao walikuwa wamekwenda huko kwa madhumuni hayo. Watumwa walikuwa wanaletwa mwambao toka bara kama vile pembe za ndovu.

Waarabu walikuwa hawaendi bara mpaka karne ya kumi na tisa. Kwa hiyo pembe za ndovu na watumwa hao waliletwa mwambao na wananchi wa makabila fulani fulani, kutegemea nani kati ya makabila hayo alipigwa vita na wenzie na nani alimshika mwingine mateka. Pembe za ndovu na watumwa hao waliletwa mwambao. Waarabu walipewa vitu hivyo na watu hao kama zawadi. Waarabu waliwapa wananchi waliowaletea pembe za ndovu na watumwa zawadi za nguo, shanga, bunduki, waya za shaba, na kadhalika.

Basi utumwa ulikuwa umekwisha kuwa biashara ya maana ingawa biashara ya pembe za ndovu ilikuwa ni ya maana zaidi bado. Usakaji wa watumwa haukuanza mpaka labda sehemu ya mwisho ya karne ya kumi na nane wakati ambao koloni za Wafaransa zilipopata faida sana katika biashara hiyo. Baada ya hapo biashara ya watumwa ilianza kukolea sana katika sehemu za bara ya Kilwa. Waarabu walipata haja zao za watumwa toka kwa makabila yaliyoteka watu katika vita zilizokuwa zikipiganiwa baina ya makabila mbali mbali ya sehemu hizo. Kwa sababu hiyo vita baina ya makabila zilizidi kufuatana na mahitaji ya Waarabu juu ya watumwa.

Ni vigumu kusema kwa uhakika jinsi biashara hii ilivyokuwa inaendeshwa lakini yaonyesha* kwamba jinsi jambo lenyewe lilivyozidi kuwa ni la kawaida katika enzi hizo ndivyo utumwa ulivyoanza kuwa kama biashara ya kawaida. Matokeo ya biashara hii ya kishenzi yalikuwa mabaya sana na ya kusikitisha. Idadi ya wananchi wa sehemu za bara ya Kilwa ilipungua sana hata ikawa ni lazima, katikati ya karne ya kumi na tisa, wasakaji watumwa wasafiri siku kumi na nane hivi kabla ya kuvifikia vijiji walikoweza kupatikana watumwa.

Wananchi ndio waliokuwa wakitumiwa na Waarabu wachukue pembe za ndovu kuzipeleka hadi mwambao. Wachukuzi wa pembe hizo, kwa jumla, walikuwa wapagazi wa kuajiriwa. Lakini punde si punde idadi ya wapagazi ilipungua sana. Vijana wenye afya walikuwa wanatakiwa na makabila yao katika kazi ya ulinzi na kupigana vita na makabila mengine. Waarabu walihitaji sana wachukuzi wa pembe zao za ndovu na kwa sababu ya ukosefu ulioelezwa, Waarabu walianza kushika wananchi na kuwashurutisha wawachukulie pembe zao za ndovu. Wananchi wengi waliokamatwa hivyo waliteswa sana na wengi waliuawa au kufa katika misafara ya kwenda mwambao. Lakini inasemekana kuwa, kwa jumla, Waarabu walipata faida sana walipowauza hata hao watumwa wachache walioweza kufika mwambao.

Ni jambo la kushangaza kuwa Waarabu hao waliofanya biashara ya watumwa na pembe za ndovu hawakushughulika na mambo ya utawala. Lakini inafahamika kuwa wachuuzi wachache waliokata shauri kubaki nyuma na kuanza kuishi nchini walikuwa bado wanamtambua Sultani wa Unguja kama Sultani wao. Katika mwambao, Sultani alikuwa ameweka maafisa wake wa forodhani na kwa hiyo inajulikana kuwa yeye ndiye mtawala wa sehemu hizo.

Ni vigumu kusema kwa uhakika juu ya maafa yaliyoletwa na utumwa kwa wananchi kwa sababu mambo mengi ambayo tungesema yalitokana na uovu wa utumwa, yalikuwa ni matunda ya vita baina ya makabila mbali mbali pia. Vita maarufu ambazo zinajulikana kuwa zilileta maafa makubwa kwa wananchi ni kama zile za baina ya Wahehe na Wangoni huko kusini mwa nchi yetu. Mateka waliokamatwa na makabila mbali mbali katika vita kama hizo ndio waliofanywa watumwa wa kwanza wa Waarabu.

Pongezi kubwa ya kukomesha biashara ya watumwa ni budi** itolewe kwa Waingereza. Wao ndio walioanza kuishambulia biashara hiyo na wakapitisha sheria ya kuzuia biashara ya watumwa mwaka 1807. Toka hapo Waingereza walijaribu bila kupumua, na kwa moyo wote, kukomesha biashara hiyo ya aibu ingawa mara kwa mara katika jitihada zao ilikuwa lazima kufikiria hali ya uhusiano wao na mataifa mengine ambayo yalikuwa bado yanapendelea biashara hiyo iendelee. Lakini mwishoni mwa karne ya kumi na tisa juhudi zao zilianza kutoa matunda ya ushindi. Masoko yote ya watumwa yalifungwa na meli zilizokuwa zikichukua watumwa zilizuiwa zisipite katika njia fulani. Hata hivyo utumwa haukukomeshwa nchini mpaka Wadachi walipoanzisha serikali yao Tanganyika.
Maelezo

* Глагол -onyesha “показывать” в неопределенно-личной форме (inaonyesha; yaonyesha) может выполнять функцию вводного слова со значением “очевидно”, “видимо”, “судя по всему”.

** Существительное budi “избавление”, “выход” в современном языке суахили все чаще стало употребляться как синоним слова lazima “необходимость” для выражения модального значения, например:

Ni budi aende huko “Ему надо пойти туда”; (Ni) budi tuimalize kazi hii kwa haraka “Нам необходимо закончить эту работу быстро”.

Напомним, что слово budi передает значение долженствования в сочетании с отрицательной конструкцией глагола -wa na “иметь”: hana budi kwenda “он должен пойти”; hatukuwa na budi kumaliza “нам надо было закончить”.
Mazoezi

2. Переведите, используя выражения из текста:

судя по всему; город с процветающей торговлей; с этой целью; в зависимости от того, кто кого взял в плен; торговля бивнями все еще была на первом месте; захват рабов; они на этом сильно наживались; дела резко пошли в гору; в соответствии с потребностями; то, как велась торговля невольниками; в те времена; результаты оказались плачевными; постепенно; наемные носильщики; их заставляли работать; они подвергались тяжким мучениям; его признавали в качестве правителя; таможенные чиновники; страдания, причиненные народу; огромное зло; захваченные пленники; ему надо отдать должное; приняли закон о запрещении работорговли; позорный бизнес.


3. Замените предлог kwa направительной формой соответствующего глагола. Не забудьте поменять порядок слов там, где это необходимо:

1. Plau nzuri ya kuku iliyopikwa kwa mume. 2. Visa vilivyoelezwa kwa watoto. 3. Picha zinazochorwa kwa ajili ya rafiki. 4. Barua zilizoandikwa kwa mpenzi. 5. Nyimbo zitakazoimbwa kwa watalii. 6. Muziki uliopigwa kwa nyinyi. 7. Pesa zilizotengwa kwa jumuiya. 8. Teksti zinazotungwa kwa wanafunzi. 9. Vyombo vitakavyoletwa kwa mafundi. 10. Milango iliyofunguliwa kwa wageni.


4. Переведите, используя конструкцию с глаголом в направительной форме:

1. Праздник, устроенный в клубе для молодежи, был очень веселый. 2. Деньги, отправленные для новой партии, потерялись в дороге. 3. Товар, проданный вам на прошлой неделе, оказался нелегальным. 4. Песни, исполняемые для высокого гостя, рассказывают о национальных героях этой страны. 5. Еда, приготовленная для вас еще вчера, уже испортилась, так как было очень жарко. 6. Вещи, купленные для меня на рынке, отправьте в деревню моим родственникам.


5. Переведите следующие словосочетания, используя служебное слово -enye:

очень утомительный рассказ; интересные иллюстрации в книге; устрашающий голос; радостные мысли; вопрос, вызывающий удивление; закон, запрещающий политическую деятельность; цены, растущие вверх безостановочно; вечно почитаемые герои; страна, привлекающая массы туристов; грустная история; избираемые депутаты; быстро распространяющиеся новости; счастливый барабанщик; умный бухгалтер; самодостаточная нация; любимый десерт; счастливчик; удачливый бизнесмен; самоотверженные доноры.


6. Переведите текст:

Kibanga ampiga mkoloni

Zama za ukoloni palitokea mzungu mmoja. Mzungu huyo hakuwa mtu mwema. Alikuwa mkali na katili sana. Kwa ajili ya ukatili wake watu walimwita Mkoloni. Wananchi wote walimchukia sana popote pale alipokwenda.

Mzungu huyo alikuwa bwana shamba. Alikuwa na bakora ambayo kila alipokwenda kukagua mashamba, alikuwa na bakora hiyo mkononi. Alipendelea sana kuitwa ‘Bwana Mkubwa’. Mkoloni huyo alifurahia sana kupiga watu. Aliwapiga watu waliposhindwa kupalilia mashamba. Aliwapiga pamba yao ilipokuwa chafu. Aliwapa taabu sana.

Katika kijiji kimoja alikuwapo mzee mmoja aliyeitwa Kibanga. Mzee huyo alikuwa mwenye nguvu, hodari na shujaa. Alikuwa fundi wa mieleka. Ingawa alikuwa mwenye nguvu, alikuwa mpole. Hivyo watu wa kijiji hicho walimpenda na kumtegemea kuwaongoza vitani.

Siku moja yule mzungu alifika kijijini kukagua mashamba ya mihogo. Jumbe pamoja naye wakatembelea mashamba. Kwa bahati mbaya mwaka ule haukuwa na mvua ya kutosha. Kwa hiyo mihogo haikusitawi. Kila wakati yule mzungu alipotazama mashamba alitikisa kichwa na kufoka. Mwisho akamwagiza jumbe kuitisha mkutano wa watu wote wa kijiji. Waliporudi kijijini jumbe akapiga mbiu. Watu wote wakakusanyika. Walipofika tu, yule Mkoloni akaanza kuwatukana, akawaambia, ‘Nyinyi watu weusi ni wavivu sana. Hamfanyi kazi sawa sawa. Mashamba yenu ni mabaya sana.’ Jumbe akataka kumjibu ili kumweleza kwa nini mihogo haikusitawi. Kabla hajamweleza yule mzungu alimrukia na kumpiga kofi. Kisha akasema, ‘Sitaki kujibiwa na wewe, mvivu wa wavivu.’ Watu wote wakakaa kimya. Hakuna aliyeweza kufanya kitu.

Kibanga akajitokeza, akasimama. Akamtazama yule Mkoloni kwa dharau sana. Kisha akamwuliza, ‘Kutuita sisi wavivu ndiyo nini? Na kumpiga umbe wetu mbele yetu, maana yake nini?’

Kabla ya kumaliza kusema, Mkoloni aliamka kitini kwa hasira, akataka kumpiga Kibanga. Alishika bakora yake mkononi. Akasema, ‘Nitakuadhibu vibaya kima we! Unajifanya kuwa shujaa? Huwezi kucheza na bwana mkubwa. Nitakupiga, kisha utakwenda jela miezi sita.’ Lakini Mkoloni hakuwahi kumwadhibu Kibanga. Aliadhibiwa yeye. Kabla ya kumfikia, Kibanga alimpiga chenga. Kisha akamrukia, akamnyang’anya bakora yake. Akaitupa, ikaokotwa na vijana, wakaificha.

Kibanga alimshika yule mzungu akamwambia, ‘Wewe umezoea kutoa amri kila siku, lakini leo utashika adabu, mbwa wee!’ Papo hapo alimnyanyua juu na kumbwaga chini, puu! Yule Mkoloni akaumia sana. Kabla ya kuamka, Kibanga alimwinua tena na kumbwaga chini kama furushi la pamba. Akamkalia.

Hapo yule Mkoloni akawa hana la kufanya. Bila ya bakora alikuwa hana nguvu. Akaomba radhi akilia, ‘Samahani! Naumia! Nihurumie! Sitafanya tena hivyo.’ Kibanga alimjibu kwa dharau, ‘Sikuachi mbwa wee! Leo utaona cha mtema kuni! Ulijiona una nguvu. Leo nitakutengeneza.’

Wazee wakamshika Kibanga na kumwomba asimpige tena. Akamwacha. Kwa shida yule Mkoloni alijivuta kwenda hemani. Alikuwa amejaa vumbi huku damu zikimtoka. Wazee wengine wakamfuata nyuma. Walinyamaza kimya, wakimhurumia. Lakini vijana walifurahi sana. Baadaye waliimba wimbo wa kumsifu Kibanga.

Jioni yule Mkoloni aliomba radhi kwa wazee. Mzee mmoja akasimama na kumwambia, ‘Umefanya vizuri kuomba radhi, nasi tunaipokea. Lakini tangu leo usijivunie ubwana. Jivunie utu. Nyinyi wakoloni mna kiburi. Mnatudharau. Kama ungetuuliza tungekuambia kwa nini mihogo haikusitawi. Haya yote yamekupata kwa sababu ya kiburi chako.

Baada ya hapo wazee wakamsamehe, lakini hawakumpa bakora yake. Ikabaki nyumbani kwa Jumbe.


7. Дайте русские эквиваленты:

-chukia mtu; mtu mkali na katili; -kagua mashamba ya mihogo; -palilia mashamba; -mpa mtu taabu; fundi wa mieleka; -wa mpole; -tikisa kichwa na kufoka; -agiza kuitisha mkutano; -piga mbiu; -piga mtu kofi; -tukana sana; -tazama kwa dharau; -jitokeza; -sema kwa hasira; -adhibu vibaya; -mpiga chenga adui; -nyanyua mzigo; -nyanyua mkono; -bwaga chini; -omba radhi; -ona cha mtema kuni; -mhurumia mtu; -jivunia ubwana; -jivunia utu; -ona kiburi; mtesa mtu mpaka afe; -shurutisha kwa nguvu; mgogoro umekolea; sheria za kishenzi; -sababisha maovu.


8. Перескажите в лицах историю из текста “Kibanga ampiga mkoloni”.


9. Переведите:

  1. Судя по всему, еще в 13-ом веке предки современных танзанийцев начали продавать заезжим торговцам бивни слонов, золото и жемчуг для отправки в заморские страны.

  2. Местное население поставляло арабам невольников и взамен получало от них подарки в виде тканей, бус, ружей, медных проводов и другой утвари.

  3. Результаты работорговли, которая велась варварским образом, были очень плачевными, поскольку население района Килвы очень сократилось.

  4. Охота за рабами достигла наивысшего расцвета в конце 18-го века, как раз в то время, когда работорговля стала очень выгодной для французских колонизаторов.

  5. Арабы испытывали острую нужду в носильщиках, поэтому они хватали крепких мужчин из числа местного населения и заставляли их работать на себя.

  6. Пленники, которых забирало племя, победившее в междоусобной войне, становились первыми, кого продавали арабам как товар.


Msamiati

lulu (-) жемчуг; жемчужина -nyanyua поднимать

waya (-; nyaya) провод; кабель uovu (ma-) вред; зло

mwambao берег (морской), mpagazi (wa-) носильщик

побережье (груза на голове, плечах)



-kolea накаляться (прям. и перен.) forodha (-) таможня

mshenzi (wa-) дикарь, варвар mieleka, miereka (-) борьба

-a kishenzi дикий, варварский (спортивная)

-shurutisha заставлять, -adhibu наказывать

принуждать mbiu (-) сигнальный рог



-tesa мучить, причинять боль -piga mbiu оповещать

teso (ma-) страдание, боль; пытка -piga chenga ускользать;

maafa (мн.) беда, несчастье; уклоняться

катастрофа kiburi (vi-) высокомерие,



-ona cha mtema kuni узнать, надменность

почем фунт лиха (идиома) pongezi (-) 1) поздравление



-omba radhi просить 2) приветствие

прощения -tukana 1) ругать,



-foka 1) бить ключом, оскорблять 2) ругаться,

пениться 2) извергаться браниться

3) кипеть негодованием -bwaga сбрасывать,

-piga kofi (ma-) давать пощечину сваливать (вниз, на землю)

-jitokeza 1) показываться, -saka гнаться, преследовать;

появляться 2) выходить вперед вылавливать



* * *

Урок 20. Somo la ishirini

(marudio)
1. Переведите текст:

KILWA KISIWANI

Kilwa Kisiwani ni moja ya miji mingi ya zamani ambayo ni kivutio cha watalii na watafiti wa mambo ya kale. Kilwa Kisiwani imeendelea kubeba majengo ya zamani yakiwa na historia ya zaidi ya miaka 9,000 iliyopita.

Kwa sasa, majengo hayo ni magofu, yakiwa yamebaki kuwa sehemu ya watalii na watafiti kujionea jinsi jamii za watu wa zamani zilivyoishi, sambamba na zilivyokuwa zikiendesha maisha ya kila siku.

Kilwa Kisiwani ilianza kupata umaarufu wake katika karne ya tisa, baada ya kununuliwa na mfanyabiashara Ali bin Al-Hassan kutoka kwa wazee wa jadi waliokuwa wakiimiliki.

Mara baada ya kununua Kilwa Kisiwani, mfanyabiashara huyo kutoka mashariki ya mbali, alijenga himaya kubwa ya kiuchumi katika ukanda wa pwani ya Afrika ya Mashariki na miji ya kando kando ya bahari ya Hindi.

Biashara kubwa ambazo ziliendeshwa na himaya hiyo zilikuwa zile za utumwa, pembe za ndovu, nguo, tende, dhahabu na shaba, vitu ambavyo viliuzwa katika masoko ya uarabuni.

Katika karne ya 13 chini ya utawala wa familia ya Mahdali Kilwa Kisiwani ilikuwa maarufu na umaarufu wake uliifanya ifahamike katika nchi nyingi za kusini na kaskazini mwa bara la Afrika.

Umaarufu wa Kilwa Kisiwani ulimfanya mtafiti Abu Abdullah Ibn Battuta kuitembelea mwanzoni mwa mwaka 1330, ambapo aliamua kuwekeza katika shughuli mbalimbali za biashara ikiwa ni pamoja na kushawishi wafanyabiashara kutoka nje kuja kuitembelea ili wawekeze pia.

Utawala wa Kiarabu katika kisiwa hicho ulikoma kwa muda katika karne ya 14 baada ya Vasco da Gama kufika kama mtafiti na baadaye kuwashawishi Wareno wenzake kuvamia ili wawekeze. Mkakati huo ulipofanikiwa, Kilwa ilijikuta mikononi mwa Wazungu kwa mara ya kwanza.

Wareno walikitawala na kufanikiwa kuhamisha kiasi kikubwa cha madini na vitu vya asili kama shanga na mavazi vilivyokuwa vikiuzwa kwa ajili ya matumizi ya miji iliyochipukia kusini mwa Afrika.

Hata hivyo, utawala wao haukudumu sana, kwani mwanzoni mwa mwaka 1512 Waarabu wakiwa na jeshi kubwa walikivamia tena na kukichukua.

Wakati wa utawala wao, Waarabu waliurejeshea hadhi iliyokuwa imepotea. Mwaka 1784, mtawala wa Oman alikichukua kisiwa hicho na kile cha Zanzibar kwa nia ya kutanua biashara zake, ambapo aliweka utaratibu mpya wa kulipa kodi na ushuru kwa watu na wafanyabiashara waliokuwa wakiingia na kutoka.

Katika juhudi za kujiimarisha, aliwatumia Wafaransa kumjengea kituo cha kijeshi na ngome kubwa aliyoifanya kuwa mahali pa kujificha na kuhifadhi dhana za kijeshi.

Historia ya kisiwa hicho inaonyesha kuwa, kati ya mwaka 1881 hadi 1918 kilikuwa chini ya uangalizi wa Ujerumani, sambamba na maeneo mengine ya Tanzania bara ambapo Zanzibar ilibaki mikononi mwa Sultan wa Oman aliyekuwa na makazi yake Unguja.

Hadhi ya Kilwa Kisiwani ilipotea ghafla mara baada ya Wajerumani kuondoka. Inaelezwa kwamba kutokana na historia mbaya ya mauaji iliyoendeshwa na watu hao, haikuwaumiza vichwa Waingereza kukiendeleza kisiwa hicho.

Badala yake, waliweka silaha nzito katika pwani ya Kilwa na kuzielekeza kisiwani hapo ili kuwaogopesha wavamizi. Majengo na vitu vilivyoko huko viliendelea kuharibika kadiri siku zilivyokwenda.

1   ...   10   11   12   13   14   15   16   17   ...   25


Verilənlər bazası müəlliflik hüququ ilə müdafiə olunur ©atelim.com 2016
rəhbərliyinə müraciət